Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Gas ikiisha unasikia Watanzania wajinga wakisema "sijui kwa nini gesi lazima iishe usiku."

Sawa gas imeisha usiku kwa nini usingekuwa na backup ya jiko la umeme?

Utamsikia Mtanzania anakwambia jiko la umeme linatumia umeme mwingi, ok well mbona ndani una vyombo vingi sana vya umeme na haulalamiki?

Kwani jiko la umeme unalitumia siku nzima?

Mtu ana flat screen ya milioni lakini jiko la umeme hata la plate 2 linamshinda.

Kuna ujinga mwingi sana kwenye jamii ya Watanzania, pesa ya kufanya au kununua vitu vya kijinga wanazo ila kuongeza units za umeme awe anatumia jiko la umeme hana.

​
Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt

1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa

Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh

Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh

Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-290 kwa wateja wa kawaida

60kWh×Tshs 290 unapata 18,000/=

Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?
​

Huu ndiyo ule mradi wa yule mhuni?
 
Nafikiri shida iko hapa:
1.Tamaduni - watu wametoka kwenye kuni na mkaa: tumekua, tumezaliwa tunaona kuni, mkaa tunapika.
2.Kabla ya REA: Miaka ya nyuma umeme ulikua upo sehemu chache sana.Vijijini haukuwepo..thus hakuna mtu angeweza kupiga campaign ya kitu ambacho the mass hawawezi kutumia.Mpaka imejikuta imezoeleka kwa watu kuwa na nishati mbadala
3.Hizi gas ziko kwa wafanya biashara, zimepigiwa promo sio ya nchi hii, hujaskia MITUNGI YA MAMA, wanaenda mpaka vijijini wanatoa bure, mitungi ipo kila kona, hata kama hutaki utanunua tu.
4.Elimu elimu, watu tupewe elimu tu, tutatumia
 
Na siku hizi majiko ya umeme simple na ambayo matumizi yake ya umeme sio makubwa yako mengi tu. Bei iko reasonable

Watanzania wanathamini sana flat screens sijui wamerogwa
Binafsi sina jiko la umeme na sababu sio gharama ya umeme bali ni uhakika wa kuwa na huo umeme masaa yote haupo.

Halafu tusipotumia Taifa Gas si Rostam atafilisika?
 
Nafikiri shida iko hapa:
1.Tamaduni - watu wametoka kwenye kuni na mkaa: tumekua, tumezaliwa tunaona kuni, mkaa tunapika.
2.Kabla ya REA: Miaka ya nyuma umeme ulikua upo sehemu chache sana.Vijijini haukuwepo..thus hakuna mtu angeweza kupiga campaign ya kitu ambacho the mass hawawezi kutumia.Mpaka imejikuta imezoeleka kwa watu kuwa na nishati mbadala
3.Hizi gas ziko kwa wafanya biashara, zimepigiwa promo sio ya nchi hii, hujaskia MITUNGI YA MAMA, wanaenda mpaka vijijini wanatoa bure, mitungi ipo kila kona, hata kama hutaki utanunua tu.
4.Elimu elimu, watu tupewe elimu tu, tutatumia
Namba 3 bold ...Watanzania hawanunui kabisa ya umeme
 
Hivi jiko la coil na induction tofauti yake nini?
Induction ni teknolojia mpya ya majiko janja ya umeme yanafanya kazi kwa mfumo wa electromagnetic.

Kwa matumizi ya nishati ya umeme ni rafiki sana na yako yanatengeneza heat haraka sana kuliko yale ya traditional electric cooker.

Screenshot_20250904-131722_Chrome.jpg
 
Mimi nilijua hili muda kidogo nilifanya kunua majiko tofauti ili nione lipi litakua na matumizi kidogo nikayapata baadhi ndio natumia huko gharama ya gesi ipo juu sana kuliko kutumia majiko sahihi ya umeme na pia watu hawapati elimu ya kutosha ili watu wachache wenye ubia na makampuni ya gesi waendelee kupata pesa..
Samahani,, unaweza kunitajia majiko mazuri yanayotumia umeme nafuu isiwe ya kioo Nina wanajeshi ndani.
 
Samahani,, unaweza kunitajia majiko mazuri yanayotumia umeme nafuu isiwe ya kioo Nina wanajeshi ndani.
Sasa hivi unachukua jiko la umeme lenye plate za kuchanganga mbili umeme na mbili gesi mimi vitu vyangu mara nyingi nanunua huku SA ndio nakuja kutumia huko maana huko wana majina yao ambayo sipo familia nayo sana na wanauza bei juu sana kama unataka ya hapa nitakuangalizia utalipia bei ya duka mimi ntakuchaji gharama ya kulileta tu huko daslm sina picha hapa nikienda macro ntakumia..
 
Sawa,, Asante
 
Shukrani ngoja nitafute,, kampuni ipo nzuri??
Kwa Tanzania kwa sasa kuna kampuni 2 tu za induction cooker zote zinafanya vizuri

Positive cooker ni Watanzania
ECOA hawa ni Wakenya

Uzuri haya ya Tanzania yana ruzuku ya shirika la UNDP hivyo bei yake iko chini ukilinganisha na ECOA ya Kenya

Usijichanganye ukaenda kwingine zaidi ya kwa mawakala wao

Ukienda Kariakoo utaishia kuuziwa majiko ya infrared watakwambia ndio induction hawajui tofauti ya induction na infrared cooker

Kwa kifupi Kariakoo hakuna majiko ya induction
 
Walisemaga umeme wa Julius Nyerere sijui wa mto rufiji ukianza, hivi utakua bado haujaanza kuzalishwa au wamesahau kupunguza bei tuwakumbushe?
 
Back
Top Bottom