Watanzania tusipomshukuru Nyerere kwa hili tutapata laana

Hilo swala lilikuepo tangu zamani, yeye amelikuta. Ndio maana hata watemi, machifu walikuwa na ushirikiano. Hata yeye alikaribishwa mjini na wenyeji kwa upendo, kwa hiyo umoja huo upo kabla yake
 
Kabla hajawa Rais Tanganyika haikuwa na tatizo la ukabila wala udini lakini aliposhika madaraka alitengeneza tatizo la udini, waislamu walianza kuminywa kisiri siri.
Una shida ww.Umenikumbusha ya prof Kigoma Malima kutaka kujiunga Chuo Kikuu lazima uwe Abdallah ama Ashura.
 
Nyerere hiki kitu alikikuta alichofanya yeye ni kudumisha hali hiyo. Yumkini Nyerere alipata shida na changamoto kudumisha hali hiyo
Huku pwani tulikuwa tukikutana kwenye vijiwe vya kahawa haulizwi mtu kabila wala Asili yake

Ukiingia interior utakuta
The largest colonial resistance war in Africa => Majimaji War ilihusisha makumi kadhaa ya makabila hii inaonyesha jinsi gani Machifu wa Makabila yetu walivyokuwa wamoja

Wakati tunaanzisha taasisi za kupigania uhuru wa nchi AA => TAA=> TANU halikadhalika mambo yalikuwa hivyo hivyo.Nyerere + Rupia + Kahama waliweza tangamana na akina Sykes + Mshume Kiate + Mwapachu + Titi + Aziz Ali + Takadiri + Mtemvu + Mufti Hassan bin Amir + Tewa Said na kutengeneza taasisi iliyo na nguvu kubwa

Mambo yalibadilika baada ya kupata Uhuru, tukaanza kusikia baadhi ya Mashirika ya Uma yakanasibishwa na kabila fulani
eti kuanzia Mfyagiaji mpaka Meneja Mkuu ni wa kabila fulani
Tukaanza kushuhudia watu wa dini fulani wakirundikana kwenye taasisi muhimu zote zilizobeba hatima ya nchi kwa uwiano wa 75:25 mpaka 80:20
Tukaanza kushuhudia ktk elimu watoto wa dini fulani wakifaulu/kufeli ktk uwiano uliyoonyeshwa hapo juu

Wakatabahu
 
KWELI TUPU. INAYONISHANGAZA KWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI NI KUCHIPUKA KWA UBAGUZI WA KIVYAMA VYA SIASA? NI HATARI KUBWA! INATAKIWA KUREKEBISHWA HARAKA. NAPENDEKEZA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA. WANASIASA VIONGOZI WA VYAMA WASHINDANE KWA UWAZI NA HAKI. WASHINDANE KWA HOJA, PIA WAWE NA TUME YAO HURU YA KUSHUGHULIKIA MASLAHI YAO
 
Inabidi sisi wenyewe kama watanzania, tukiona swala linapelekwa nje ya mstari tupambane ili lirudishwe katika misingi yake.

CCM imeifikisha hii nchi mahali hakuna hoja za watanzania, bali kuna hoja za CCM, na hoja za wapinzani. Sioni ni wapi tunasimama kama watanzania kwenye hoja zetu. Labda mahali tulipo pamoja japo ni kwa maumivu, ni mfumuko wa bei.
 

Kama taifa lina umoja kwa nini Nyerere alipeleka jeshi Zanzibar na mpaka leo limebaki? Umoja wa kulazimishana na mtutu wa bunduki na vifaru.
 
Baba wa Taifa angekuwepo kipindi hiki Angenyonga watu wengi sana! Kuna Taasisi kubwa na makampuni bado zinaendekeza hayo mambo kwa Usiri mkubwa sana.....Huwezi kulijua hilo km Hujabaguliwa.
 
Haya mambo ya kuulizana makabila kwa kweli hayana msingi wowote. Ni bora kwenye mahoteli wawe wanauliza ID namba au kwa mgeni aulizwe passport namba.
 
Baba wa Taifa angekuwepo kipindi hiki Angenyonga watu wengi sana! Kuna Taasisi kubwa na makampuni bado zinaendekeza hayo mambo kwa Usiri mkubwa sana.....Huwezi kulijua hilo km Hujabaguliwa.
Baba wa taifa aliacha misingi bora sana. Inabidi tuilinde na kuisimamia ipasavyo ili misingi hiyo isije kubomoka.
 
Hilo swala lilikuepo tangu zamani, yeye amelikuta. Ndio maana hata watemi, machifu walikuwa na ushirikiano. Hata yeye alikaribishwa mjini na wenyeji kwa upendo, kwa hiyo umoja huo upo kabla yake
Mkuu BrownRange inawezekana kweli hilo swala lilikuwepo kabla yake. Lakini na yeye aliposhika madaraka alilisimamia kwa nguvu zake zote, na alikemea wale waliotaka kujaribu kutengeneza ubaguzi kupitia makabila nk.
 
Nashukuru sana mkuu Adilinanduguze , kama ni hivyo basi kuna ulazima wa kurudia katika umoja wetu ule ule uliokuwepo kabla ya uhuru.
 

Yaani tumshukuru Laanatullahi Nyerere aliyesababisha kuuwawa watu kwa maelfu Zanzibar baada ya kuivamia kwa msaada wa Wakoloni Waingereza waliomweka madarakani baada kupinduliwa ? Mnyama huyu ndiye aliyeipoteza dola yetu ya Zanzibar kwa kukubali kuwatumikia Mabwana zake waliomweka madarakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…