Watanzania tusipomshukuru Nyerere kwa hili tutapata laana

Watanzania tusipomshukuru Nyerere kwa hili tutapata laana

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salam, ningependa nielekee kwenye mada husika.

Ndugu watanzania na wana JF wenzangu, katika pita pita yangu ya kutafuta ugali wangu, nimefanikiwa kukutana na watu mbali mbali waliotoka katika nchi mbali mbali za Africa na nje ya Africa.

Hakika kukutana nao watu hao kumenifanya nifahamu mambo mbali mbali yanayohusu nchi zao na tamaduni zao.

Katika kufahamu huko ndipo nilipokuja kuona upendo wa kweli aliokuwa nao baba yetu wa Taifa mwl J.K. Nyerere kwa sisi watoto wake au wananchi wake.

Nchi hizi nyingi unakuta hazina utaifa. Kwa mfano kuna wacongo ambao lugha yao kuu ni lingala tu, wangala hawa wakikutana na wacongo wanaoongea kiswahili huwa hawapatani kabisa, kiasi kwamba unaweza ukafikiri kuwa watu hao ni wa nchi mbili tofauti.

Yani mcongo anae ongea kiswahili yupo radhi kumsaidia mtanzania, mkenya au muongea kiswahili yeyote mwenzake kuliko kumsaidia muongea lingala.

Hivyo hivyo na kwa ndugu zao wangala ambao huwaona wenzao waongea kiswahili kuwa sio wacongomani original, wangala huamini kwamba waongea kiswahili ni migrants waliongia congo miaka mingi iliyopita wakitokea katika nchi kama vile Tanzania, Burundi, Rwanda nk.

Tukija kwa upande wa Zimbabwe pia kuna ubaguzi katika ya makabila makubwa mawili yenye kuongea lugha tofauti, yani washona (shona) na wandebele (ndebele).

Pia hawa wamekuwa hawana umoja hata chembe. Unakuta mfano mshona labda anapewa deal la kutafuta wafanya kazi na boss wake, mshona atahangaika kutafuta washona wenzake na akiwakosa basi bora deal hilo ampe mtu yeyote kutoka katika nchi nyingine kuliko kumpa mzimbabwe mwenzake wa kabila la ndebele hata kama wanapanga katika mjengo mmoja.

Na hii ipo hata kwa wandebele ambao hupeana kazi wenyewe kwa wenyewe, huku wakiwaacha ndugu zao washona kwenye mataa. Washona anaamini kuwa wandebele ni migrants walio ingia Zimbabwe kutoka Afrika kusini miaka mingi iliyopita.

Kadhalika hata kwa jirani zetu kama vile Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda tumeweza kuona migawanyiko hiyo ambayo huendelea mpaka nje ya mipaka ya nchi zao. Ila kwa Tanzania hali imekuwa tofauti.

Pamoja na utofauti wa itikadi zetu za kisiasa, kidini, kabila nk. Lakini linapokuja swala la kitaifa tunakuwa kitu kimoja. Leo hii mtanzania akipata tatizo lolote huku nje tutamchangia kwa sababu ya utanzania wake, na sio kwa ajili ya dini yake, chama chake, kabila lake au mkoa wake.

Tunaamini sisi wote ni wamoja, tunaoishi katika nyumba moja, ya baba mmoja na mama mmoja.

Kwa wenzetu ukileta taarifa za mmoja wao kama anaumwa au kafariki, utasikia wanauliza.. kwanza huyo kijana aliekufa, kupata tatizo au kuumwa ni muhutu au mtusi, ni muongea lingala au kiswahili, ni mshona au ndebele, ni mkikuyu au mjaluo nk.

So kwa hili la baba wa taifa kutujenga na kutufanya watanzania wote tuwe kitu kimoja katika utaifa, ni la kupongezwa sana. Japo kwa sasa kuna baadhi ya changamoto ndogo ndogo zimekuwa zikijitokeza, lakini ule msingi wa utaifa bado upo.

Nani kama Nyerere? Asanteni sana kwa kunisoma. Picha ya chini kabisa baba wa taifa mwl J. Nyerere akikumbatiana kwa furaha na mh J. Kikwete. RIP baba wa Taifa letu
 

Attachments

  • images (85).jpeg
    images (85).jpeg
    14.7 KB · Views: 25
  • images (86).jpeg
    images (86).jpeg
    19.3 KB · Views: 26
Mwendazake na Mpemba wametusahaulisha ya Mwalimu na sasa wameturudisha huko kwenye kuulizana Makabila.

Nimeshangaa sana Juzi, Trafiki kuniuliza: Kwani wewe kabila gani? Aisee!! Nlimind na amenifikirisha mpaka saahizi!!?
 
Mwendazake na Mpemba wametusahaulisha ya Mwalimu na sasa wameturudisha huko kwenye kuulizana Makabila.

Nimeshangaa sana Juzi, Trafiki kuniuliza: Kwani wewe kabila gani? Aisee!! Nlimind na amenifikirisha mpaka saahizi!!?
Tusikubali kurudishwa katika enzi za ukabila, dini wala ukanda. Hayo yalikwepo kabla ya uhuru, lakini baada ya uhuru mwl Nyerere aliyaondoa haya. Ndo maana leo tunatambuana kiutanzania wetu na sio ki ukabila, udini wala rangi zetu.
 
Tusikubali kurudishwa katika enzi za ukabila, dini wala ukanda. Hayo yalikwepo kabla ya uhuru, lakini baada ya uhuru mwl Nyerere aliyaondoa haya. Ndo maana leo tunatambuana kiutanzania wetu na sio ki ukabila, udini wala rangi zetu.
Kuna mambo yanaendelea chinichini na yananyamaziwa.
Unaikumbuka inshu ya Diwani, Ashura & Taarifa ya Polisi?
 
huyu mzee tulipewa na Mungu, kwa kifupi mojawapo ya nchi zilizopendelewa duniani katika uumbaji Tanzania tumo ni vile tu viongozi wetu wengi wao ni wabinafsi waliopitiliza wanajijali wao na matumbo yao na matumbo ya familia zao.
Hakika mkuu. Nchi nyingi zilihitaji kiongozi aina ya Nyerere, lakini hawakumpata. Sisi tulipewa na Mungu lakini ndo hivyo, baadhi hawakuweza kuona faida yake.
 
Back
Top Bottom