Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Pesa zetu, upange cha kuzinunulia wewe!!

Tena na unatutukana kabisa. Mnunulie mama yako na ndugu zako wqnatosha.
anajiona amewahi kununua jiko la umeme kwa hivyo sisi sote tumekuwa washamba
 
Kwahiyo umeshindwa kutangaza biashara kwa staha.
Ebu Acha mipasho bwn pesa zetu wenyewe alafu utupangie matumizi🤣🤣
 
Na siku hizi majiko ya umeme simple na ambayo matumizi yake ya umeme sio makubwa yako mengi tu. Bei iko reasonable

Watanzania wanathamini sana flat screens sijui wamerogwa
Kwaiyo umeamua ufanye biashara ya majiko ya umeme ili ututukane sasa?
 
Induction cooker sawa, ila jiko la umeme hapana.
Sawa ikiwa mtu ataweza kuafford induction cooker ni sawa uzuri wa hayo ni energy efficient

Iwe ni induction au electric bado inapunguza gharama
​
 
Mpaka miti iishe ndiyo tutanunua jiko la gesi.
 
Usitufokee bana umekuja kwangu ukakosa chakula? Iwe jiko la gesi au la umeme tunachohitaji msosi mtamu uje mezani
 
Mkuu, sio kuwa tunatakiwa kurekebisha chanzo. BEI YA UMEME. Punguzeni bei ya umeme watu watanunua majiko. TV ukiinunua kwa bei ghali matumizi yake yanakua ya gharama ndogo, mfano TV ya Inchi 55 ukiiwasha kwa masaa 24 itatumia unit 2 tu za umeme, ila jiko linalotumia Watt 2,500 ukilitumia kwa masaa 2.5 tu, unalinunua kwa labda laki 2 ila litatumia Unit 6 za umeme, sasa kwa mwezi mzima jiko tu litatumia unit 180 na hapo matumizi ni masaa 2.5 tu kwa siku na unit 1 ni Tshs. 357 hivi.

Kwa mwezi 1, jiko litakutoboa Tshs. 65,000/= ambayo hiyo ukinunua gesi utatumia miezi 2 kwa mapishi hayohayo unayofanya kwenye umeme. Punguzeni bei ya umeme, watu watanunua majiko.
 
ila jiko linalotumia Watt 2,500 ukilitumia kwa masaa 2.5 tu, unalinunua kwa labda laki 2 ila litatumia Unit 6 za umeme
Kwa nini ununue jiko la watt 2500? Utumie gesi masaa 2.5 kila siku utatoboa miezi 2?
 
Yaani mimi nilichoka sana, nilipoambiwa nilipie elfu 15 kama kodi ya kiwanja, sababu tu nyumba ina chumba juu (underground/ ghorofa). Kila sakafu ni Tshs. 7,500/= wakati nyumba za sakafu 1 wanalipa Tshs. 1,500/=
Unawaambia TRA sasa kwa nini kwenye ghorofa msichaji tu sakafu 2 kuwa Tshs. 3,000/=. Kuchaji elfu 15 si ni wizi kabisa huo?? Bongo ukinunua gari la miaka ya karibuni (latest) ushuru + kodi inakua kali, ukijenga ghorofa, kodi kubwa.. wanataka watu tuwe na magari ya zamani, tujenge nyumba za chini tu nk Think Tank wa serikali hao
 
Mkaa ndio habari ya mjini kwa sisi wachoma mahindi wa Mugumu Serengeti.
 
Tanzania inawaandaa watu waishi maisha ya kimasikini hata kama wana ajira unakuta mtu anajibana balaa kwa kila matumizi yake na pesa anayo kwa sababu ameandaliwa hivyo ni Watanzania wachache utawakuta wanaishi maisha wanayotaka wao maana serikali imewabana mno ila hao wanaokuja kukukagua wao wapo gorofani na wanalipia kidogo tu..
 
Kwa nini ununue jiko la watt 2500? Utumie gesi masaa 2.5 kila siku utatoboa miezi 2?
 
Kwa nini ununue jiko la watt 2500? Utumie gesi masaa 2.5 kila siku utatoboa miezi 2?
Si ndio standard. Jiko la single burner, induction cooker linakula watt 1600 huko, sasa utakua na jiko la single burner kwenye modern home?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…