Watanzania tusipomshukuru Nyerere kwa hili tutapata laana

Mkuu 'Dudumizi', najua wewe siyo mgeni sana humu JF, na ninakumbuka vyema michango yako humu Jukwaani.

Ila sielewi hasa ni nini msukumo uliokufanya uweke mada hii hapa, ambayo kwa kiasi kikubwa na kwa bahati mbaya sana ni kama imekwishapitwa na wakati.

Unayoyaeleza kwenye andiko lako gumu (kutokana na uwasilishaji wake wa kiuandishi), ni mambo ambayo yalikuwepo miaka michache iliyopita. Siku hizi tuna makundi mbalimbali, kila kundi likipigania maslahi yake zaidi kuliko utaifa alioufanyia kazi kubwa Mwalimu Nyerere.

Leo hii tunayo makundi kama ua UCCM na wenzao; kuna wanaoamini zaidi udini wao kuliko uTanzania wao.
Siku hizi ni sifa kujitambua kuwa wewe ni Msukuma, na unaona raha kabisa kuzungumza lugha yako hata kama kuna wasioelewa chochote juu ya lugha hiyo.

Sasa hivi tupo kwenye shughuli kubwa ya "Kuifungua nchi."
Kuifungua nchi nako kunaonekana kuwa kama ni kutafuta njia za kuwapata watu wenye uwezo wa kuunda kundi lao lenye uwezo wa kuwa tofauti na makundi mengine. Tutatumia nguvu nyingi kuliunda kundi hili kwa gharama kubwa dhidi ya makundi mengine.

Hii ni mifano michache tu inayoweza kukuonyesha kwamba kazi kubwa aliyoifanya Mwalimu Nyerere, tena kwa mafanikio makubwa, sasa hivi ni kama kuna juhudi kubwa ya kuibomoa kazi hiyo.
 
Kabla hajawa Rais Tanganyika haikuwa na tatizo la ukabila wala udini lakini aliposhika madaraka alitengeneza tatizo la udini, waislamu walianza kuminywa kisiri siri.
Walianza kuminywa kivipi mkuu? Hebu tufafanulie.
 
Mkuu Kalamu1 , kwanza napenda kutumia nafasi hii kukushukur kwa kufuatilia michango yangu na ya wana JF wenzetu mbali mbali. Kwa hakika haya ya ubaguzi unayoyasema mengi yanafanyika ndani ya mipaka yetu, na sio nje ya mipaka yetu. Sikatai kwamba hata nje bado kuna makundi mbali mbali ya uchama kama vile ccm wana mashina yao mengi nje ya nchi, ambayo yanaendesha shughuli za kichama kwa watanzania wanaoishi katika nchi hizo.

Halikadhalika na Chadema, Cuf na vyama vingine navyo vina mashina yao mbali mbali huku nje kwa ajili ya masilahi yao na ya vyama vyao kama ilivyo kwa ccm. Ila linapokuja swala la utaifa, mfano kuna mtanzania amepigwa risasi akafari na baadae kuhitajika michango kwa ajili ya kuusafirisha mwili wake, basi wengi huchangia kwa kigezo cha kumchangia mtanzania mwenzetu, na sio kuchanga kwa vile ni mnyatulu mwenzetu, mzaramo mwenzetu, muislamu mwenzetu, mkristo mwenzetu nk.

Kuna nchi zina ubaguzi wa ndani na nje. Yani raia wanabaguana wakiwa ndani ya nchi na nje ya nchi pia. Mfano unakuta mcongo amefariki inapokuja taarifa kwa wacongo wenzie utaona wanaanza kuuliza vipi aliekufa ni msema lingala au mswahili. Ukisema tu ni msema lingala, basi utasikia wasema kiswahili wanajibu kama ni msema lingala basi atazikwa na wangala wenzake sisi huo msiba hautuhusu.

Kwahiyo mkuu pamoja na kwamba kuna changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika nchi yetu, lakini bado ile misingi ya umoja na utaifa haijabomoka, sijui labda kwa huko mbeleni kama watanzania hatujakuwa macho kukemea ubaguzi wa aina yoyote.
 
Nafikiri hapo kwenye kabila wangetoa na badala yake wangekuwa wanauliza utaifa, au namba ya kitambulisho cha uraia.
 
Kwahiyo mkuu pamoja na kwamba kuna changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika nchi yetu, lakini bado ile misingi ya umoja na utaifa haijabomoka, sijui labda kwa huko mbeleni kama watanzania hatujakuwa macho kukemea ubaguzi wa aina yoyote
Hizi unazoziita "changamoto", ndiyo chachu (mbegu) mbaya kabisa inayotupeleka huko, tena kwa haraka sana, ambako tulidhani kuwa sisi hatupo tena.

Aliyoyafanya Mwalimu katika eneo hili yalitakiwa kuendelezwa (kupaliliwa) kwa makini zaidi na viongozi wote waliokuja baada yake, lakini sasa utaona kuwa kuna baadhi yao wanaong'oa hata mizizi ya mbegu hiyo muhimu.
Tulishafikia mahali ambapo kujua au kujitambulisha kwa mtu kwa kabila lake ilikwishakuwa haina maana yoyote.
 
Ya nimekuelewa mkuu. Nafikiri ni vizuri sisi wananchi kama raia halali wa nchi hii tupambane na wale wanaojaribu kuiharibu misingi hii bora kabisa iliyoachwa na baba yetu wa taifa.
 
Alikuwa akiwabagua katika madaraka na wengine kuwekwa ndani kwa visingizio mbalimbali.
Ok mkuu.. ila mbona hata wakristo wapo waliokosa kuwekwa katika uongozi. Wapo pia waliofungwa, na wengine kukimbia nchi kama vile kina Oscar Kambona nk.
 
Piga Vita udini na ukabila unagawa watu
 
Piga Vita udini na ukabila una gawa watu
 
Mwendazake na Mpemba wametusahaulisha ya Mwalimu na sasa wameturudisha huko kwenye kuulizana Makabila.

Nimeshangaa sana Juzi, Trafiki kuniuliza: Kwani wewe kabila gani? Aisee!! Nlimind na amenifikirisha mpaka saahizi!!?
Tena mwendazake ndio alikuwa akipiga kampeni kwa kilugha na kujivunia kabila lake kila mara,,
 
Nafikiri hapo kwenye kabila wangetoa na badala yake wangekuwa wanauliza utaifa, au namba ya kitambulisho cha uraia.
Hilo takwa la hoteli kujaza kabila ni takwa la Polisi/ Uhamiaji. Haja ya kubadili ujinga huu iko pale pale. Polisi walirithi kwa Mkoloni. Mie ambaye mama na baba huwa ni makabila tofauti huwa napiga kamari nijaze kabila lipi kila ninapohitajika. Wabunge wetu wao ni kushangilia bajeti basi; hili hawalioni. Sasa hivi wapenzi wa makabila tofauti kuoana imeenea mno kwetu Tanzania, pia sifa ya huyo huyo Baba wa Taifa; kwa hiyo ni kero kweli kweli watoto wao kuwauliza kabila!

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
..Tanganyika haikuwa na tatizo la ukabila kabla ya uhuru.

..Kwa hiyo Mwalimu Nyerere alienzi na kutunza hali ya undugu na maelewano iliyokuwepo.

..Lugha ya Kiswahili nayo ilikuwa imesambaa maeneo mengi ya Tanganyika.

..Kwasababu Kiswahili kilikuwa kikieleweka na Watanganyika waliowengi ilikuwa rahisi kwa Tanu kueneza ujumbe wa kudai uhuru nchi nzima.

..Mwalimu alifanya juhudi kubwa kueneza ELIMU kwa Watanzania wote bila ubaguzi.

..Mwalimu pia alichukua maamuzi ya kuandikisha Watanzania wote ktk majeshi yetu.

..Wakoloni walikuwa wakiandikisha makabila fulani majeshini, Mwalimu aliondoa utaratibu huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…