Wameghakamia utafiti,uchimbaji na uchakataji wa hyo gesi yan wabongo tunataka gesi iwe mali yetu kwa zaidi ya 30% kwa kutochangia chochote turidhike tu na hyo 16%
Mkuu 'Hakimu Mfawidhi', mada yako ni muhimu sana, na maswali uliyouliza yanahitaji majibu.
Hivi kuna njia zipi zinazotambuliwa na serikali ambazo zikitumiwa inalazimu wahusika watoe majibu?
Kwani serikali kuwajibika kwa wananchi maana yake ni nini, si ni pamoja na kuwapa wananchi taarifa sahihi mara wanapotaka taarifa hizo?
Haya maswali uliyouliza humu yameulizwa mara kwa mara na watu mbalimbali lakini hayapati majibu sahihi kutoka kwa wahusika. Kwa hiyo inabaki kurudiarudia tu maswali hayo hayo, na kila anayekuja kuchangia kwenye mada kama hii yako anakuja na majibu kivyake anavyojisikia mwenyewe.
Kwa mfano: juzi hapa Zitoo katoa maoni yake juu ya swala kama hili hili, likihusiana na mgodi wa Kabanga Nickel kule Ngara, kwamba mgodi huo ni wa Barrick kupitia mgongoni.
Kaeleza kwamba hiyo sheria inayozungumzia umiliki wa serikali, ile asilimia 16, kwamba hiyo ni gheresha tu, kwa maana asili mia hiyo ni umiliki wa kampuni, na kwamba siyo umiliki wa mgodi! Hakuna aliyekanusha au kusahihisha taarifa hiyo kama ni kweli ama sio kweli.
Haya unayoyaweka hapa yanaumiza roho sana kwa watu wanaoyafuatilia. Inaumiza sana kama kweli mali asili zetu zinageuzwa na kuwa mali za watu wengine na sisi kubaki tukiambulia masalia, eti tunafaidika kwa kodi, mrahaba na ajira ambazo hata haziwanufaishi watu wengi. Inaumiza sana.
Sasa angalia, hii mada umeiweka hapa, na hutapata jibu lolote la maana. Inasikitisha sana.
Mkuu nakumbuka hii imetokana na sheria mpya ya madini kama ulivyosema ingawa sina hakika kama tulifikia majadiliano na makampuni ya gesi, naona nguvu nyingi zilielekezwa kwenye madini mengine kama dhahabu na Almasi.
Mkuu Hakimu Mfawidhi , sheria ilisema extractive industry yote!, chochote kinachochimbwa kwenye ardhi ya Tanzania, 16% ni mali ya Watanzania ambao ndio wenye ardhi hiyo. Kwangu tatizo la sheria hii ni sheria mpya, wakati inanatungwa, tayari tulikuwa na mikataba ya zamani ya umiliki wa asilimia 100% chini ya 100% kwa mwekezaji.
Baada ya Bunge letu kutunga sheria mpya ya madini, niliuliza
Wanabodi, Kwanza naunga mkono marekebisho ya sheria hizi kufanyika, kwa sababu yanafanyika kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na maslahi ya Watanzania badala ya maslahi ya wawekezaji, japo siungi mkono miswada hii kuletwa kwa hati ya dharura kwa sababu tayari kuna mikataba mingi iliyopo...
www.jamiiforums.com
Wiki iliyopita, nimezungumza na Waziri Dotto Biteko, amekiri kuwa serikali ina negotiate na wawekezaji na wote wamekubali kutekeleza sheria hii mpya ya 16% free carried shares
Elimu ya shares inahitajika sana Tanzania. Hizo class B shares ni shares kamili zina hadhi sawa na class A shares, the only thing ambacho hazina ni fixed and non transferable, yaani haziwezi kuongezeka wala kuuzwa. Huku kutokujua tofauti ya class A shares na class B, sikulaumu wewe, hata wachumi wetu wa UDSM akiwemo Zitto , hizi class b shares alikuwa hazijui, na alipandisha bandiko hili Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho
na mimi ambaye sio mchumi bali muelimishaji umma, nilijitolea kumuelimisha hapa.
Wanabodi, Huu ni muswada wa makala ya gazeti. Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazungumzia kazi ya vyama vya upinzani...
www.jamiiforums.com
Na kwa faida ya wale wasio na time to follow links, naomba nilirudie lile darasa Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.
Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.
Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.
P
Mimi Nimejibu: Hili la hisa za daraja B ni kweli lakini sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Hizi hisa aslimia 16 za Tanzania, ni free carried shares, tumepewa bure, na kote free carried shares huwa haziuzwi ila sii kweli kuwa hazina voting rights. Pia sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Naomba hapa ikumbukwe, shares zinazouzwa ni shares za Acacia zinazo trade kwenye London Stock Exchange tuu, hata yale mambo ya PUSU ni mambo yao, sijasikia lolote kuhusu shares za Acacia zinazo trade kwenye DSE, hivyo business ya hisa za Acacia ndani ya DSE zinaendelea as usual.Hata baada ya sale kukamilika, hivyo kampuni mpya italazimika kuuza 30% ya hisa zake kwenye DSE na Watanzania wenye fedha, watakuwa free kununua hisa hizo kwenye soko.
Tukija kwenye voting rights, sii kweli kuwa Tanzania hatuna voting rights, bali ni kawaida kwa free shares zote hazina voting rights ya pro rata ya share to shares bali tuna voting rights za block shares. Sisi Tanzania wenye free carried shares za 16%, serikali yetu iteteua mjumbe mmoja wa bodi ambaye ni Mtanzania, ataingia na kuwa mjumbe wa bodi ya hiyo kampuni mpya, kwa zile asilimia 16% za shares zetu na ndani ya kikao cha bodi, atakuwa na voting righs za kupiga kura 1 as a block vote kuwakilisha zile shares 14, wakati wajumbe wengine wa bodi, watakaowakilisha zile subscribed shares za asilimia 84%, wanatakuwa na voting rights ya votes 84 kwa uwiano wa share to shares votes pro rata according to shares subscription. Hivyo ndani ya bodi ya hiyo kampuni Mtanzania atakayeingia humo, atakuwa anapiga kura moja kuwakilisha the block ya zile shares zetu 16 za bure, na katika mgao wa faida, sii kweli kuwa tutapata mgao baada ya wale wengine, huu ni uongo!, Tanzania tunagaiwa mgao sawa kabisa wa faida kwa mujibu wa shares hizo.
Kwa wasio jua kuhusu shares za group A na group B shares za group A ni shares za watu walio invest kwa kutoa fedha zao kununua shares, yaani subscribed shares, na shares group B ni shares za heshima, shares za hisani zinazotolewa bure, shares hizi za hisani haziruhusiwi kuuzwa, wala kuwa disposed or transferred na zina block votes rights. Hili hufanyika kwa makampuni kuwapa hisa za heshima land owners, mfano UAE, hakuna foreigner anayeruhusiwa kumiliki ardhi, ardhi yote ni ya wazawa, hivyo investor akija lazima aingie ubia na wazawa mzawa anatoa land, investo ana jenga, kama alivyofanya Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!.
Mwisho wa siku Magufuli alikuwa ni mwanasiasa na sifa ya mwanasiasa kwenye kujenga hoja inayovutia ni adding elements of ‘sensationalism’ kwenye mambo asioyakubali as a way of shoking people and gaining support.
Uzuri ni kwamba wasaidizi wake vipanga walimwelewa na walikuwa wazuri kwenye kutoa ufafanuzi zaidi mbeleni (tatizo watu awakuwa wafuatiliaji tu).
Natural resources ni mali ya nchi husika hiyo tafsiri ilitolewa na UN in the 1960’s if I am correct kutokana na mgogoro wa Indonesia or some country in that region na mwekezaji wake on who own the resources (need to refresh my mind on that).
Hiyo precedence ndio msingi wa aina ya mikataba iliyotengenezwa kwenye natural resources.
Sasa basi mtu anapofanya exploration na kugundua natural resources ata kama ni mali ya nchi husika anakuwa na exclusive rights ya kurudisha hela yake na reasonable economic benefits on the find.
Maana yake nini uwezi kuamka asubuhi moja na kusema mjomba ata kama umegundua Gas/Mafuta sasa hivi tunataka kwenda wenyewe (what about his risks) ndio maana kuna stabilazation clauses kulinda mambo kama hayo; ambapo kuwatoa inabidi ulipe fidia kibao ambazo not worth it.
Moreover kugundua reserve za Mafuta/Gas is one thing kuyatoa yalipo na kuyachakata for commercial usage ni jambo lingine, kuna kujenga oil rigs, kuyapeleka kwenye refineries, kuyachakata, kuyauza and so forth with upstream and midstream business. Nchi maskini kama Tanzania aina huo mtaji but then do we need a $30 billion dollar LNG plant, maana hizo hela lazima tulipe na faida ya mwekezaji na hela yenyewe kama asilimia kubwa kakopa bank na yeye with higher interest ni shida.
Hizi ndio sababu you don’t want a clueless individual like Makamba to spearhead complicated negotiations kama hizo. Kwenye kichwa chake anawaza praise, atafute residence contributors wa Bloomberg waliopo Tanzania wamuandike how the ministers is business friendly and forward thinking he is (just an idiot).
Hivi hawa wapumbavu huwa wana fikia vipi hizo position, its beyond me.
Kwa ili JK msimsingizie it’s just how things work.
Mtu anaefanya exploration anakuwa na exlusive rights za part of economic benefits and buyouts in such contracts are not cheap especially if the reserve is immense.
Muhimu hapo ni kupata mkataba wenye faida kwa nchi.
Kwa ili JK msimsingizie it’s just how things work.
Mtu anaefanya exploration anakuwa na exlusive rights za part of economic benefits and buyouts in such contracts are not cheap especially if the reserve is immense.
Muhimu hapo ni kupata mkataba wenye faida kwa nchi.
Yeye alishindwa nini kupata huo mkataba wenye faida kwa nchi?
Una maana yeye ni kilaza kiasi hicho kiasi kwamba hakujua kuwa huo mkataba haukuwa na faida kwa nchi?
Contract ni ya muda gani kwa hao wawekezaji kurudisha gharama na kupata faida? hisa za serikali ni asilimia ngapi? ndo maana magu hakuwa na mzuka nako hadi kuangukia kwenye bwawa la stiglaz.......
Kikwete hajawahi kusaini mkataba wa maana kuhusu nchi yetu , hata hiyo bagamoyo port haitakuwa na jipya licha ya wale wapambe kudai eti rais alidangsnywa na kuwa hashauriwi vizuri
Mkuu hakuna sheria inayosema Tanzania itapata 16% na ecomic benefit; that was just exclusively for the specific contract (ata kama tulipigwa kutokana quality ya team yetu ya majadiliano given the duration to which ACCACIA and other previous have earned on those investments).
Mikataba ya natural resources inataratibu zake kibongo najua wapo wengi wanaoelewa hayo mambo mainly wizarani. Ila mtu ambae kutokana na ufafanuzi wake kwenye hayo maswala ambae unaweza sema uelewa wake auna mashaka ni Dr Mpango, timu yoyote ya majadiliano bila ya kumshirikisha ni kujipa disadvantage.
Sasa wale wanaosema upungufu wa wa umeme ni sababu ya serikali ya awamu ya tano kwa kutokutumia ges ya mtwara ili hali hasi sio ya kwetu walikuww wamelogwa
Wanabodi, Nimekutana na hii kitu, nimeisoma, sio tuu nimeshangaa, bali nimechoka, imeniacha hoi, ukisoma ukaona jinsi tunavyoibiwa rasilimali zetu, na wanaofanya tuibiwe, ni wenzetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza, mtu unaweza kupata wazimu, ukarukwa na akili, ukikamata SMG, unaweza...
www.jamiiforums.com
Hali hiyo ilikuwa zamani, lakini sasa tuna sheria mpya ya madini na extractive industry yoyote, kila kinachopatikana, asilimia 16% ni mali ya Watanzania. Yaani serikali yetu ina own 16% ya migodi yote, hivyo japo ni kweli kila kinachovunwa ni mali ya mmiliki, hivyo Watanzania ni wamiliki wa hiyo 16% ya free carried shares kwenue rasilimali zote za extractive industry.
P
Wakati wapinzani bungeni wanapinga maamuzi ya serekali kugawa gesi yetu kwa hao wawekezaji mpaka kufikia hatua ya kutoka nje ya buñge ili kuonyesha msisitizo kwa wananchi ili muungane nao kuipinga serekali na kupinga ujinga wa buñge lililokuwa na wabunge wengi wa ccm si mliwaona wajinga na mkaendelea na maisha yenu, Sasa mnatakaje?
Hii gesi ndio ile nilisikia ilitolewa bure kwa mchina ili kumuokoa prince aliekutwa na madude China.
Kwa uliyoandika hapa sishangai, japo kuna vichwa ngumu wanakomalia mradi wa LNG kwao bora uanze wapige hela, suala la kukamilika au kutokamilika kwake hawana habari nalo.
Tunaongoza kwa kuwa na majungu na mihemko bila kuwa na majibu yoyote ya kisayansi ili kulisaidia taifa letu. Kwanza lazima tufahamu wazi kuwa technologically tuko nyuma sana, pia hata mitaji ya kuwekeza kwenye miladi mikubwa ya kuvuna rasilimali zetu hatuna hivyo loop ya kukwepa mikataba ya unyonyaji ni ndogo Sana. Jaribu ufanye tafiti usilipuke na kutuhumu mtu hizi ni chuki za kijinga ili upate uelewa wa mambo kwa usahihi
Kuna mambo bado hayajawekwa sawa na yakaeleweka vyema.
Gesi inayochimbwa mtwara sio ya watanzania, ile gesi ni ya makampuni ya kigeni na sio ya Watanzania.
Ieleweke pia kwamba Gesi ile iko 18% nchi kavu na 82% majini ama baharini kwenye kina kirefu.
Ieleweke zaidi kwamba shirika la mafuta na petroli la Taifa ama TPDC wao ni watu wa kati kati ama middle man wa gesi inayozalisha umeme Tanzania.
TPDC wao wananunua gesi kutoka kwa makampuni ya kigeni yanayochimba gesi na kisha kuiuzia TANESCO, yaani makampuni yanachimba, yanapiga gharama za uchimbaji na faida yake, yanaiuzia TPDC, kisha TPDC anaweka cha juu na yeye anaiuzia TANESCO halafu TANESCO anazalisha umeme anauzia wananchi.
Kwa kiswahili chepesi ni kwamba, kwenye gesi ya mtwara TPDC ni dalali ama machinga wa gesi, yeye mwenyewe hana gesi ila kutokana na sheria za nchi, ana umiliki kidogo wa hisa kwenye hayo makampuni yanayochimba gesi. Serikali ama TPDC hawana kisima hata kimoja cha gesi, wao pia wananunua.
Hivyo basi ifahamike kwamba umeme wa gesi hautakuja kua bei Rahisi Tanzania kwa sababu gesi ina madalali ama inapitia mikono mingi na kila wakala ama dalali anaweka cha juu hadi kumfikia TANESCO na tanesco kuwafikishia walaji ambao ni wanachi.
Hivyo ifahamike zaidi kwamba gesi iliyoko kusini 90% ilishauzwa na wamakonde wakae wakijua hawana gesi pale, sio yao ni ya makampuni ya kigeni.
Na hao unaosikia wanasema uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata gesi utabadili maisha ya watanzania ama wanaita game changer huo ni uongo wa wazi kwani kiwanda hicho faida pekee ambayo tutaipata kwa Tanzania ni ajira, kodi na vitu vidogo vidogo lakini sio hasa keki ama nyama yenyewe ya gesi kwani gesi sio yetu.
Ukitaka kujua kitakachotokea kwenye gesi kwa kujenga mtambo wa LNG ni kuangalia faida tunayopata kwenye viwanda vya sukari, je tunafaidi uwepo wa bei ndogo ya sukari ama tunafaidi vitu vidogo vidogo kama ajira ya watu wachache, kodi na vitu vingine vidogo vidogo ila bei ya sukari iko juu.
Tunapeana matumaini ila ukweli ni kwamba we are fucked up.
Wakati wapinzani bungeni wanapinga maamuzi ya serekali kugawa gesi yetu kwa hao wawekezaji mpaka kufikia hatua ya kutoka nje ya buñge ili kuonyesha msisitizo kwa wananchi ili muungane nao kuipinga serekali na kupinga ujinga wa buñge lililokuwa na wabunge wengi wa ccm si mliwaona wajinga na mkaendelea na maisha yenu, Sasa mnatakaje?
Sio lazima ulete siasa chonganishi unaweza kutuwekea hapa yaliyokuwa mapendekezo ya kambi ya upinzani juu ya uvunwaji wa gesi yetu na namna yatakavyotekelezwa ili kuleta faida nchini. Nchi ni yetu wote sio kwamba wapinzani ndio wenye akili kuliko wengine hapana hata wao nibinadamu wanakosea. Acha siasa leta mawazo yako mwenyewe hili nijukwaa watu wanaweza kujifunza na kuhamasika
Yeye alishindwa nini kupata huo mkataba wenye faida kwa nchi?
Una maana yeye ni kilaza kiasi hicho kiasi kwamba hakujua kuwa huo mkataba haukuwa na faida kwa nchi?
Biashara ya natural resources ina stages zake ‘exploration’ ni first stage hayo ni makubaliano pekee ambapo makampuni yana bid kutafuta mafuta/Gas. It is very risky and expensive especially when it’s in deep sea kunakupata na kukosa.
Sasa wakipata wanakuwa na exclusive rights za ku gain economic benefit based on potential amount of reserves.
Ndio maana Dr Muhongo alipoletwa kitu cha kwanza alichofanya ni kupeleka hati ya dharura ya sheria ya mikataba ya Production Sharing Agreement (PSA) on what amount of benefit they are entitled to based on reserve after they recoup their investment.
Mpaka hapo unakuwa ushatoa exclusive rights za nani mwenye haki ya kutoa hayo mafuta uki kiuka kuna compensation kwa sababu watu washachukua risk na walitegemea kuvuna; hapa ndipo serikali ya JK ilipoishia
Baada ya hapo unahitaji investment za kutoa hizo resources zilipokuwa na inahitajika hela ya kujenga rigs, refinery/LNG plant, pipes and so forth; now this provides a chance to discuss on share of benefit based on return of investment and sunk costs; haya makubaliano kama nchi atuja afiki bado na ndio mjadala unaofuata.
This stage complicated tofauti na simple arguments za local contents na upuuzi mwingine watu kama kina Zitto wanavyo ongelea. The finance are very very very complicated ukikosea utajuta ndio maana wao hawana haraka kwa sababu wanajua wana rights za kuchimba so they need a good deal in the long run.
Kutoa pressure kwa upande kwao ni swala la kuwapa hela watu kama hakina Zitto kukosoa hatua za serikali
With simple economic loss nchi one haraka ya kuingia hiyo mikataba kichwa kichwa.
JK ahusiki na hii hatua ila anaweza shawishika na upuuzi wa mtu kama Zitto na habari zake za local context. Na yeye JK kutumia hizo info kumpa pressure mama kutokana na hoja za kipuuzi and nonsense from twitter.
Contract ni ya muda gani kwa hao wawekezaji kurudisha gharama na kupata faida? hisa za serikali ni asilimia ngapi? ndo maana magu hakuwa na mzuka nako hadi kuangukia kwenye bwawa la stiglaz.......
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.