Watanzania tutamlinda, kumpigania na kumtetea Rais Samia kwa gharama yoyote ile

Nani kamuua MZEE KIBAO na kwann ???
 
Hakuna anayependa utekaji
Hakuna kiongozi mwenye kuzuia ukemeaji wa wa utekaji

Ila Kuna tofauti kati ya kuhoji utekaji na kutumia tukio la utekaji kuchonganisha wananchi na serikali

Usijitoe ufahamu
Kilichosemwa ndo ukweli
 
Sema maccm; sio Watanzania-aibu mtaipata bure
 
Kwani kuna Rais anayelipwa mshahara Mkubwa kumpita Rais wa Marekani? Vipi kuhusu ulinzi wake? Acha umbumbumbu wako hapa ndugu yangu mtanzania uliyejaa msongo wa mawazo
Acha upuuuzi na uvivu wa kufikiri, ulinzi anaopewa ni Kodi zetu, mshahara anaolipwa ni Kodi zetu, ulinzi gani anaouhitaji zaidi kutoka kwetu, zaidi ya yeye kutimiza wajibu wake??
Akivuruga akapishana na mtazamo wa wananchi, tutoke tukaandamane na mabango yaliyoandikwa KAUPIGA MWINGI???
akivuruga uhusianao na nchi zingine kwa kutokupembua kauli na misimamo yake sie tutengeneze video za kumtetea MITANO TENA?

NB; Mbali na kuwa yeye ni Rais ni mwanasiasa pia, anahitaji kutengeneza ushawishi na kwenda na upepo wa watu wake.

CCM ndo wanakazi ya kumtetea coz lengo lao ni kubaki kwenye Dola, msitusumbue walala hoi.
 

Ibada ya kweli ya kumtukuza Mungu ni ile ambayo inakemea Uovu na kutukuza HAKI na AMANI kwa Watu wote.

Vitendo vya uhalifu mbaya wa kuteka watu, kuwatesa, kuwabaka, kuwalawiti, kuwajeruhi kwa namna mbalimbali ikiwemo na kuwamwagia tindikali, kuwashambulia kimwili na kihisia, kuwekea sumu, na kuua ni vitendo vya UOVU MBAYA WA SHETANI. Yeyote yule anayetenda vitendo hivi au kuunga mkono vitendo hivi viovu, huyo ndiye SHETANI mwenyewe.
Kutenda au kuunga mkono vitendo hivi Viovu ni kufanya Ibada ya Kumtukuza Shetani, na kupinga Vitendo hivi Viovu ni kufanya Ibada ya Kumtukuza Mungu.

Kati ya hawa Watu wawili ambao wanakumbana hapa Tanzania kwa sasa ambao umewagusia kwenye hili bandiko lako, Je, Nani atakuwa ni SHETANI na nani atakuwa ni Malaika wa Mungu kwa jinsi unavyowaona wewe Kutokana na matendo yao hao Watu??
 
Mimi niondoe siyo mmoja wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…