Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Uchumi wa kati bila udikiteta ndiyo hunoga, kuwa na uchumi wa kati huku ukikandamiza demokrasia lazima ushuke kurudi kwenye uchumi wa chini tena, bila demokrasia hakuna maendeleo yatadumu
 
Mkuu Kama anaka kujibiwa Basi mwambie apeleke hoja zake hizo World Bank walioitanga Tanzania kufikia huo Uchumi wa Kati.

Hakuna Mtanzania wa Aina yoyote Ile alieamuka asubuhi na kwenda kutangaza kuwa tumefikia Uchumi wa Kati.

Sasa nashangaa Kama vile wapingaji wa taifa wanaanza kuilaumu serikali ya Tanzania kuhusu huu Uchumi utafikiri imeua Wala kumukwaza mtu.
Nini kazi ya upinzani? Kazi ya upinzani ni kupinga mapungufu kukosoa Serikali iliyopo madaktari , kazi ya upinzani siyo kufagilia maigizo ya CCM.
 
Mkuu Kama anaka kujibiwa Basi mwambie apeleke hoja zake hizo World Bank walioitanga Tanzania kufikia huo Uchumi wa Kati.

Hakuna Mtanzania wa Aina yoyote Ile alieamuka asubuhi na kwenda kutangaza kuwa tumefikia Uchumi wa Kati.

Sasa nashangaa Kama vile wapingaji wa taifa wanaanza kuilaumu serikali ya Tanzania kuhusu huu Uchumi utafikiri imeua Wala kumukwaza mtu.
1593807571067.png
 
Ulitaka tufanyeje maana per capita income ndiyo inayotumiwa kupima hizo nchi sasa ulitaka waseme siyo. Hata hizo nchi zilizoendelea nazo hupima hivyo hivyo.
 
Tatizo la Upinzani wa nchi hii huwa hakubali lolote kwao kila Kitu ni kukosoa tu!!

Zitto Kabwe ndio ulibaki mpinzani Pekee niliekukubali Sana Ila nilikuona mtu ambae huna jema siku ya kuvunjwa Bunge la TZ kwà mwaka 2015-2020, Ile siku unahojiwa ukadai et Rais wa awamu ya 3 na 4 walihutubia Bunge Mara 3 Hadi 4 ndani ya mhula mmoja Sasa amekuja Rais awamu ya 5 kahutubia Mara mbili tu na ukasisitiza et hiyo ni ishara kuwa mihimili hiyo miwili haina mahusiano mazuri kwà awamu hii, wakati hapo kabla niwewe ndio ulikuwa unatuaibisha kuwa Bunge halina maamuzi linatekeleza Yale yote yanayoamuliwa na Rais Mara Mhimili wa bunge upo chini ya Rais Sasa Mimi nikawa nahoji hivi Kama hiyo mihimili miwili haina mahusiano mazuri yaan haisikilizani iweje leo Sasa Rais aingilie majukumu ya Bunge na Bunge hilohilo unalolalamikia halina mahusiano mazuri na Rais litii maagizo Toka kwà Rais!!

Kimsingi hata hapo tulipofikia sio HABA tushukuru kwà hiki kidogo tulichonacho!!!
 
Nchi haina maendeleo na pato kwa mwananchi wa chini bado linahesabika kwenye Nchi masikini sana Duniani, misaada itakatwa kwani Tanzania imeonekaa ipo kwenye uchumi wa kati haihitaji msaada
Ukiwa akili ya kutegemea misaada kila kukichaa hutakaa uendelee..jitahidi sana kuishi kwa kujitegemea utasonga mbele zaid..achana na akili za kimaskini..kuishi kwa kutegemea mifuko ya watu..tegemea mfuko wako mkuu..
 
Zityo ni mpotoshaji, jalitakii mema taifa, anatumia karama yake vibaya, Hana tofauti na akina tiputipu.

Uzuri sikuhizi kuna order, amuulize lisi. Alipotosha akapewa dozi

Mtu mmoja akaathirika Kwa manufaa ya taifa
Halijaanza leo. Yesu alitundikwa msalabani baada ya farisayo maarufu kusema mtu mmoja lazima afe Kwa ajiri ya ukombozi wa taifa


Mawazo binafsi nikiwa nimetumia kileo.
 
Tatizo la Upinzani wa nchi hii huwa hakubali lolote kwao kila Kitu ni kukosoa tu!!

Zitto Kabwe ndio ulibaki mpinzani Pekee niliekukubali Sana Ila nilikuona mtu ambae huna jema siku ya kuvunjwa Bunge la TZ kwà mwaka 2015-2020, Ile siku unahojiwa ukadai et Rais wa awamu ya 3 na 4 walihutubia Bunge Mara 3 Hadi 4 ndani ya mhula mmoja Sasa amekuja Rais awamu ya 5 kahutubia Mara mbili tu na ukasisitiza et hiyo ni ishara kuwa mihimili hiyo miwili haina mahusiano mazuri kwà awamu hii, wakati hapo kabla niwewe ndio ulikuwa unatuaibisha kuwa Bunge halina maamuzi linatekeleza Yale yote yanayoamuliwa na Rais Mara Mhimili wa bunge upo chini ya Rais Sasa Mimi nikawa nahoji hivi Kama hiyo mihimili miwili haina mahusiano mazuri yaan haisikilizani iweje leo Sasa Rais aingilie majukumu ya Bunge na Bunge hilohilo unalolalamikia halina mahusiano mazuri na Rais litii maagizo Toka kwà Rais!!

Kimsingi hata hapo tulipofikia sio HABA tushukuru kwà hiki kidogo tulichonacho!!!
Acha ngonjera mkuu..jibu hoja za mhe.zitto..hv nyie watu wa ccm mkoje??
 
Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati? - Zitto Kabwe



Tangu jana nimeona shamrashamra kubwa kuhusu kinachoitwa mafanikio ya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Kati. Kuingia Uchumi wa Kati ni hatua nzuri lakini inayohitaji ufafanuzi wa kiuongozi. Hatua hii ikifanyiwa propaganda itaonekana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano wana uhaba wa mafanikio au hawajui wanachoshangilia. Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.



Benki ya Dunia inaitambua nchi kuwa ya Uchumi wa Kati pale ambapo Pato la Wastani la Wananchi wake lipo kati ya Dola za Marekani 1,090 hadi 12,235 kwa mwaka. Katika kundi hili kuna Uchumi wa kati wa chini kabisa, Uchumi wa kati wa chini, Uchumi wa kati kati na Uchumi wa kati wa Juu. Kwa kimombo zinaitwa Lower Middle Income, Low Middle Income, Middle Income, Upper Middle Income.

Hiki kinachoshangiliwa hapa kwetu ni ile hatua ya kwanza, yaani tupo Getini kabisa. Pato la Wastani la kila Mtanzania limevuka Dola za Marekani 1,090 ( taarifa pia zinaonyesha kuwa Benki ya Dunia imeshusha vigezo na hivyo kupanua Goli ).



Hichi kipimo kinachotumika ni nini ?



Pato la Wastani (income per capita) ni jumla ya Pato la Taifa (GDP) ukiligawa kwa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo aliyezaliwa leo.

Yaani unachukua mapato ya Watanzania matajiri kama kina Bakhresa, Rostam Aziz, Mohamed Dewji na kadhalika, pamoja na Mapato ya vijana waendesha bodaboda, wakulima wa nyanya Ilula-Iringa na watu wasio na kipato kabisa kisha ugawe kwa kila Mtanzania kwa sawa. Kinachopatikana ndio wastani wa Pato la kila Mtu.

Ni hesabu za nadharia tu. Ni muhimu sana kuelewa nadharia hii kwamba wastani wa Pato la mtu ni Hesabu tu ya kujumlisha na kugawanya lakini sio uhalisia wa Pato la Mtu.



Pato la Taifa la Tanzania kwa bei za mwaka 2019 lilikuwa shilingi Trilioni 139. Mwaka 2019, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na Watu Milioni 54 ambapo Pato la wastani la kila mtu lilifikia shilingi 2,577,967. Kiasi hicho cha pato la wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2019 ni sawa na dola za Marekani 1,096 hivyo kuwa tumevuka kiwango cha Benki ya Dunia cha kuwa na Uchumi wa Kati.



Mwaka 2015, Pato la wastani la Mtanzania lilikuwa limefikia wastani Dola za Marekani 1,060. Kwa hiyo tulikuwa tumepungukiwa Dola za Marekani 30 tu ili kufikia ‘Lower Middle Income’ ambayo ndio tumeifikia sasa. Imetuchukua miaka 5 kuongeza $30 kwa kila Mtanzania kama wastani wa Pato lao.

Kwa wastani kila Mwaka Serikali imeweza kuongeza wastani wa Dola 6 tu kwa Mwaka kwa kila Mtanzania, yaani shilingi 14,000 tu kwa fedha za kitanzania.



Hatujafikia Lengo



Maendeleo ya Tanzania yanaongozwa na Mpango wa Maendeleo ya Taifa. Lengo letu kwenye Mpango huo ni “Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati wa wastani wa Pato la mtu kufika Dola za Marekani 3,000 ifikapo 2025. Kuvuka mpaka na kufikia hatua tuliyofikia ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu.



Kama imetuchukua miaka 5 kuongeza Dola 30, itatuchukua miaka mingapi kuongeza Dola 2,100? Hii maana yake ili kufikia Wastani wa Pato la Mtanzania la Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka, katika miaka 5 ijayo, tunapaswa kuongeza pato letu maradufu. Bado tuna mwendo mrefu kufikia lengo letu la kuwa na Uchumi wa Kati.



Nimeshangaa sana kuona Kuwa Baadhi yetu wakiwemo viongozi wanatamka kuwa Tanzania imefikia lengo la uchumi wa Kati miaka 5 kabla ya muda uliopangwa. Sio kweli kwani lengo tulilojiwekea ni Dola za Marekani angalau 3,000 kama Pato la Wastani la kila Mtu kwa Mwaka. Kusema kuwa tumefikia lengo ni dalili kuwa tuna uhaba wa mafanikio, tena uhaba mkubwa. Lakini pia kuna hatari kubwa ya kutoka kwenye mstari wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa kujidanganya kuwa tayari tumefikia lengo.



Hata kama tungekuwa tumefikia lengo tulilojiwekea bado tunapaswa kupokea habari ya nyongeza ya wastani wa pato kwa kila mtu kwa tahadhari kubwa sana. Kuna faida na hasara ya kupanda daraja hili. Ukiwa ‘under developed low income country’, faida yake ni kupata misaada na mikopo yenye unafuu mkubwa. Ni sawa na mtoto mdogo anayepewa vyakula vya kupondwa pondwa. Hii inatoa ahueni kubwa kwa nchi kujijenga kiuchumi. Ukifaulu na kuingia kwenye kundi la uchumi wa kati hii mbeleko inaondoka. Sasa utapaswa kukopa mikopo ya kibiashara zaidi ambayo riba yake ni kubwa. Kwa lugha nyingine, mikopo inakuwa ghali na misaada inapungua sana. Yaani matarajio ni kuwa sasa umekuwa mkubwa ujitafunie. Mikopo ya Biashara ambayo tayari tumeanza kuchukua kiasi cha kuwa 34% ya Deni la Taifa. Benki ya Dunia imetoa mwanya wa Deni letu la Taifa kuwa kubwa na lenye gharama kubwa kulihudumia.



Faida ya kuwa uchumi wa kati ni kwamba ukomo wa Nchi wa kukopa katika masoko ya Fedha na mitaji inapanuka kuliko sasa. Hivyo unaweza kufanya mambo makubwa zaidi. Hasara yake ni gharama ya mikopo hiyo inaumiza uchumi ambapo mara nyingi sana unakuwa si imara sana kwa kuwa mara nyingi, uchumi huo hubebwa na takwimu tu ambazo zinaweza zisiakisi maisha halisi ya watu.



Mathalan, nchi zenye madini na mafuta, pato la Taifa linaweza kuonekana kubwa lakini vigezo vya hali ya maisha ya watu (Human Development Index) ikawa chini sana. Nchi nyingi za Low Middle Income zinalalamika sana kuomba zifikiriwe upya na mashirika ya kifedha. Baadhi ya Nchi zinaomba kwa Benki ya Dunia zishushwe daraja ili kukwepa hasara hizi. Sisi tunashangilia sana. Nadhani hatujui tunachoshangilia ni nini.



Kwa Nchi kama yetu ni muhimu sana Viongozi kuwa na uwezo mkubwa wa kutofautisha kati ya Uchumi wa Takwimu na Uchumi Halisi wa Wananchi. Uhalisia ni kuwa uchumi wa wananchi ni goi goi sana. Hali ya maisha ya wananchi imeanguka kutokana na kupungua kwa shughuli za uchumi za uzalishaji mali. Katika miaka 5 Serikali ya Awamu ya Tano imetumia Bajeti ya Shilingi Trilioni 162 sawa na wastani wa Dola za Marekani 1,173 ukizigawa kwa kila Mtanzania. Hata hivyo katika miaka hiyo 5 Pato la Mtanzania limeongezeka kwa Dola za Marekani 30 tu. Hii maana yake ni kuwa Matumizi yetu ya Bajeti hayaongezi shughuli za Uchumi za Wananchi wengi.



Kwa mfano, wakati tumetumia Shilingi 1.8 Trilioni kwenye matumizi ya kununua Ndege 11 zinazotumiwa na 5% ya Watanzania, katika miaka 5 tumetumia Shilingi Trilioni Moja tu kwenye matumizi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotegemewa na 67% ya Watanzania. Bajeti hii ya Kilimo ni 0.6% ya Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka 5.



Kutokana na Hali hiyo ya matumizi yasiyozingatia shughuli za uchumi za wananchi, taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania Economic Upadte number 11 ) inaonyesha kuwa jumla ya Watanzania 2.7 milioni wameingia kwenye dimbwi la umasikini Kati ya Mwaka 2017-2019. Unakuwaje Nchi ya Uchumi wa Kati wakati mamilioni ya Wananchi wanakuwa masikini kila mwaka ?



Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa kasi tuliyokuwa nayo kwa miaka 5 iliyopita inatia mashaka ikiwa tutafika lengo letu la Uchumi wa Kati miaka 5 ijayo iwapo tukiendelea na maono haya, fikra hizi na matendo haya. Kuvuka mpaka ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu. Mpango wa Taifa unatutaka tufikia Pato la Kila Mtu la walau Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka ifikapo 2025.



Kufikia lengo hili inakuja na wajibu mkubwa kwa kila mmoja wetu kama Taifa na tunahitaji Uongozi na maono mapya. Tunahitaji Wananchi wawe na Raha na Furaha, wakifanya Kazi kwa bidii na kufurahia matunda ya jasho lao ( #KaziNaBata ).



Lindi, Tanzania

3/7/2020
Only Great Thinkers 'll understand this article.

Praising team a.k.a utopolo 'll never understand this since their frontal lobes are shrunk and sunk.
 
Zityo ni mpotoshaji, jalitakii mema taifa, anatumia karama yake vibaya, Hana tofauti na akina tiputipu.

Uzuri sikuhizi kuna order, amuulize lisi. Alipotosha akapewa dozi

Mtu mmoja akaathirika Kwa manufaa ya taifa
Halijaanza leo. Yesu alitundikwa msalabani baada ya farisayo maarufu kusema mtu mmoja lazima afe Kwa ajiri ya ukombozi wa taifa


Mawazo binafsi nikiwa nimetumia kileo.
Amepotosha wapi?? Mbona unatuletea mipasho
 
Mm naamin tupo kweny Uchum w Kati sabab naona Wana JF n weng xn ckuiz hii n kumaanisha w2 wengi wna Milik xim janja na wana hela za Kununua MBs xo k2 ni kati qwel
 
Sasa unakuja kulialia huku jf si upande tu ndege Tena mpaka Kwenye ofisi za hao WB walioitangaza kuwa Imefika Uchumi wa Kati.

Sasa unatuumiza vichwa Sisi ambao hatukuhusika na kutangaza huo Uchumi..

Kama umeishiwa pesa ya karamu na karatasi ya kuandikia barua world bank + nauli ya ndege we anzisha tu Uzi wa kukuchangia uende Tena.

Msaliti mkubwa wewe utaendelea kuweweseka na maombi yako ya mabaya juu ya taifa hili kamwe hayatafua dafu.

Proud to be Tanzanian[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Mkuu pole sana!
 
Hawa ni wachumia tumbo Rais Magufuli ameziba rushwa na ufisadi waliozoea kuiba ndio maana wanapiga kelele
Tan

Tanzania hata ufanye nini kinaonekana kibaya tu sasa hawa watu ambao tunawaona ni wasomi mwingine anajua kuliko mwenyekiti wa Benki ya Dunia bwana Zito kabwe anatoa povu la kuwadanganya watanzania wasione kazi nzuri ya serikali. Kuna tofauti gani kati ya Kenya na Tanzania huko kenya wapo watu wanalala na njaa na kipato duni kama kwetu sasa mbona Kenya waliingizwa kwenye nchi za kipato cha kati tangu 2015 sijaona kuwabeza. Tungebaki kwenye LDC bado Zito angetoa povu zaidi. Kwa Tanzania ukichukua fedha za serikali ukaenda zako Marekani kutafuta mabibi na kuzitumbua basi wapo watu watakusifia sana na kukutolea mfano kwamba wewe ni kiongozi mzuri.
Vyovyote itakavyokuwa jua au mvua rais wetu ni JPM, tazama Mungu anavyomwekea mkono wake mpaka Tanzanite za kilo kumi zinapatikana chini ya utawala wake tulizoea kuona size ya kokoto tu.
 
Hujaeleweka hata kidogo, nchi nying xinahagaika kufikia hatua hii sijuw we w ni nani upinge hatua nzur kama hii
Ameelezea na kufafanua vizuri tu hata mtoto wa shule ya msingi anaelewa.
Wewe utakua umejaza mavi kichwani badala ya ubongo
 
Back
Top Bottom