Sajo
Platinum Member
- Nov 8, 2010
- 4,540
- 8,256
Kweli kabisa, mfano TANESCO, Hawataki kutoa ile tariff ya matumizi madogo, ambapo unaishia unit 75 kwa mwezi na gharama ni Tshs. 9,000/=, wanasema ni ya vijijini tu, ilhali mtu wa mjini anayelipa elfu 25 kwa mwezi (ambayo ni matumizi kwa nyumba nyingi za Tanzania) anakua amepata unit 70, hivyo angequalify kabisa kupata ile tarrif ya watumiaji wadogo. Lakini TANESCO haohao wanawapa wafanyakazi wao unit 50 bure kila mwezi.Tanzania inawaandaa watu waishi maisha ya kimasikini hata kama wana ajira unakuta mtu anajibana balaa kwa kila matumizi yake na pesa anayo kwa sababu ameandaliwa hivyo ni Watanzania wachache utawakuta wanaishi maisha wanayotaka wao maana serikali imewabana mno ila hao wanaokuja kukukagua wao wapo gorofani na wanalipia kidogo tu..