Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Wanabodi,

Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari.

Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, sasa katika hizo tatu, media ya Tanzania inafanya vizuri katika eneo la uhabarishaji, na kutoa burudani, lakini katika uelimishaji, bado tuna matatizo, na katika eneo la uchambuzi wa habari, news analysis ndio kabisa, media zetu nyingi hazina uwezo huo, kwasababu hazina watu wenye uwezo huo, matokeo yake, mtu akisema kitu, media zinachukua na kukirusha tuu hivyo hivyo kama kasuku, bila kukichakata na kukifanyia analysis.

Juzi kati hapa rais wetu Mhe. Mama kazungumzia need ya Watanzania kumchagua rais mwanamke mwaka 2025 kwa kusema tutamsimamisha Mwanamke, media zimelidaka kama lilivyo kikasuku kasuku na kuanza kulivurumisha, hivyo kuleta mjadala mkubwa kwenye media na mitandao ya jamii, mara kaanza kampeni mapema, mara kajiteua, mara ni ubaguzi wa kuwabagua wanaume, mara hivi mara vile, hivyo bandiko hili ni kuwasaidia kidogo, kuwafanyia a simple analysis ya alichokisema rais Samia.

Kwanza ni ombi kwenu Watanzania wenzangu, kwanza tuunge mkono msimamo wa rais wetu Samia kuwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2025, tuufanye, sio tuu ni zamu ya kuchagua mgombea mwanamke, bali tuifanye ndio zamu ya ukombozi rasmi wa mwanamke katika siasa, sio tuu tuchague rais mwanamke, bali tuchague wabunge na wadiwani wanawake kwa wingi na kuifikia ile 50/50 ya azimio la Beijing na hata kupita, ila kwenye urais, sio lazima ndio awe Mama Samia, anaweza kuwa yeye au mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa kwasababu mpangaji sio yeye, wala sio sisi, mpangaji ni YEYE. Hivyo ikitokea, YEYE amepanga rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 awe ni mwanamke, then rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 atakuwa ni mwanamke, ila mwanamke huyo atakuwa ni yule aliyepangiwa na YEYE, kuwa rais wetu 2025, kama aliyepangiwa na YEYE ni yeye Mama Samia, then who are we kusema no?, kama ni yeye aliyepangiwa, na YEYE, then ni yeye!, ila kwa vile mpaka sasa YEYE bado hajasema kampangia nani, naomba Watanzania tuwe tayari kujiandaa kisaikolojia kuikubali mipango ya YEYE kwa mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa na YEYE kuwa rais wetu 2025 and not necesarly ni Mama Samia.

Hivyo mimi naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwasabubu kiukweli kabisa, wanawake wana uwezo sana wa uongozi na wengine kuliko hata wanaume, ila siku zote, tumekuwa tukiwakandamiza kutokana na kutawaliwa na mfumo dume kwa miaka nenda miaka rudi, na mpaka Mungu alipoingilia kati. Kama Mungu asingeingilia kati na JPM akaendelea hadi 2025, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke, lakini baada ya Mungu kuingilia kati na Tanzania kwa mara ya kwanza tukapata rais mwanamke, na Mama Samia ameisha onyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza, then why not 2025 asiwe mwanamke sasa sio tena kwa kudra za Mwenyeenzi Mungu bali kwa chaguo la Mungu kwa Tanzania na kupata endorsement ya Watanzania kwenye sanduku la kura, kumchagua rais mwanamke na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Na hili likifanyika na likakamilika kikamilifu, uchaguzi wa 2025 tukapata 50/50 ya wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufuta viti maalum, vitakuwa havihitajiki tena, vikiendelea kubaki ni wastage of time, money and resources.

Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, ila Mungu huweza kulikatiza chaguo lake wakati wowote na kumchagua mwingine, hii haikuanza leo, toka enzi za Nabii Musa, alikatizwa hakuingia nchi ya ahadi Canan, kwa sababu fulani. Everything happens for a reasons anazojua Mungu mwenyewe, hivyo hata Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania labda hadi 2025 ni Mungu tuu mwenyewe anajua. Kama Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema nasi hapa katikati kabla ya 2025, kwasababu hata JPM, hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, vivyo hivyo kwa Samia 2025, ni Mungu tuu pekee ndiye ajuaye amepanga nini na amempangia nani, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa sasa wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua utaratibu wa CCM, anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if ndivyo na YEYE alivyopanga!.

Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is sure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha mwanamke huyo ni lazima awe ni yeye!, anaweza kuwa ni mwanamke mwingine yoyote!. Hivyo ni busara kwa rais wetu Samia, kwa sasa, hili la ugombea wa 2025, asilizungumze zungumze sana kwa sasa, ni vyema akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kumpa Kaizari yaliyo ya Kaizari kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na kwa yale ya Kimungu, tumpe Mungu kwa kumuachia Mungu mwenyewe!.

Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

Nenda ukanisome in between the lines, nilisema nini kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, katika mabandiko haya. Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? na hapa Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Ukiisha soma, kama una uwezo to read in between the lines, jibu utakuwa umelipata.

Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

2025 Twende na Mwanamke!.

Paskali
Update
Kuna hii sauti imeibuka Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Hasira za ugonjwa wa big ego Syndrome
 
Nagombea jimbo la kawe kupitia CCM.
Me ni zao la uvCCM nimetokea uvccm hadi now I'm matured ndani ya chama.
Need u'r support (material & moral support).
Kwa jimbo la Kawe, usipoteze muda wako na fedha zako, unless wewe ni inside man you have za inside kuwa aliyepo anatoswa!, na akitokea akatoswa the next is dogo Furaha Dominic. Mwakani Gwaji Boy atafanya makubwa Kawe hadi kumchinjia baharini itashindikana, jipime msuli kama unaweza kumkabili Furaha, then kwako Kawe njia nyeupe!. Will support you!
P
 
Kwa maoni yangu, uchaguzi hutegemea wagombea waliojitokeza kugombea nafasi fulani na kati ya hao wagombea, mwenye sifa zaidi kuliko wengine ndiye anayepaswa kuchaguliwa.
That is how it should be, ila CCM tuna utaratibu wetu wa mserereko midway, hivyo mgombea wa 2025 ni mserereko, inachapishwa fomu moja tuu, hakuna ushindani, hakuna upinzani.
Lakini kwa sasa kusema tumchague mwanamke as if tuna list ya wagombea tayari naona ni kwenda nje kabisa!
Hapana!, lengo la kusema tumchague mwanamke ni kwasababu aliyepo ameingia kwa kudra tuu ya Mwenyezi Mungu, CCM haina
Utaratibu na mgombea urais mwanamke, hivyo kwasababu tumepata mgombea mwanamke
By default only, then 2025 twende na mwanamke ili sasa awe ni amechaguliwa.
Hatumchagui tu mtu kwa vile ni mwanaume au mwanamke, bali yule mwenye sifa zaidi kati ya wagombea wenzake.
Yes ni kweli sexual orientation ya gender ya mtu sio miongoni mwa vigezo, bali zinaangaliwa sifa tuu, ila ukweli unabaki kuwa gender imetumika miaka mingi kuwabagua wanawake na kuwakandamiza, hata humu tuna ma male chouvenists wanaoamini mwanamke hawezi.

Ukishindanisha watu mwenye sifa zaidi akawa mwanamke, hapewi, atapewa mwanaume anaye fuata, na hivyo ndivyo nilivyoelekezwa kuhusu 2025 kwenye HII sauti!。

P
 
That is how it should be, ila CCM tuna utaratibu wetu wa mserereko midway, hivyo mgombea wa 2025 ni mserereko, inachapishwa fomu moja tuu, hakuna ushindani, hakuna upinzani.

Hapana!, lengo la kusema tumchague mwanamke ni kwasababu aliyepo ameingia kwa kudra tuu ya Mwenyezi Mungu, CCM haina
Utaratibu na mgombea urais mwanamke, hivyo kwasababu tumepata mgombea mwanamke
By default only, then 2025 twende na mwanamke ili sasa awe ni amechaguliwa.

Yes ni kweli sexual orientation ya gender ya mtu sio miongoni mwa vigezo, bali zinaangaliwa sifa tuu, ila ukweli unabaki kuwa gender imetumika miaka mingi kuwabagua wanawake na kuwakandamiza, hata humu tuna ma male chouvenists wanaoamini mwanamke hawezi.

Ukishindanisha watu mwenye sifa zaidi akawa mwanamke, hapewi, atapewa mwanaume anaye fuata, na hivyo ndivyo nilivyoelekezwa kuhusu 2025 kwenye HII sauti!。

P
Hili fundisho gumu kulielewa, maana linatetewa na mtu mmoja tuu.🤣🤣🤣
 
hapana"BIG NO!", mpango amekemea sana hii tabia naona watu hamjamuelewa vizuri. Hii tabia ya wanaume kutaka kutawaliwa na wanawake ni hatari sana kwa ukuaji wa taifa...jamani eleweni basi...hata Quran na Biblia haitaki hayo mambo 😎
 
Kwa jimbo la Kawe, usipoteze muda wako na fedha zako, unless wewe ni inside man you have za inside kuwa aliyepo anatoswa!, na akitokea akatoswa the next is dogo Furaha Dominic. Mwakani Gwaji Boy atafanya makubwa Kawe hadi kumchinjia baharini itashindikana, jipime msuli kama unaweza kumkabili Furaha, then kwako Kawe njia nyeupe!. Will support you!
P
Unakuwa fooled na mashindano ya rede???
Gwaji ameshindwa ku-deliver. Anzia na barabara DMDP kawe tumepata km chache sana.
Na hapo kawe haijawahi guswa kwenye DMDP.
 
Gwaji, aliahidi, atanunua tinga tinga 10, za kuchonga mabarabara kila kata, tinga tinga moja na lori mbili. Utekelezaji ndio 2025, hahitaji DMDP, yeye mwenyewe ata i DMDP Kawe!.
P
 
Hii tabia ya wanaume kutaka kutawaliwa na wanawake ni hatari sana kwa ukuaji wa taifa...jamani eleweni basi...hata Quran na Biblia haitaki hayo mambo 😎
Kuna tofauti kati ya kutawaliwa na mwanamke na kuongozwa na mwanamke, Mtume Muhammad (SAW), mwenyewe, kuna mambo kibao aliongozwa na mwanamke Bi. Hadija. Tanzania haitawaliwi na mwanamke, inatawaliwa na CCM, inayoongozwa na mwanamke. Kuna mambo kibao, mwanamke ni mzuri kuliko mwanaume.
P
 
hapana"BIG NO!", mpango amekemea sana hii tabia naona watu hamjamuelewa vizuri. Hii tabia ya wanaume kutaka kutawaliwa na wanawake ni hatari sana kwa ukuaji wa taifa...jamani eleweni basi...hata Quran na Biblia haitaki hayo mambo 😎
Hivi kwa nini mwanamke akitunga mimba (akakaa nayo miezi 9), akakuzaa, akakutunza na kukulea hata ukakakua na kupata mafanikio uliyonayo, bado unamwona mtu dhaifu, asiyefaa mbele ya mwanaume, nk? Kama kuna makosa yanatendeka na wanawake, hakuna yanayotendeka na wanaume? Kuna mama mmoja alinisimulia kwamba alivyokuwa msichana siku moja alitumwa sokoni jioni, wakati wa kurudi nyumbani wakati giza limeshaingia alipofika karibu na kichaka fulani alishtukia mtu anamshika kwa nyuma na kumziba mdomo, huku akimvutia kichakani alikokwenda kumbaka. Alipofika nyumbani akamwambia mama yake kilichomtokea. Kwa vile kubakwa kunaambatana na stigma, mama yake alimwambia atoke pale kijijini, akaishi kwa ndugu yake mbali na kijijini kwao na kisha huyo msichana aliamua aende kukaa mjini ili kubakwa kwake kusije kukafahamika kwa watu. Akiwa huko mjini, kumbe mimba ilishika na alishtukia imeshakuwa, na akaamua asiitoe. Kwa hiyo, first born wake (ambaye yupo hadi sasa, na ambaye pia alishakuwa mtu mzima na kuolewa na kuzaa watoto) ndiye anayemsaidia akiyumba kiuchumi, maana aliolewa na mume mwenye uwezo. Nilishabahatika kukutana naye huyo binti, ni mtu wa miaka kama 35 hivi, na anaonekana usoni mwenye furaha. Nilimuuliza mama yake kama alimwambia binti yake kama ni product ya kubakwa, akasema ndiyo, maana ilibidi amwambie ukweli. Kila nikimwona huyo binti yake, nakumbuka hicho kisa. Sasa hii roho yetu ya kukosa shukurani inatoka wapi?
 
Gwaji, aliahidi, atanunua tinga tinga 10, za kuchonga mabarabara kila kata, tinga tinga moja na lori mbili. Utekelezaji ndio 2025, hahitaji DMDP, yeye mwenyewe ata i DMDP Kawe!.
P
Sasa Advocate ushaanza kuwa mchekeshaji.
Hivi kwa elimu yako+umri wako hadi leo unamuamini Gwajima????
Jamaa ni muongo kuwashinda hata bongo movie.
 
Pale mwanzo hata mimi sikumuamini, na niliwahi kuuliza humu, Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais na nikawashangaa Watanzania wanamwamini Gwajima kuliko hata rais wao! Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko Rais wao?
Lakini baada ya Kuaminiwa na JPM..., who 'm I nisimuamini?. Tinga Tinga kumi , moja kila kata zitakuja, malari mawili ya mchanga kila kita yatakuja, zile boti 100 za kuvulia samaki zitaletwa, wale wavuvi 100 watapelekwa Marekani.

Hata hii treni ya umeme,
View: https://youtu.be/JTs_mLe9KLw?si=CO3C5sz2dt3t2dUw itakuja, bado tunasubiria uzinduzi siku chache zijazo.

Hata hii private jet Gulf Stream
View: https://youtu.be/xyTATLaaNOU?si=lOXPKf0suMQ1Uaaf
Itakuja.

Vuta tuu subra!.

Mimi nimeshavuta tuu subira nikachoka na nilichoka zaidi niliona siku moja "anafufua mfu" kanisani kwake! Nikaona hii imani tunaipeleka mbali au yenyewe ndiyo inayotupeleka mbali tuu. 🤣🤣🤣
 
sasa ndugu yangu sijauliza maana ya kutawaliwa au kuongozwa!, haya yote ni "nonsense"...mambo ya ccm kuongoza au mwanamke yote ya nini...??

Mwanamke kuwa TOP katika namna yoyote ile iwe kifamilia, kitaasisi au kiinchi..ni hatari sana kwa ustawi ...kiimani ama kikawaida yaani si kikristo ama kiislam. Huku tulikofikia sisi kama nchi..ni kwamba miaka minne hii "tumebeti" tumeshikilia roho mkononi kama taifa hatuna furaha kwasababu juu kabisa kuna mwanamke anaongoza/anatawala. Tumezoea na tutaendelea kuzoea nafasi za juu kabisa za kimaamuzi anakaa MWANAMUME hizo zingine za chini yake hamna shida akikaa mwanamke au mlemavu au yeyote asiyejiweza hakuna shida sana. Kwahiyo tuendelee kuelewa tu kwamba sisi wanaume wa taifa hili kwasasa tunaendelea kutawaliwa/kuongozwa na MSHANGAZI TU wala hakuna lingine 😎
 
Hivi kwa nini mwanamke akitunga mimba (akakaa nayo miezi 9), akakuzaa, akakutunza na kukulea hata ukakakua na kupata mafanikio uliyonayo, bado unamwona mtu dhaifu, asiyefaa mbele ya mwanaume, nk? Kama kuna makosa yanatendeka na wanawake, hakuna yanayotendeka na wanaume? Kuna mama mmoja alinisimulia kwamba alivyokuwa msichana siku moja alitumwa sokoni jioni, wakati wa kurudi nyumbani wakati giza limeshaingia alipofika karibu na kichaka fulani alishtukia mtu anamshika kwa nyuma na kumziba mdomo, huku akimvutia kichakani alikokwenda kumbaka. Alipofika nyumbani akamwambia mama yake kilichomtokea. Kwa vile kubakwa kunaambatana na stigma, mama yake alimwambia atoke pale kijijini, akaishi kwa ndugu yake mbali na kijijini kwao na kisha huyo msichana aliamua aende kukaa mjini ili kubakwa kwake kusije kukafahamika kwa watu. Akiwa huko mjini, kumbe mimba ilishika na alishtukia imeshakuwa, na akaamua asiitoe. Kwa hiyo, first born wake (ambaye yupo hadi sasa, na ambaye pia alishakuwa mtu mzima na kuolewa na kuzaa watoto) ndiye anayemsaidia akiyumba kiuchumi, maana aliolewa na mume mwenye uwezo. Nilishabahatika kukutana naye huyo binti, ni mtu wa miaka kama 35 hivi, na anaonekana usoni mwenye furaha. Nilimuuliza mama yake kama alimwambia binti yake kama ni product ya kubakwa, akasema ndiyo, maana ilibidi amwambie ukweli. Kila nikimwona huyo binti yake, nakumbuka hicho kisa. Sasa hii roho yetu ya kukosa shukurani inatoka wapi?
Mwanamume atakula kwa jasho na mambo mengine atayapata kwa jasho, ila mwanamke atazaa kwa uchungu....chunga familia nk kwa uchungu tu. Under "ceteris paribus"...yaani hayo mengine yote uko sahihi..na anayetakiwa kuyafanya ni mwanamke wala hakuna mjadala ila kichwa cha nchi ni Mwanamume..ukijikwaa kidogo usije ukasahau ukataka uhalalishe kwamba aendelee kukaa pale HAPANA
 
H

Hapo mwanaume "kichwa cha nchi" inategemea ni jamii gani - patrilineal au matrilinear . Ukienda kwenye matrilineal societies, hicho "kichwa cha nchi hakionekani". Nimekaa kwenye matrilinear society miaka 8, angalau nina uzoefu huo. Mwanaume, mfano, among the Chewa ni 'ceremonial' hana mamlaka kwa watoto, hata kwa mkewe. Hata mtoto akitaka kuolewa au kuoa si yeye anayetoa idhini. Na pia anayeamua nani atoke nyumbani akaishi anakotaka (kati ya mwanaume na mwanamke) ni mwanamke, na si mwanaume. In fact, mwanamke ndiye anayemfulumusha mwanaume kwa kumwambia "Toka hapa nyumbani, rudi kwenu" au "katafute sehemu nyingine ya kuishi. Sikutaki." Sasa hapo kichwa cha nchi ni nani, anayefulumushwa (asiye na mamlaka) au anayebaki nyumbani (mwenye mamlaka)?
 
sasa ndugu yangu sijauliza maana ya kutawaliwa au kuongozwa!, haya yote ni "nonsense"...mambo ya ccm kuongoza au mwanamke yote ya nini...??

Mwanamke kuwa TOP katika namna yoyote ile iwe kifamilia, kitaasisi au kiinchi..ni hatari sana kwa ustawi ...kiimani ama kikawaida yaani si kikristo ama kiislam. Huku tulikofikia sisi kama nchi..ni kwamba miaka minne hii "tumebeti" tumeshikilia roho mkononi kama taifa hatuna furaha kwasababu juu kabisa kuna mwanamke anaongoza/anatawala. Tumezoea na tutaendelea kuzoea nafasi za juu kabisa za kimaamuzi anakaa MWANAMUME hizo zingine za chini yake hamna shida akikaa mwanamke au mlemavu au yeyote asiyejiweza hakuna shida sana. Kwahiyo tuendelee kuelewa tu kwamba sisi wanaume wa taifa hili kwasasa tunaendelea kutawaliwa/kuongozwa na MSHANGAZI TU wala hakuna lingine 😎
Duh。。。!, hii male chauvinism ya kiwango hiki! kaz kwelkwel!。
P
 
Pale mwanzo hata mimi sikumuamini, na niliwahi kuuliza humu, Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais na nikawashangaa Watanzania wanamwamini Gwajima kuliko hata rais wao! Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko Rais wao?
Lakini baada ya Kuaminiwa na JPM..., who 'm I nisimuamini?. Tinga Tinga kumi , moja kila kata zitakuja, malari mawili ya mchanga kila kita yatakuja, zile boti 100 za kuvulia samaki zitaletwa, wale wavuvi 100 watapelekwa Marekani.

Hata hii treni ya umeme,
View: https://youtu.be/JTs_mLe9KLw?si=CO3C5sz2dt3t2dUw itakuja, bado tunasubiria uzinduzi siku chache zijazo.

Hata hii private jet Gulf Stream
View: https://youtu.be/xyTATLaaNOU?si=lOXPKf0suMQ1Uaaf
Itakuja.

Vuta tuu subra!.
P

Sasa hapa ndo nimekuelewa.
Kumbe unatumia "fasihi" kufikisha ujumbe.
 
Wanabodi,

Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari.

Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, sasa katika hizo tatu, media ya Tanzania inafanya vizuri katika eneo la uhabarishaji, na kutoa burudani, lakini katika uelimishaji, bado tuna matatizo, na katika eneo la uchambuzi wa habari, news analysis ndio kabisa, media zetu nyingi hazina uwezo huo, kwasababu hazina watu wenye uwezo huo, matokeo yake, mtu akisema kitu, media zinachukua na kukirusha tuu hivyo hivyo kama kasuku, bila kukichakata na kukifanyia analysis.

Juzi kati hapa rais wetu Mhe. Mama kazungumzia need ya Watanzania kumchagua rais mwanamke mwaka 2025 kwa kusema tutamsimamisha Mwanamke, media zimelidaka kama lilivyo kikasuku kasuku na kuanza kulivurumisha, hivyo kuleta mjadala mkubwa kwenye media na mitandao ya jamii, mara kaanza kampeni mapema, mara kajiteua, mara ni ubaguzi wa kuwabagua wanaume, mara hivi mara vile, hivyo bandiko hili ni kuwasaidia kidogo, kuwafanyia a simple analysis ya alichokisema rais Samia.

Kwanza ni ombi kwenu Watanzania wenzangu, kwanza tuunge mkono msimamo wa rais wetu Samia kuwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2025, tuufanye, sio tuu ni zamu ya kuchagua mgombea mwanamke, bali tuifanye ndio zamu ya ukombozi rasmi wa mwanamke katika siasa, sio tuu tuchague rais mwanamke, bali tuchague wabunge na wadiwani wanawake kwa wingi na kuifikia ile 50/50 ya azimio la Beijing na hata kupita, ila kwenye urais, sio lazima ndio awe Mama Samia, anaweza kuwa yeye au mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa kwasababu mpangaji sio yeye, wala sio sisi, mpangaji ni YEYE. Hivyo ikitokea, YEYE amepanga rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 awe ni mwanamke, then rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 atakuwa ni mwanamke, ila mwanamke huyo atakuwa ni yule aliyepangiwa na YEYE, kuwa rais wetu 2025, kama aliyepangiwa na YEYE ni yeye Mama Samia, then who are we kusema no?, kama ni yeye aliyepangiwa, na YEYE, then ni yeye!, ila kwa vile mpaka sasa YEYE bado hajasema kampangia nani, naomba Watanzania tuwe tayari kujiandaa kisaikolojia kuikubali mipango ya YEYE kwa mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa na YEYE kuwa rais wetu 2025 and not necesarly ni Mama Samia.

Hivyo mimi naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwasabubu kiukweli kabisa, wanawake wana uwezo sana wa uongozi na wengine kuliko hata wanaume, ila siku zote, tumekuwa tukiwakandamiza kutokana na kutawaliwa na mfumo dume kwa miaka nenda miaka rudi, na mpaka Mungu alipoingilia kati. Kama Mungu asingeingilia kati na JPM akaendelea hadi 2025, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke, lakini baada ya Mungu kuingilia kati na Tanzania kwa mara ya kwanza tukapata rais mwanamke, na Mama Samia ameisha onyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza, then why not 2025 asiwe mwanamke sasa sio tena kwa kudra za Mwenyeenzi Mungu bali kwa chaguo la Mungu kwa Tanzania na kupata endorsement ya Watanzania kwenye sanduku la kura, kumchagua rais mwanamke na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Na hili likifanyika na likakamilika kikamilifu, uchaguzi wa 2025 tukapata 50/50 ya wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufuta viti maalum, vitakuwa havihitajiki tena, vikiendelea kubaki ni wastage of time, money and resources.

Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, ila Mungu huweza kulikatiza chaguo lake wakati wowote na kumchagua mwingine, hii haikuanza leo, toka enzi za Nabii Musa, alikatizwa hakuingia nchi ya ahadi Canan, kwa sababu fulani. Everything happens for a reasons anazojua Mungu mwenyewe, hivyo hata Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania labda hadi 2025 ni Mungu tuu mwenyewe anajua. Kama Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema nasi hapa katikati kabla ya 2025, kwasababu hata JPM, hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, vivyo hivyo kwa Samia 2025, ni Mungu tuu pekee ndiye ajuaye amepanga nini na amempangia nani, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa sasa wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra tuu za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua utaratibu wa CCM, anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if ndivyo na YEYE alivyopanga!.

Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is sure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha mwanamke huyo ni lazima awe ni yeye!, anaweza kuwa ni mwanamke mwingine yoyote!. Hivyo ni busara kwa rais wetu Samia, kwa sasa, hili la ugombea wa 2025, asilizungumze zungumze sana kwa sasa, ni vyema akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kumpa Kaizari yaliyo ya Kaizari kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na kwa yale ya Kimungu, tumpe Mungu kwa kumuachia Mungu mwenyewe!.

Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

Nenda ukanisome in between the lines, nilisema nini kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, katika mabandiko haya. Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material? na hapa Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Ukiisha soma, kama una uwezo to read in between the lines, jibu utakuwa umelipata.

Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

2025 Twende na Mwanamke!.

Paskali
Update
Kuna hii sauti imeibuka Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Huyu aliyepo analikomboa vipi Taifa wezi anafanya nini, Deni la taifa kupaa zaidi, utekaji anachukua hatua gani kwa sasa mwanamke hapana
 
Back
Top Bottom