Watanzania waliokwama Ukraine kusaidiwa kuondoka na Russia kutaichafua Sana nchi kipindi ambacho Russia inatengwa na Dunia

India na China hawajailaani Russia. In the end wale waliompinga Joe Biden,in terms of world population ni wengi zaidi.
 
Hatima yake (wanasema)ni kwamba Russia wataiteka nusu ya Ukraine. Hawawezi kuiteka Ukraine yote kwa sababu wakifanya hivyo,yàani kwenda kwenye mipaka ya nchi ya NATO,italeta ubishi.
 
Wajuaji wa mambo mpo wengi kweli! We ulitakeje kwa mfano.
Yeye yupo nyumbani kwake Dar anaingia na kutoka muda wowote autakao hivyo anaongea anavyojisikia.

Mkuu vijana wetu wanateseka Ukraine, inatumika njia yoyote kuwaokoa, hayo mengine ya kumtenga Russia yatafuata baadae.
 
Putin hajawahi kufika Tanzania, ni habari ya uongo inayotembea whatsapp.
 
Unauhakika huo? Unajua majeshi ya Tanzania wakati huo wamepata mafunzo mengi Russia. Na wakufunzi wengi walitoka Russia. Nakumbuka nikiwa mdogo chipukizi, tulikwenda Russia kwa mafunzo ya mwaka mmoja, nilikuwa nasoma Shule ya msingi.

Tulifundishwa baadhi ya mbinu za kijeshi, namkumbuka Major general Mwita Marwa akija kutukagua, na tulifanya gwaride la heshima kwake, na baadae katika sherehe kubwa mbele ya Rais Nyerere. Tukapitishwa wachache sana tuliochaguliwa baadae kwenda Urusi.
Nadhani hujui mengi ya uvunguni kati ya Russia na Tanzania.
 
naona habari ya bwana Putin kuwahi kuja tanzania imekuja kuwa trend kubwa sana
 
Picha inayosemwa kuwa ni Putin na Samora ni Samora na komandoo mwingine wa kirusi mwaka 1984 siku ambayo Marehemu Samora alitembelea Bagamoyo kutizama mafunzo waliyokuwa wakipewa askari wa Msumbiji. Samora alifanya ziara Tanzania mwaka 1984 ndio akaenda hapo kambini.

Wale warusi walikuwa na makazi yao pale Gymkhana pembeni ya uwanja wa Golf miaka hiyo ya themanini na tisini.
 
Hongerasana mamasamiakwa kujalikila mtanzania atangekuwa injeyanchi Angekua mwendazakeangesema kwaniserikariimewatuma huko kumbukamsumbiji
 
Waondoke wote ila mtoto wa monalisa abakie kidogo
 
Honestly, kwa maoni yangu, mada yako inaongoza kwa kuwa ya hovyo tangu mwaka huu uanze.
Narudia tena, vita huijui hata kidogo. Wenzako wanakimbia kuokoa maisha yao, wewe unataka wachague njia ya kupita inayokufurahisha wewe kwa sababu za kisiasa ili uliyoiita nchi yako isipate doa?!
Wakati wewe hapo uko zako tu umetulia home unakula sijui kunde za wapi!
 
Tanzania siyo WANAFIKI. Nchi Ina misimamo yake na itaisimamia kweli. Hatuungi kitendo cha NATO kuihadaa Ukraine. Na hatujikombi kwa USA. Kwa hilo tunasimama na mwenye haki
 
Hujui ujamaa ulivyotufanya tutembee peku na kuishi kwenye nyumba za nyasi miaka 40 baada ya Uhuru. Maendeleo ya kisekta yamekuja kuanzia 1995. Tulipojiunga na uchumi wa dunia. Tukirudi tulipotoka ni shida

Sasa hapa vinahusiana nini na ujamaa?!
 
Waombe basi hao walioichokoza Russia wawasaidie ndugu na watoto wetu waliokwama Ukraine ili waweze kurudi salama.
Hata hivyo sikulaumu kwa sababu hujawahi kuwa na ndugu aliyeko kwenye mashaka ya maisha yake.
 
Kipi bora Watanzania wafe kwasababu ya kuitenga Urusi? Urusi na nchi za "Sadec" zina historia ndefu sana. Urusi na China ndio zilizosaidia ukombozi wa kusini mwa bara la Afrika. Je unajua undani wa vita kati ya Ukraine na Urusi? Ukidandia kwa kufwata vyombo vya habari vya magharibi utapotea. Poland nchi ambayo ilikataa wahamiaji toka Syria na Afghanistan, leo hii inasifiwa kwa kuwapokea wakimbizi wa Ukraine ambao ni wazungu wenzao, wamefanana hata nywele zao. Hii ndio dunia tunayoishi - fungua akili zako na si kuimba mambo ya vyombo vya habari vya magharibi.
 
Wanajustfiy tu! Basi lingefanyika kimya kimya sio kuonesha wema wa Urusi wakati ambao dunia inashuhudia ukatili wake wa Hali ya juu kabisa kwa watu wa Ukraine
Ni utapiamlo wa akili kufikiri kuwa wakati huu ambao Russia wako busy na jambo lao la vita kuwa wanawajali watu/wanafunzi wa nje ambao hata hawapo Russia bali wapo Ukraine.
 
Ndiyo maana tunasema nchi yetu haifungamani na upande wowote. Kwa sera yetu hiyo ya kutofungamana na upande wowote hatuna lawama kwa hilo
 
Kwa hiyo ulitaka wafe?,ungekuwa na nduguyo huko usingefurahia huu uamuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…