Watanzania wako juu ya Katiba, Katambi yuko sahihi kuzuia mikutano

Gen Z wetu wala hawana neno bado, ukiona kobe juu ya mti kuna aliyempandisha.
 
Ila kama Kuna kundi moja linatesa wengine na kufanya litakavyo ?
 
Gen Z wamejifunza kwa namna ngumu sana katika lile tukio la October 29. Mpaka leo mwendokasi haupo kutoka pale Magomeni wilayani mpaka Morocco kwa sababu ya upuuzi wa hao vijana wanaodhani wanayo haki kuliko mtu yoyote.
Kaka kuna hesabu zilikwenda vibaya. Mpango mzima ulikuwa kuiangusha serikali, yaliyobakia yote unayoyaona sasa ni baada ya mpango kufeli. Hata huyu kaka yetu Lissu kuna watu walimsababishia shida hii ya sasa nadhani wanajilaumu sana kuona mhe. Lissu yuko pale sasa. Watu hao walianza kwa kumshauri/kumtaka achukue fomu agombee uongozi mkuu wa chadema.
 
Ila kama Kuna kundi moja linatesa wengine na kufanya litakavyo ?
Kaka hiyo ni dhana tu inayopandikizwa ndani ya jamii. Wewe ni mtanzania, una ndugu, rafiki na jamii inayokuzunguuka, je, una mtu wako kati ya hao ambae ameteswa na hilo kundi linolotesa watu. Mimi hapa nina mke, watoto, wazazi, babu na bibi, ndugu, marafiki na jamaa zangu ambao hakuna hata mtu mmoja ambae ameteswa, kutekwa wala kuuliwa na hilo kundi unalosema lipo linatesa wengine. Hata hivyo, kati ya watu wangu mimi yupo amabae aliwahi kuwekwa mahabusu kwa mwaka mzima kwa tuhuma za wizi, upo aliyewahi kupigwa kwasababu ya kutembea na mke wa mtu.

Kaka nikwambie kitu ili kuwa salama kwenye nchi yoyote kuna wajibu lazima uutimize kwanza. Yaani kuna haki na wajibu, lakini wajibu lazima utangulie kabla ya haki kukufuata.

Siasa ni kazi kama kazi nyingine, na wako watu wametajirika kwa kazi ya siasa bila kujali anatoka chama gani. Hawa akina Sugu, Mbowe, Mnyika, Prof Jay, Mdee, nk wako vyama vya upinzani kama kazi, wanaishi kwa kazi hiyo, hivyo lazima wafanye siasa ili wale. Na ili upate watu wa kukusikiliza ni lazima upinge kila kitu cha chama pinzani hasa chama tawala. Wako tayari kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine kwasababu ya fedha bila kuwaomba radhi wala ruksa wafuasi wake. Hebu Ona watu waliohama vyama kwaajili ya kutafuta ni wengi sana hata kuwataja najisikia kichefuchefu, akiwemo Mchungaji Peter Msigwa.

Tumia akili yako kaka siasa ni mchezo mchafu, mzuri na hatari pia. Siasa ni ajira sawa na ajira nyingine tu, akina Sugu wana mahotel kwa kazi hiihii ya kukushawishi wewe uwapeleke bungeni na Ikulu na kupata ruzuku ya matanuzi. Usichome nchi yako kwa ahadi ya kujengewa nchi kama Canada, ni wapumbavu wanakudanganya.
 
Gen Z wetu wala hawana neno bado, ukiona kobe juu ya mti kuna aliyempandisha.
Baada ya mapinduzi kushindwa wakaanza kujiliza kwa ICC wakitegemea SSH atapelekwa kushtakiwa huko The Hague.

Ukitaka kujua hawa wanatumwa, hawajali kabisa madhara ya ujinga wa kuichoma nchi hawajali kuhusu umaskini unaozaliwa baada ya nchi kuchomwa.
 
Tanzania kuna mahakama au kuna majengo ya mahakama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…