kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Wakati wa vurugu katiba na sheria vinasimama kufanyakazi kusudiwa. Kwenye vurugu na vita hakuna mwenye haki yake, vyote kwa 100% vinapotea ghafla halafu unabakia utawala binafsi, yarabi nafsi yangu. Kama DHAMIRA ya Waziri wa mambo ya ndani, Katambi ni kuzuia haki moja tu ili kulinda haki nyingine zote za kikatiba tunamuunga mkono kwa 100%. Akifanya hivyo atakuwa amechagua dhambi ndogo (the least evil).
Watu wakumbuke hata Sudani, Congo, Somalia, Ukraine, Iran, Lybia wana Katiba lakini hakuna haki wala demokrasia sasa hivi kwasababu ya makundi yaliyokuwa yakidai haki bandia. Kumechafuka na hakuna namna ya kurudisha haki za kikatiba katika nchi hizo.
Kama demokrasia inaweza kusababisha raia wasiokuwa na hatia wafe, wakimbie majumba yao, wakose matibabu, wawe vilema, wasiende shule wala kupata chanjo basi demokrasia hiyo haifai na ni batili. Kama kuna kifungu cha Katiba au sheria ambacho kinazuia kuzuia haya yasitokee nchini basi kifungu hicho tukifute mara moja.
Kama mkusanyiko unahamasisha uvunjifu wa amani kwanini mkusanyiko huo usizuie hata na mtu yeyoyote tu? Mfano, kwenye mkusanyiko mtu anapanga tumtoe mtu mahabusu mwenye kesi mahakamani au aliyefungwa kwa amri ya mahakama mkusanyiko kama huo sio sawa kiendelea kuwepo.