Kuna Mtanzania alikuambia hataki kulipa kodi! Au kukatwa hizo tozo? Watu wanalalamikia matumizi yake, yaliyojaa ubadhirifu mkubwa na ufisadi wa kutisha!
Lakini pia watu wanalalamikia namna wahamasishaji wenyewe wa hizo kodi/tozo kuwa mstari wa nyuma kwa kukwepa kulipa, huku wanyonge na watu wa kawaida wakiwajibishwa ipasavyo!
Mfano mzuri ni Kesi ya Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kulalamikia mishahara ya Wabunge kutokukatwa kodi, Mshahara wa Rais nao tunasikia haukatwi kodi, nk. Hiki kitu ndicho kinacho amsha hisia hasi kwa raia.
Ili kodi na tozo zilipwe kwa urahisi, viongozi wawe mfano wa kuigwa kwa kulipa hizo kodi, lakini pia kuzitumia kwa matumizi sahihi! Na siyo kuzitapanya, kama ilivyo sasa.