Watanzania tusiwe wanafiki, Tozo ni muhimu kwa upana wake

Kwahiyo Wabunge hawatumi Miamala !? Au wameo wapo Excluded. Yaani Wamepeleka namba Zao zitolewe Kwenye Makato
 
Hamkulalamika hivyo wakati wa Magufuli, kuwa fedha wanazonyang'anya wafanya biashara zinaenda wapi?
Arusha Beureu De Change zimeporwa na vyombo vya serikali, hela ilienda wapi?
Ndio maana nasema tusiwe wanafiki.
Hii tabia ya kila kitu kurejea kwa mwendazake ni ya kipuuzi kwa sababu haiwezi kumrejesha mtu aliyetangulia mbele za haki. Pili hata mti wa mnazi una akili nyingi kukuzidi wewe kwa sababu unatambua ya kwamba ikija tufani na upepo mkali unainama kuupisha na upepo ukipita mnazi unarudi wima kuendelea na maisha.
 
Kwahiyo Wabunge hawatumi Miamala !? Au wameo wapo Excluded. Yaani Wamepeleka namba Zao zitolewe Kwenye Makato
Nimejumuisha KODI na TOZO kwenye maelezo yangu. Wabunge na Rais wana kesi ya kutolipa Kodi stahiki.

Natambua fika Tozo zinahusu makundi yote! Lakini bado, maumivu mengi yako kwa raia wa kawaida, wanaifanya miamala kila siku ukilinganisha na hao Wabunge.
 
Watanzania wengi tunapenda vinavyoelea ,hatutaki kinda.
 
Ndio maana tunasisitizwa Tuchague Viongozi Sahihi. Naona Jambo Hili Tutajifunza Baadae kwenye Uchaguzi
 
Tozo ni muhimu je hicho kiwango kitaleta tija? mimi nadhani kiwango bado siyo rafiki ,sera ili ili ifanikiwe ni lazima iwe shirikishi 'ineffective public policies always fail'
 
Mabwenyenye wa nchi hii wanaishi maisha ya kufuru alafu wanataka watu maskini wakatwe tozo, mwalimu, daktari anaishi kwa kutegemea mshahara wale ila wakuu wa wilaya/mikoa, wabunge, MARAS, MADAS na nk... Wanahudumiwa kila kitu na serikali nje ya mshahara wao, kwa no wasiishi kwa kutumia ujira wao? Wana uspecial gani wao? Uzalendo wa kweli ulipaswa kuanzia kwa hawa na hiki ndo kinawavunja moyo watanzania
 
Huu ndio ujinga mliopandikizwa na wajinga wenzenu.
Sasa hao unaona ndio matajiri wako wangspi nchini dhidi ya nyie mliokubali kuitwa kijinga ati "wanyinge"?
Ukitawaliwa kiakili utabaki nyuma dsima.
Lipa tozo bana!
 
Ujinga huo kamuhadithie babu yako kijijini.
 
Ndio maana nasema mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Hiyo transoarency ilikuweoo Awamu ya tano?
Mtu kachota tril 1.5 na kamfukuza CAG aliyehoji, mlikuwa wapi
?
 
Ndio maana nasema mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Hiyo transoarency ilikuweoo Awamu ya tano?
Mtu kachota tril 1.5 na kamfukuza CAG aliyehoji, mlikuwa wapi
?
Awamu ya tano hakukuwa na Tozo mind you na kwa mambo ambayo yamefanyika kama una akili timamu huwezi kuanza kuhoji ikiwa unaona miundombinu inajengwa kwa kasi yani mambo yanafanyika na kuna dira ya kiongozi aliyepo madarakani inayofanya kazi. Yapo mabaya yake pia ila hakukuwa na huu ushenzi wa kupora wananchi fedha zao kwa mgongo wa uzalendo!

Nikikuuliza msimamo wa kiongozi wa sasa ni upi unaweza elezea japo kwa machache?
 
Tozo ni muhimu je hicho kiwango kitaleta tija? mimi nadhani kiwango bado siyo rafiki ,sera ili ili ifanikiwe ni lazima iwe shirikishi 'ineffective public policies always fail'
Tusijidanganye.
Iitwe TOZO au KODI yote ni mamoja.
Hiyo hela inaingia serikalini kufanya yale yaliyotazamiwa.
Miradi ya SGR na Stiglaz Umeme yote inahitaji hiyo tozo na kodi.
Kwamba ni kwa kiwango kipi itabaki kuwa issue, swala hapan i kwamba yale yalioanzwa kujengwa kimaendeleo ni lazima yakamilike iwe kwa kodi au tozo.
 
Wewe kwa sababu ulikuwa hukamuliwi ndio maana unalia sasa.
Nyie ndo haswa lengo la hii mada.
Wanafiki mliokuwa hamguswi na Magufuli, kila kikicha mnamshangilia kama hmna akili nzuri.
Sasa mmeguswa.
Lipeni tozo bana.
 
Tatzo tozo nyingi na kama una lain tatu ukifanya muamala wanakukata pote na kila ukifanya muamala unakatwa kwanini wasiweke hata 500 kila tozo bado kampuni za simu wakukate,ila acha akili itukae maana sisi maskin ndio hupenda ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…