Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Hatuna jinsi ni yeye tena 2025 mpaka 2030.
Namuomba sana mama awe anasimamia uwajibikaji ikiwezekana awe anatumbua kimyakimya. Na afanye ufuatiliaji wa karibu kupunguza gharama za vitu mbalimbali kupanda. Vifaa vya ujenzi vinapanda mara 3 ndani ya mwezi mmoja, vyakula,mafuta ya kula, umeme .

Ashughulikie kiuhakika suala la kupanga wamachinga ikiwezekana serikali inyanganye baadhi ya maeneo ili wamachinga wapate nafasi.

Hakuna suala linaachiwa vibaya kukua na kuendelea kama watu kujenga mpaka barabarani maeneo kama barabara ya mwenge to bagamoyo, barabara kama za mwananyamala sasa hivi wanajenga mifereji kwenye milango ya watu sijui kwanini lukuvi havunji nyuma zilizojengwa tofauti na mawe ya viwanja. Kawe nako kunakuwa kituko wabomoe nyumba zote zilizozidi barabarani
 
Hajamaliza mwaka kelele nyiingi. Kuna waliokereka hawakutaka awe rais uyu mama kutokana na imani yake na uzanzibari. Lakini wapo wakristo wanamkubali na wanampenda sana. Wabarikiwe
Kila akikosolewa eti kwa sababu ya dini. Upuuzi mtupu. Hizo dini zenu za kuletwa na wageni zina faida gani!?
 
Hajamaliza mwaka kelele nyiingi. Kuna waliokereka hawakutaka awe rais uyu mama kutokana na imani yake na uzanzibari. Lakini wapo wakristo wanamkubali na wanampenda sana. Wabarikiwe
Mwambie mama yako huyo aache kelele. Hata mwaka hana kashaanza kelele za kugombea 2025.
 
Nawaza tu kwa kasumba waliyo nayo wananchi wa jinsia zote kuhusu kuongozwa na mwanamke na zaidi anatoka Zanzibar inahitajika nguvu ya ziada.wanawake wenyewe wengi hawaamini mwanamke miongoni mwao anaweza kuwa rais ukiondoa haiba za kiasili za kuchukiana wao kwa wao bila sababu.
 
Mwambie mama yako huyo aache kelele. Hata mwaka hana kashaanza kelele za kugombea 2025.

Uislamu ndio tatizo kwenu. Lakini tambua kuwa nchi ikiongozwa na musilamu inakuwa kiuchumi, wananchi wananeemeka na kufurahia. Refer wakati wa Mwinyi na kikwete ata wakristo wenyewe wanalitambua ilo,, na uyu mama ataiweka sawa 2mpe muda.
 
Kila akikosolewa eti kwa sababu ya dini. Upuuzi mtupu. Hizo dini zenu za kuletwa na wageni zina faida gani!?

Labda zilizoletwa na wazungu ndiyo hazina faida kwenu japo naheshimu sana imani za wengine.

Kuhusu uisilamu ni heri ukae kimyaa, maana hujui unachokiongea. Tunawashukuru sana waarabu kusambaza dini ya Mwenyezi Mungu (uisilamu) bara la afrika n.k. Mungu awabariki sana.
 
Hakuna mpumbavu wa kupoteza muda kuchagua mwanamke sorry sana
 
Hakuna mpumbavu wa kupoteza muda kuchagua mwanamke sorry sana
Heshima kitu cha bure!, usitukane watu wapumbavu kisa kuchagua mwanamke ukajikuta unapata laana ya bure ya kutukana wazazi wako, kwa kutukana huku, unamaanisha kumchagua mwanamke ni upumbavu na anayechagua mwanamke ni mpumbuvu!, can you imagine mpumbavu wa kwanza kwenye maisha yako alimchagua nani ndio wewe ukazaliwa!. Vitu vingine tuacheni ujinga!.
P
 
Mkuu Albaab , ni YEYE ndiye huziweka serikali za mataifa, ni YEYE pekee ndiye ajuaye nani ataamka kesho na nani atafika 2025!, hili ni nje ya uwezo wetu!.
Utaalamu wangu wa news analysis nimeupatia chumba cha habari, mimi ni mwandishi wa habari/mtangazaji, nimekaa newsroom miaka 30 kabla kustaafu rasmi mwaka jana.
P
 
Sawa mkuu, habari ya YEYE ni according to you ila sio general fact.
Mambo ya kusema YEYE ni dalili za kushindwa jambo maana YEYE ndio mwisho wa yote, sasa swala la uraisi sio mwisho wa yote mkuu, not for me!
 
Nchi ilipofikia hatuhitaji kipaumbele cha mteule wa rais kuwa jinsia fulani, bali tunahitaji mtu ambaye atauvaa uongozi na kuwa jasiri wa kutuvusha watanzania katika maendeleo, unachojaribu kusema hapa ati ni zamu ya kina mama kana kwamba hawa jinsia nyingine hawana haki, lakini unatumia lugha ya kificho kumpigia debe chini chini Mama Samia ili yeye ndio awe mteule wa urasi kwa mwaka 2025.
 

Anakosea sana uyu kijana,,,kama yeye hampendi cc 2nampenda,,,kama vipi achukuwe kamba akajinyonge
 
Wewe hata dini uzijui laana itatoka wapi ? Inatoka kwa mungu au mwanadamu ???? maana hata mungu mwenyewe ajataka mwanaume kuongozwa na mwanamke ndiyo maana mwanaume ni kichwa kwa mujibu wa dini ,au wewe una laana yako unaimiliki binafsi ambayo ni mali yako unawalaani watu utakavyo wewe ,maana kwa mujibu wa dini zote mbili mimi nipo sahihi wala sijatukana,
 
Wananchi wana shida lukuki mwaka huu-tozo, bei juu, wamachinga, bodaboda, maji, njaa!! Na sisi tunaongelea uchaguzi baada ya uchafuzi wa 2020 ambao umetuletea wabunge wanaotetea serikali badala ya wananchi??
Wapi katiba mpya na tume huru ambayo itawapatia wabunge bora??
 
Kwa hiyo Uislamu ndio umesema mwanamke aongoze wanaume!?
 
Yaani Kama Kuna MTU anajua kujikomba,Basi na Wewe Ni first class aisee ! Umejikomba wee Enzi za JPM,Lakini wapi! Haikuzaa matunda.Jitahidi kipindi hiki Cha Bi.Mkubwa ujikombe Kisawasawa.Labda atakuona.Ila kumbuka Mama alishasema anaangalia utendaji na Sio kujikomba kwenu.MARA NYINGI WANAOJIKOMBA HUWA SIO WATENDAJI WAZURI.Maana hawajiamini.
 
Umejikomba wee Enzi za JPM,Lakini wapi! Haikuzaa matunda.Jitahidi kipindi hiki Cha Bi.Mkubwa ujikombe Kisawasawa.Labda atakuona.Ila kumbuka Mama alishasema anaangalia utendaji na Sio kujikomba.
Nijikombe ili nipate nini?. Hili bandiko wewe ndio umeliona ni la kujikomba?. Kwa vile Mama Samia sasa ni rais wetu, hivyo yeyote atakayemsifu au kumpongeza ndio atahesabika anajikomba, ili ateuliwe DC!. Jee wale waliompongeza Mama Samia kabla hajawa rais, pia walikuwa wakijikomba?.





P
 

Mzee wa njaa kaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…