MK254,
..msimamo wa serekali yetu kuhusu mgogoro wa Sahara Magharibi vs Morocco unafedhehesha.
..na zaidi Mfalme wa Morroco ametupa "ZAWADI" kutokana na serekali yetu kulegeza msimamo.
..pamoja na hayo siwezi kuelekeza lawama zote kwa serekali ya awamu ya 5.
.Kwa kumbukumbu zangu Tz tulianza kujikomba-komba kwa Morocco wakati wa awamu ya 4. Naamini awamu ya 4 ndiyo waliobadilisha muelekeo wetu.
..walichokosea awamu hii ni kukubali "ZAWADI." kitendo hicho ni cha kujidhalilisha. Tungebadili msimamo wetu wa awali, lakini tukakataa "zawadi" watani zetu kama Kenya wasingetucheka kama inavyotokea sasa hivi.
..Sikutegemea tuboronge namna hii huku Wizara ya Mambo ya Nje ikiongozwa na mtu mwenye uzoefu kama Balozi Dr.Mahiga.
NB.
..hata siasa zetu za ndani nazo zimechukua muelekeo mbaya.
..CCM ya miaka hii inafanana na KANU ya enzi za Mzee TOROITICH ARAP MOI.