Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Tanzania inawaandaa watu waishi maisha ya kimasikini hata kama wana ajira unakuta mtu anajibana balaa kwa kila matumizi yake na pesa anayo kwa sababu ameandaliwa hivyo ni Watanzania wachache utawakuta wanaishi maisha wanayotaka wao maana serikali imewabana mno ila hao wanaokuja kukukagua wao wapo gorofani na wanalipia kidogo tu..
Kweli kabisa aisee. Yaani watu tungeweza kabisa kununua magari ya kisasa, kuishi kwenye makazi bora na tukalipa kodi vizuri kabisa, ila serikali ndio hivyo inapambana sana kuhakikisha tunaishi kimaskini kiasi tunaogopa hata kununua majiko ya umeme. Juzi nimenunua mafuta ya Taa, lita 1 ni Tshs. 4,000/= hapa Dar, sasa haya mafuta ndio yalikuwa msaada kwa wanavijiji huko ndichi ambako REA hakuna mpaka leo wala hawawezi kununua mitungi ya gesi. Wataweza kweli kununua mafuta ya taa kwa jinsi yalivyo ghali?
 
Mtoa mada ni mpumbavu. Tanzania pamoja na kuwa na idadi ya watu inayokaribia milion 70 ina nyumba za makazi ambazo hasizidi milion 11 . Hii inamaana zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanashea nyumba na umeme, umeme wa kushea kidesturi haufai katika matumizi makubwa kwan ni chanzo cha migogoro
 
Kila kinachotendeka kwenye jamii ujue kimeshafanyiwa utafiti wa kina. Usijione Watanzania waliokataa kutumia majiko ya umeme ni wajinga kama ulivyosema ila huo ujinga ni wako wewe ambaye hujafanya utafi.

Katika vitu ambavyo vinakula umeme ni jiko la umeme. Hivi vingine pasi,friji havitumii umeme sana. Jiko linatafuna umeme hatari. Kama uko kwenye matumizi makubwa kama ulikuwa unatumia umeme wa 20000 kwa mwezi ukiongeza jiko itakula mpaka 45,000+ kwa mwezi. Na kama ulikuwa unatumia umeme wa 9000 kwa mwezi basi itabidi uende kwenye matumizi makubwa ukianza kutumia jiko,itakubidi uende mpaka 40+ kwa mwezi. Hii imefanyiwa utafiti
 
Si ndio standard. Jiko la single burner, induction cooker linakula watt 1600 huko, sasa utakua na jiko la single burner kwenye modern home?
Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt

1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa

Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh

Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh

Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-250 kwa wateja wa kawaida

60kWh×Tshs 250 unapata 15,000/=

Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?
​
 
Ukiwa unapika. Lakini pia licha ya mapungufu ya umeme wa Tanesco muda wa umeme kuwepo ni mwingi hivyo haiwezi kuathiri kivile kwenye mapishi. Ukikata hapo unacheza na gesi au mkaa. Chakula lazima kiliwe​
Nikiwa na gesi au mkaa ,uhakika wa kupika na kuivisha ni 100% ila kwa Umeme ni mashaka!
 
Kweli kabisa aisee. Yaani watu tungeweza kabisa kununua magari ya kisasa, kuishi kwenye makazi bora na tukalipa kodi vizuri kabisa, ila serikali ndio hivyo inapambana sana kuhakikisha tunaishi kimaskini kiasi tunaogopa hata kununua majiko ya umeme. Juzi nimenunua mafuta ya Taa, lita 1 ni Tshs. 4,000/= hapa Dar, sasa haya mafuta ndio yalikuwa msaada kwa wanavijiji huko ndichi ambako REA hakuna mpaka leo wala hawawezi kununua mitungi ya gesi. Wataweza kweli kununua mafuta ya taa kwa jinsi yalivyo ghali?
Electrical appliances bongo ni ishu tunaua vision ya macho kwa kutumia TV ambazo hazina ubora mpaka leo tupo busy kuuliza ipi TV nzuri au pasi nzuri kwa sababu kodi zake zipo juu sana watu wanapoteza muda kwa kufua nguo kwa mikono kwa sababu hizo washing mashine ni anasa ukimwambia mzawa zipo za mashine za kuosha sahani tena bei ndogo mzawa hawezi kuamini vitanda tunatumia vyenye magodoro ya kunesa watu wengi tuna matatizo ya migongo tukidhani ni umri kumbe ni kutumia vitu visivyo na ubora kwa muda mrefu wanaotakiwa kusimamia ubora wapo busy na vitu vya hovyo hovyo macro Johannesburg huwa wanakua na Friday sale bei inakua sawa na bure kabisa kwa vitu ambavyo Tanzania kuvipata mpaka utoe jasho kweli ila nunua kipeleke Tanzania watakuja watu kukikagua hapo ili mradi ushindwe kulipia tu harafu wao wapate bure..
 
Gharama ya umeme ipo juu kidogo Tanzania ingawaje ukitumia kama backup sio mbaya
Hapana kwa Tanzania unless unalinganisha na Bure (kijijini kuokota kuni) basi ndio itakuwa juu Ingawa kijijini Tariff Zero ni 100/= per Unit; kwahio kwa Tanzania Umeme upo chini kwa sasa in comparison na gesi

maana umeme huo huo unalipia kiwanja chako pia una VAT
Kiwanja sio kwamba unalipia ukitumia umeme kiwanja unalipia regardless ila Umeme ni platform ya kukusanya hizo 18,000/= kwa mwaka hivyo utumie usitumie utalipa hio pesa, na VAT hata ikiwekwa bado umeme is cheaper
na wanatamani waweke Import duty ingawaje umeme ni wa kwetu wao wataweka tu na kusema unatoka Ethiopia maana wa Mtera una gharama sana Wabongo wakishapata madaraka sio watu kabisaa.
Huo ndio upuuzi sababu kama wamesema kuna umeme ziada wangeweza kushusha zaidi hata Tshs 20/= per Unit ili tusitumie Kodi zetu kuagizia LPG ambayo ndio inatumika majumbani.... Tena sio Tshs 20/= hata watu wangeweza kupikia bure kwa umeme kwa kupata credit kwa kuwauzia Tanesco Umeme kwa wanaokusanya kwenye Solar Panels zao

Kuna majiko ya single burner yana 1000 watt

1000 watt ni sawa na 1kWh kwa saa

Tuseme kwa kadirio la juu unatumia jiko kwa masaa 2 kila siku yaani 2kWh

Kwa siku 30 za mwezi utakuwa umetumia 60kWh

Kwa sasa Tanesco wanachaji 1kWh kwa Tshs 100-250

60kWh×Tshs 250 unapata 15,000

Kwa mwezi unaweza kutumia gesi ya shilingi ngapi?
​
Sema yale hayo majiko yanahitaji sufuria zile ngumu upo sahihi mkuu toa elimu ili watu watoke waliko karirishwa.
 
Hapana kwa Tanzania unless unalinganisha na Bure (kijijini kuokota kuni) basi ndio itakuwa juu Ingawa kijijini Tariff Zero ni 100/= per Unit; kwahio kwa Tanzania Umeme upo chini kwa sasa in comparison na gesi

Kiwanja sio kwamba unalipia ukitumia umeme kiwanja unalipia regardless ila Umeme ni platform ya kukusanya hizo 18,000/= kwa mwaka hivyo utumie usitumie utalipa hio pesa, na VAT hata ikiwekwa bado umeme is cheaper

Huo ndio upuuzi sababu kama wamesema kuna umeme ziada wangeweza kushusha zaidi hata Tshs 20/= per Unit ili tusitumie Kodi zetu kuagizia LPG ambayo ndio inatumika majumbani.... Tena sio Tshs 20/= hata watu wangeweza kupikia bure kwa umeme kwa kupata credit kwa kuwauzia Tanesco Umeme kwa wanaokusanya kwenye Solar Panels zao

Mkuu usitumie nguvu kunijibu nasema Tanzania umeme upo juu Tsh 5000 inanunua unit 98 Zambia wakati kwa Tanzania sijui utapata unit ngapi kwa hizi Nchi Zambia,SA na nchi zingine tunatumia umeme kwa kupikia,kuoga maji moto maji baridi na vitu vingine na unit utakazotumia kwa mwezi ni kawaida sio nyingi kama Tanzania ambako watu wanaotumia maji moto maji baridi ni wachache sana.
 
Tuseme Jiko la umeme lina Watt 2000 japo ni kadogo kwa umbo ukikawasha ni kama umewasha TV kumi za inchi 65 kwa pamoja. Tuchukulie hauna matumizi mengi Unatumia kwa masaa mawili kwa siku ni unit 4, kwa mwezi unit 120 ambao ni umeme wa kama 50,000!
Bongo bei ya umeme haipishani na nchi za mabeberu wakati average income tunatofautiana pakubwa sana.
Unapika nini kwa kutumia watt 2000 hapo na uki convert hizo watt 2000 kwenye gesi ni kama umetumia lita ngapi ?

Issue ni appliances sasa hivi kuna slow cooker ambayo inaweza kuivisha chini watts 200 (ambayo hio zamani ilikuwa ndio taa ya nje moja ambayo ilikuwa inawaka usiku kucha)

Kuna Pressure Cooker, kuna Jug Kettle kuchemshia maji..., na hapo wala sijaongelea Induction Cooker

Kwahio kwa Bongo tunachohitaji zaidi ni Elimu kuhusu umeme na watu kutambua kwamba hio gesi tunailipia Kodi na kuiagiza na ruzuku hivyo tuweze kushinikiza serikali ishushe umeme sababu ni Huduma na sio Biashara....

Mkuu usitumie nguvu kunijibu nasema Tanzania umeme upo juu Tsh 5000 inanunua unit 98 Zambia wakati kwa Tanzania sijui utapata unit ngapi kwa hizi Nchi Zambia,SA na nchi zingine tunatumia umeme kwa kupikia,kuoga maji moto maji baridi na vitu vingine na unit utakazotumia kwa mwezi ni kawaida sio nyingi kama Tanzania ambako watu wanaotumia maji moto maji baridi ni wachache sana.
Tshs. 5,000 hapa Tanzania unapata unit 14 mkuu kwa tarrif ambayo ndio tupo watanzania wengi
 
Yes Umeme Tanzania ni Gharama kulingana na kwamba unaweza ukashuka sababu kuna vyanzo vingi ila haupo juu kushinda gesi, Gesi ipo juu zaidi ila ndio hivyo propaganda za wauza Gesi

Tanzania Unit kwa Tariff Zero ambapo ndio wanagawiwa mitungi bure ili waweze kuingia kwenye hii Biashara ya watu ni kwamba Kwa Tshs elfu Tisa na Ushee unapata units 75; na wakati huo huo kwa gesi unit moja ni kama mia tatu na ushee

Kwahio point yako kwamba wanatumia umeme sababu ya gharama ya umeme ni void ab initio; ofcourse ni kweli kama wanatumia kuni sababu ni bure..., ila kama wanatumia gesi ni kutokana na miss information
 
Tshs. 5,000 hapa Tanzania unapata unit 14 mkuu kwa tarrif ambayo ndio tupo watanzania wengi
Zambia kununua umeme hauna kodi ndio maana wanapata unit nyingi na pia hizi nchi mtu akiondoka nyumbani kuzima taa sio big ishu kama Bongo mtu anaweza kurudi kisa kasahau kuzima taa mbili sio kwa sababuya usalama hapana kwa sababu ya bill ya Tanesco.
 
Tshs. 5,000 hapa Tanzania unapata unit 14 mkuu kwa tarrif ambayo ndio tupo watanzania wengi
Na kwa gesi elfu tano unapata Units ngapi ? Ukiweka na ufanisi wa vyombo vya umeme sasa hivi plus Kodi yako ambayo inalipwa kama ruzuku sababu ya gesi utajikuta kwamba kama Mtanzania unakuwa short changed

1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 15kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 15kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 15kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 15 equals to approx = 204 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 15 una Units takriban 204
Kwa mchanganuo mrefu angalia

Umeme wa tanesco sio wa kuuamini. Kuña kipindi ulikua unakata kisha unarudi mkali sana watu walipata hasara za kutosha
 
Yes Umeme Tanzania ni Gharama kulingana na kwamba unaweza ukashuka sababu kuna vyanzo vingi ila haupo juu kushinda gesi, Gesi ipo juu zaidi ila ndio hivyo propaganda za wauza Gesi

Tanzania Unit kwa Tariff Zero ambapo ndio wanagawiwa mitungi bure ili waweze kuingia kwenye hii Biashara ya watu ni kwamba Kwa Tshs elfu Tisa na Ushee unapata units 75; na wakati huo huo kwa gesi unit moja ni kama mia tatu na ushee

Kwahio point yako kwamba wanatumia umeme sababu ya gharama ya umeme ni void ab initio; ofcourse ni kweli kama wanatumia kuni sababu ni bure..., ila kama wanatumia gesi ni kutokana na miss information
Mimi nilijua hili muda kidogo nilifanya kunua majiko tofauti ili nione lipi litakua na matumizi kidogo nikayapata baadhi ndio natumia huko gharama ya gesi ipo juu sana kuliko kutumia majiko sahihi ya umeme na pia watu hawapati elimu ya kutosha ili watu wachache wenye ubia na makampuni ya gesi waendelee kupata pesa..
 
Zambia kununua umeme hauna kodi ndio maana wanapata unit nyingi na pia hizi nchi mtu akiondoka nyumbani kuzima taa sio big ishu kama Bongo mtu anaweza kurudi kisa kasahau kuzima taa mbili sio kwa sababuya usalama hapana kwa sababu ya bill ya Tanesco.
Naangaliaga tamthilia ya Mpali DSTV, unakuta nyumba za vijijini kabisa huko Zambia wanatumia majiko ya umeme (Oven).
 
Naangaliaga tamthilia ya Mpali DSTV, unakuta nyumba za vijijini kabisa huko Zambia wanatumia majiko ya umeme (Oven).
Ndugu yangu mmoja amesoma pale anasema Tanzania mnapata hela kama Nchi masikini ila matumizi yake ni ya ki Hong Kong vitu vipo juu mno wao mambo ya router home ni muda mrefu kodi ya hilux haizidi Tsh 8m wakati ukija nalo Tanzania utaliacha boda na wana sheria ya kunyang'anya mali ukishindwa kulipia kodi ndio limeenda hilo ukiangalia hata Bus analopanda mzambia kusafiri ni tofauti na sisi ingawaje wao wameamka juzi tu kwenye usafirishaji wa abiria walikua wanaenda mjini kulishangaa Scandinavia bus wao leo wapo na series Ir 8 iriza body.
 
Back
Top Bottom