Ila kama Kuna kundi moja linatesa wengine na kufanya litakavyo ?
Kaka hiyo ni dhana tu inayopandikizwa ndani ya jamii. Wewe ni mtanzania, una ndugu, rafiki na jamii inayokuzunguuka, je, una mtu wako kati ya hao ambae ameteswa na hilo kundi linolotesa watu. Mimi hapa nina mke, watoto, wazazi, babu na bibi, ndugu, marafiki na jamaa zangu ambao hakuna hata mtu mmoja ambae ameteswa, kutekwa wala kuuliwa na hilo kundi unalosema lipo linatesa wengine. Hata hivyo, kati ya watu wangu mimi yupo amabae aliwahi kuwekwa mahabusu kwa mwaka mzima kwa tuhuma za wizi, upo aliyewahi kupigwa kwasababu ya kutembea na mke wa mtu.
Kaka nikwambie kitu ili kuwa salama kwenye nchi yoyote kuna wajibu lazima uutimize kwanza. Yaani kuna haki na wajibu, lakini wajibu lazima utangulie kabla ya haki kukufuata.
Siasa ni kazi kama kazi nyingine, na wako watu wametajirika kwa kazi ya siasa bila kujali anatoka chama gani. Hawa akina Sugu, Mbowe, Mnyika, Prof Jay, Mdee, nk wako vyama vya upinzani kama kazi, wanaishi kwa kazi hiyo, hivyo lazima wafanye siasa ili wale. Na ili upate watu wa kukusikiliza ni lazima upinge kila kitu cha chama pinzani hasa chama tawala. Wako tayari kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine kwasababu ya fedha bila kuwaomba radhi wala ruksa wafuasi wake. Hebu Ona watu waliohama vyama kwaajili ya kutafuta ni wengi sana hata kuwataja najisikia kichefuchefu, akiwemo Mchungaji Peter Msigwa.
Tumia akili yako kaka siasa ni mchezo mchafu, mzuri na hatari pia. Siasa ni ajira sawa na ajira nyingine tu, akina Sugu wana mahotel kwa kazi hiihii ya kukushawishi wewe uwapeleke bungeni na Ikulu na kupata ruzuku ya matanuzi. Usichome nchi yako kwa ahadi ya kujengewa nchi kama Canada, ni wapumbavu wanakudanganya.