Na kazi inaendelea au ni maneno tu!
Mkuu 'Hakimu Mfawidhi', mada yako ni muhimu sana, na maswali uliyouliza yanahitaji majibu.
Hivi kuna njia zipi zinazotambuliwa na serikali ambazo zikitumiwa inalazimu wahusika watoe majibu?
Kwani serikali kuwajibika kwa wananchi maana yake ni nini, si ni pamoja na kuwapa wananchi taarifa sahihi mara wanapotaka taarifa hizo?
Haya maswali uliyouliza humu yameulizwa mara kwa mara na watu mbalimbali lakini hayapati majibu sahihi kutoka kwa wahusika. Kwa hiyo inabaki kurudiarudia tu maswali hayo hayo, na kila anayekuja kuchangia kwenye mada kama hii yako anakuja na majibu kivyake anavyojisikia mwenyewe.
Kwa mfano: juzi hapa Zitoo katoa maoni yake juu ya swala kama hili hili, likihusiana na mgodi wa Kabanga Nickel kule Ngara, kwamba mgodi huo ni wa Barrick kupitia mgongoni.
Kaeleza kwamba hiyo sheria inayozungumzia umiliki wa serikali, ile asilimia 16, kwamba hiyo ni gheresha tu, kwa maana asili mia hiyo ni umiliki wa kampuni, na kwamba siyo umiliki wa mgodi! Hakuna aliyekanusha au kusahihisha taarifa hiyo kama ni kweli ama sio kweli.
Haya unayoyaweka hapa yanaumiza roho sana kwa watu wanaoyafuatilia. Inaumiza sana kama kweli mali asili zetu zinageuzwa na kuwa mali za watu wengine na sisi kubaki tukiambulia masalia, eti tunafaidika kwa kodi, mrahaba na ajira ambazo hata haziwanufaishi watu wengi. Inaumiza sana.
Sasa angalia, hii mada umeiweka hapa, na hutapata jibu lolote la maana. Inasikitisha sana.