Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Tatizo umeme sio wa uhakika mfano unapika ugali mara umekatika si utaishia kunywa uji ndio maana watu wengi wanaishia kutumia gesi inakuwa na uhakika chakula kuiva bila shida
 
Kila kinachotendeka kwenye jamii ujue kimeshafanyiwa utafiti wa kina. Usijione Watanzania waliokataa kutumia majiko ya umeme ni wajinga kama ulivyosema ila huo ujinga ni wako wewe ambaye hujafanya utafi.

Katika vitu ambavyo vinakula umeme ni jiko la umeme. Hivi vingine pasi,friji havitumii umeme sana. Jiko linatafuna umeme hatari. Kama uko kwenye matumizi makubwa kama ulikuwa unatumia umeme wa 20000 kwa mwezi ukiongeza jiko itakula mpaka 45,000+ kwa mwezi. Na kama ulikuwa unatumia umeme wa 9000 kwa mwezi basi itabidi uende kwenye matumizi makubwa ukianza kutumia jiko,itakubidi uende mpaka 40+ kwa mwezi. Hii imefanyiwa utafiti
Weka basi ufafanuzi wa huo utafiti hapa
 
Nimekuwa nikitumia jiko moja la umeme watt 1500. Umeme matumizi madogo wa sh 5000 unabaki na kubaki kwa siku 30. Hapo jiko linapika wali, mboga na ugali. Jiko za kawaida hazili umeme labda uwe unazilisha
Jiko gani hilo mkuu. Weka picha na details, ndio haya wanayosema induction cooker?
 
Shida ni,Umeme kuwa ghali,Umeme kutokupatikana wakati wote na Mkaa.
Ukipiga hesabu vizuri unaweza kukuta gharama ni zilezile au zaidi ya hapo, kumbuka jiko la umeme linatumia muda mchache tofauti na la mkaa.
 
20260512_213829.jpg
 
Gas ikiisha unasikia Watanzania wajinga wakisema "sijui kwa nini gesi lazima iishe usiku."

Sawa gas imeisha usiku kwa nini usingekuwa na backup ya jiko la umeme?

Utamsikia Mtanzania anakwambia jiko la umeme linatumia umeme mwingi, ok well mbona ndani una vyombo vingi sana vya umeme na haulalamiki?

Kwani jiko la umeme unalitumia siku nzima?

Mtu ana flat screen ya milioni lakini jiko la umeme hata la plate 2 linamshinda.

Kuna ujinga mwingi sana kwenye jamii ya Watanzania, pesa ya kufanya au kununua vitu vya kijinga wanazo ila kuongeza units za umeme awe anatumia jiko la umeme hana.


​
Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt

1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa

Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh

Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh


Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-290 kwa wateja wa kawaida

60kWh×Tshs 290 unapata 18,000/=

Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?

Pia siku hizi kuna majiko janja ya umeme ya induction haya kwenye matumizi ya nishati ya umeme ni rafiki sana na ni teknolojia ya kisasa. Ukinunua induction cooker hautajuta
​
majiko ya umeme yanayofaa ni aidha infrared au induction
 
Back
Top Bottom