Kipondo Cha ugoko
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 878
- 1,511
Tanzania ndo inchi isiyokua na direction,nchi haina malengo haina mipango. Kila kitu kinaendeshwa kisiasa siasa tu.Tutanyanyaswa hadi akili itukae.
Tutanyanyaswa hadi tujitambue.
Tutanynyaswa hadi Elimu itakapotusaidia.
Nchi iko gizani tuko kimya.
Kazi maofisini zinafanyika kwa kudra ya Tanesco, wakiamua wanakata, au wakupe umeme kwa muda wao.
Tuna Rais ambaye hakemei huu ujinga, hachukui hatua za dharura.
Rais alipswa:
Aachane na ziara nje ya nchi kwa hali ya dharura iliyopo nchini.
Tatizo la umeme linapaswa kuchukuliwa kama vile taifa limevamiwa tuko vitani.
Taifa lingeweza hata kusitisha SGR na miradi mingine kwa muda tupate umeme thabiti.
Wauze hata ndege nusu au zote tuondokane na aibu ya umeme.
Wasitishe hata ziara za hovyo za vyama vyote ruzuku ya vyama vyote iingizwe kwa umeme kama mkopo wa ndani.
NANI ATALETA MTAJI WAKE KUFANYA UWWKEZAJI MKUBWA NCHI YA GIZA?
Rais anashauriwa na nani?
Hata kama hakuna mshauri yeye haoni?
Kwanini ccm msimtoe huyu rais mtuletee mtu mzalendo wa kweli?
INauma sana
Inaudhi sana
Inakera sana
Inasikitisha sana
Inachefua sana.
Halafu badala ya kuchapa kazi uache legacy unatufuta chawa wakusifie hata ukichecheua na unawalipa aah.
Kwanini Tanzania tu?
Kwanini aibu hii?
Kwanini mateso haya?
Lini Mungu ataamua ugomvi?
..................
Note: wewe unayesoma na husemi neno likupate jambo
Kubwa zaidi watawala washawaona Watanzania ni hamnazo so wanajifanyia watakavyo wakijua hamna watu wa kuhoji na kushikia bango mambo ya muhimu kama ukosefu wa umeme. Watanzania wako bize na misomisondo na hivyo ndivyo CCM wanavyopenda.