SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
,Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati? - Zitto Kabwe
Tangu jana nimeona shamrashamra kubwa kuhusu kinachoitwa mafanikio ya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Kati. Kuingia Uchumi wa Kati ni hatua nzuri lakini inayohitaji ufafanuzi wa kiuongozi. Hatua hii ikifanyiwa propaganda itaonekana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano wana uhaba wa mafanikio au hawajui wanachoshangilia. Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu...