Watanzania tunaimba viwanda mdomoni, Kenya wanajenga viwanda

Watanzania tunaimba viwanda mdomoni, Kenya wanajenga viwanda

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kwa vile awamu hii imejipambanua kwa sera ya viwanda, nilitegemea kuona serikali ya Tanzania ikiwawezesha wawekezaji wa ndani na wa nje kuanzisha viwanda vya aina hii.

Pamoja na vurugu zao wenzetu wakenya wameweza vipi, kwa nini sisi tuendelee kujidanganya na kuwadanganya wananchi kuwa ukiwa na vyerehani vinne ndiyo maendeleo ya viwanda.

FB_IMG_1523181492690.jpg
FB_IMG_1523181484682.jpg
FB_IMG_1523181476457.jpg
FB_IMG_1523181466419.jpg
FB_IMG_1523181456156.jpg
 
Kaka Quinine sisi hatuimbi Viwanda, bali tunajenga viwanda, lengo letu na Kenya ni tofauti sana, Sisi mbiu yetu kuwa vyerahani vinne ni viwanda tofauti na wenzetu wanaowaza big factory

Kupata uwekezaji mkubwa kama huo ni lazima Lobbying ya nguvu ifanyike, na hao Big company kama Peugeot, Iveco, Ashok Leyland nk kuwapata mabosi wake ni level ya Marais, sio Mwijege akanegotiate na Iveco, JK alijishusha kwa Dangote na matokeo tukayaona,
Kama raisi hataki kutoka nje kuongea na hao Big companies unategemea Big project kutoka wapi?
 
Watuambie na taxi holiday incentIves walizotoa! All of them hawatalipa kodi kwa miaka kati yards 15 mpaka 30. Magufuli asiruhusu magari haya yauzwe Tanzania maana kuna makampuni yamekubali kuwekeza na yatalipa kodi.
 
FB_IMG_1523185344285.jpg
FB_IMG_1523185392314.jpg
FB_IMG_1523185403080.jpg
FB_IMG_1523185412119.jpg
FB_IMG_1523185425485.jpg
Embu fanyeni kuswipe muone matusi ya wakenya. Huku kwetu tunapigiwa kelele za viwanda usiku na mchana alafu viwanda vinafunguliwa Kenya. Kenya na mavurugu yao yoooote ya uchaguzi Ila wawekezaji wanaona bora wakafungue maviwanda Kenya kuliko TZ tunapojifanya tuna amani. Kama amani ndio kila kitu Kenya na Tz Wapi kuna amani? Mbona wawekezaje wanachagua huko kusikokuwa na amani wanatuacha sisi mabingwa wa amani?? Tatizo ni moja tu Nani akawekeze kwenye nchi yenye rais kichaa aisie eleweka kesho ataamkaje na kuamua kukamata makontena yao bandarini na kuwadai matrilioni ya kodi?? Nani aje kuwekeza kwenye nchi ambayo hawachelewi kuitwa majizi?? Tatizo ni tuna Rais kichaa.
.
.
.
Nimewaza hivi siku kiwanda kimoja tu kikubwa kama hivi vinavyofunguliwa Kenya kingefunguliwa TZ, uwiiiiiiiiiiiii mama yangu nahisi nchi ingesimama mwezi mzima. Uwiiiiiii tungetangaziwaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka tukome.Mpaka watoto waliondani ya matumbo ya mama zao wangesikia matangazo ya Rais kuleta kiwanda cha Nissan Tanzania.... Siku ya ufunguzi ndo angechamba mpaka. Maana sasa hivi anaenda kuzindua UKUTA ila tunaonyeshwa live na mineno inamtoka utasema kalewa sasa imagine siku alete moja tu ya viwanda hivi vilivyoko Kenya si ataharisha??
 
Back
Top Bottom