Mkuu, naona hesabu zako zina tofauti kubwa sana na uhalisia:
View attachment 3345039
1) Mteja mwenye matumizi ya unit 0-75 kwa mwezi analipa 100/= kwa unit 1, sasa kwa mfano wako hapo juu unit 75-60(za jiko tu) anabaki na unit 15 tu za matumizi mengine yote ya umeme (taa, TV, friji n.k) yaani atumie unit 0.5 kwa siku. Inafikirisha sana
2) Mteja kwenye matumizi ya unit 76 na zaidi kwa mwezi analipa 350/=( ya kwenye makaratasi tu ya uhalisia ni 356.35562087/=) ambayo ni 78% umeme, 18% VAT, 1% EWURA, 3% REA. Unit 60 × 356.3556087/= unapata 21,381.337252/=
Mtungi mdogo wa gesi unauzwa 22,000/= (butane 6 kgs)
Bei ya mtungi wa gesi Vs jiko jipya LA umeme
Jiko la umeme linaweza kupata hitilafu na hivyo kuhitaji ufundi, gharama za Fundi wa vifaa vya umeme zinahusika. Sijapata kuona mtungi wa gesi na jiko lake vimeharibika.
Wapishi karibuni mtueleze hilo la muda wa kupika (Masaa 2 kwa siku kwa mujibu wa mleta mada)
Na muda wa kupika chakula X kwenye gesi Vs kwenye jiko la umeme. Karibuni sana waungwana