Watanzania Wana shida gani mbona hawalipi kisasi( Retaliation)Kwa walioua ndugu zao?

Kila mfano wa watu waliopigwa majumbani ni master Tindwa na Sheikh Shariff Majini. Leteni na majina mengine basi ili m-justfy hoja yenu ya kwamba watu waliuliwa majumbani
 
Sasa hivi unamuona huyo Mahita yuko sawa kisaikolojia na kiafya?
 
Kila mfano wa watu waliopigwa majumbani ni master Tindwa na Sheikh Shariff Majini. Leteni na majina mengine basi ili m-justfy hoja yenu ya kwamba watu waliuliwa majumbani
Picha hiyo hapo ya tukio la Arusha yule mama aliyepigwa risasi nyumbani kwake huoni damu mlangoni au umevaa miwani ya mbao?
 
Kila mfano wa watu waliopigwa majumbani ni master Tindwa na Sheikh Shariff Majini. Leteni na majina mengine basi ili m-justfy hoja yenu ya kwamba watu waliuliwa majumbani
Madai ya matumizi mabaya ya silaha hayatolewi na wana JF pekee au mitandaoni pekee, tume pia imetoa haya madai. kujustfy hoja si hoja tena, hoja ni kuelewa why? Kwanini ilikuwa lazima wauwawe?
 
Zamani sikuelewa waarabu wawili kufunga minyororo msafara wa vijeba na kuwaswaga kama mifugo miles kibao ila sasa ndiyo naelewa!!
 
S. a unaona watz wanapigwa hata hawajitetei. Mrusi kapigwa kasambaza ngumi mpaka vijana wa s.a wakaomba poo
 
Most ya walioingia kwenye vurugu za 29/10 ni majobless, vibaka (panyaroad) na mateja. Kuna wengine wameshukuru kupunguziwa ghasia. Kwa hiyo suala la kisasi halipo
Kwa maoni yako walistahili kuuliwa badala ya kuwashitaki ili mahakama ziwahukumu kwa haki? Nakuombea ili uzao wako wasikosekane majobless na vibaka na ikimpendeza Mungu akujazie wote. Una roho mbaya kuliko shetani.
Kwani hao siyo binadamu?
 
Ma jobless kwenye vituo vya mabasi, sokoni, na kwenye mikusanyiko wako very vulnerable kujiunga na makundi ya jinai au uhalifu kwa sababu hawana shughuli.

That's fine if it fits your narrative, but petty thieves aren't Tanzania's problem. Wote tunajua kwanini vijana walipigwa bunduki, labda tujitoe ufahamu tu
 
Usifundishe mambo ya visasi, kulipizana visasi ni jambo baya,wewe ni mtu wa namna gani?
 
Usifundishe mambo ya visasi, kulipizana visasi ni jambo baya,wewe ni mtu wa namna gani?
Huyo katoka hapa miaka ile wazazi wako serikali hii hii kimagumashi kapigiwa pande aende US kwa nafasi za watoto masikini,hata hajawahi kuijua nchi yoyote hasa Africa jinsi ya hizo nchi maisha yanavyokwenda anapayuka tu na kutaka vita itokee bongo.
Nimeenda sana Rwanda, ajifunze huko, leo hii watutsi na wahutu wanaishi pamoja, hata kama wahutu walifawafanyia unyama uliopita maelezo watutsi, lakini hakuna visasi leo hii.
Hata Kenya wameshasahau na Late Odinga alikubali yaishe waanze upya.
 
Hatuko hivyo kwa sababu hatujui kupigania haki zetu na kujitetea tunapoonewa. Nchi za wengine huyo mama yako asingejitapa mbele ya media kuua wananchi wake kiasi kile kwa jeuri.
 
Kila mfano wa watu waliopigwa majumbani ni master Tindwa na Sheikh Shariff Majini. Leteni na majina mengine basi ili m-justfy hoja yenu ya kwamba watu waliuliwa majumbani
wanatajwa hao kwa sabb ni maarufu, nikikutajia Mwajuma Hassan nae aliuwawa ndani kwake, ww utamjua? watu wa lumumba akili mnaziachaga wapi?
 
Wakati Tanganyika ikipata Uhuru wake, wazee wa Pwani walifanya tambiko la kiti cha urais, rais mwenyewe pamoja na makazi yake. Waliweka alama kuu mbili za kudumu za kinga dhidi ya watu wote wenye nia mbaya naye ama kiti chake.

Kwanza waganga wa kienyeji walikuja na madai ya kumpa "kinga" rais na urais wake kupitia alama ya "mwenge" ili asilogwe, asianguke, asichoke, au achaguliwe tena katika kila mwaka wa uchaguzi.

Pili, ndege aina ya tausi aliwekwa katika makazi ya ikulu kwa imani za kishirikina. Waganga waliamini itakuwa ni alama kuu ya ulinzi wa rais. Watu wote wenye nia mbovu naye watapata bahati mbaya, umasikini, au hata kifo. Wanaamini "macho" yaliyopo kwenye manyoya ni macho ya ulinzi ya mizimu, ama ni kinga thabiti dhidi ya uchawi. pamoja na majini.

Hizi alama ndizo alama kuu za kuwapumbaza Watamzania. Ili kulinda kinga hizi makafara hufanywa na marais ikiwemo umwagaji mkubwa wa damu za wananchi katika kila awamu ya urais katika mazingira ya kutatanisha zikiwemo ajali, utekaji utesaji, mauaji, n.k. kuendana na mahitaji na imani za mkalia kiti.

Kwa jnsi mkalia kiti anavyoluwa mbali na hofu ya Mungu, ndivyo kadiri ambavyo huvitumia vibaya vyombo vya dola katika kafara zake. Vinatumika vibaya kukandamiza wananchi na kumwaga damu nyingi zizokuwa na hatia.

Kwa hiyo basi, ni vigumu mno kwao kufanya kisasi kwa matendo ya kafara za kipagani yanayokuwa "manipulated" na Kiri kikuu.

Katika ripoti ya Jaji Chande amegusia kidogo kuhusu mambo hayo na kusema mojawapo ya sababu ya watu kupotea na kutojulikana walipo ni ushirikina na mapenzi!

Yaani Tume iimekuja na findings na kuweka code kuhusu mapenzi ya viongozi yatimizwe kwa sababu zap za kafara za kishirikina.
 
Naamini una point nzuri sana sana, if you revenge wataona kutuua ni haki yao.... wekeni mkakati
 
anyway, umewajumuisha watanzania kuwa hawalipi kisasi, wewe umelipa kisasi gani mpaka mda huu, ukiachana na kuwajaza watu upepo
 
Diaspora mna mental health sioni umuhimu mpaka mna mawazo yaliyopitwa na wakati.

Badala ya ku-share ideas za msingi nyie mnajaza watu upepo waandamane , wauliwe , walipe visasi n.k

Huku nyie na familia zenu mkiwa safe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…