dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,958
- 9,516
Ha haha haaa ahaaaKatika Nchi ambayo hata kupatwa Kwa mwezi watu wanaishukuru serikali..kuwaelimisha ni kupoteza muda
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha haha haaa ahaaaKatika Nchi ambayo hata kupatwa Kwa mwezi watu wanaishukuru serikali..kuwaelimisha ni kupoteza muda
Nbs sindio wapika takwimu ili kumfurahisha mteuzi?Asante kwa ufafanuzi
====
Mkuu naweza kupata utaratibu wa kitafiti uliotumiwa kupata takwimu hii ya 2.7 mil kuingia kwenye dimbwi la umaskini? Je. NBS yetu ilihusishwa kwenye utafiti huu?
Umeelewa alichoandika Zitto?Sasa unakuja kulialia huku jf si upande tu ndege Tena mpaka Kwenye ofisi za hao WB walioitangaza kuwa Imefika Uchumi wa Kati.
Sasa unatuumiza vichwa Sisi ambao hatukuhusika na kutangaza huo Uchumi..
Kama umeishiwa pesa ya karamu na karatasi ya kuandikia barua world bank + nauli ya ndege we anzisha tu Uzi wa kukuchangia uende Tena.
Msaliti mkubwa wewe utaendelea kuweweseka na maombi yako ya mabaya juu ya taifa hili kamwe hayatafua dafu.
Proud to be Tanzanian[emoji1241][emoji1241][emoji1241]
Muhimu ni wewe kukiri kwamba unapoenda kijijini ukirudi mjini zawadi ni kitu ambacho unatarajia, ina maana wenyeji hadi kufanya ivyo wamezalisha ziada.Nikishaona mtu anazungumzia maendeleo/uchumi kisha matarajio yake yakawa ni mtu nachafukwa kabisa. Haya maendeleo ya kutegemea mtu mmoja ndio yalitukwamisha wakati wa Nyerere. Tulikwenda vizuri sana mwanzo, lakini mwisho wake tukaishia kuvaa viraka na kugeuka masikini wa kutupwa.
Unasema kuwa huko vijijini kuwa ukienda unapewa zawadi kadhaa kama mahindi nk. Hilo ni kweli kabisa, lakini kwenye utoaji wao, wanatoa kwakuwa wametosheka au wako nje ya poverty circle? Ninachoona huwa wanatoa kwa sababu ya upendo, na mazoea yetu waafrika ya kumkirimu mgeni. Hayo masoko anayowapigania ni kama kilichotokea kwenye korosho?
Wakati wa Nyerere tulikwama, maana watu kama akina Zito wenye mitazamo mbadala walionekana maadui, na mawazo ya mtu mmoja tu yakawa ndio sahihi! Na ww hapa naona unaelekea kulekule kuwa Magufuli yuko sahihi, na michango ya kina Zito ndio inamkwamisha Magufuli ambaye unajua atakutoa ulipo kwa mawazo yake sahihi! Hapa naona unaoongozwa na mahaba niue zaidi. Nimecheka sana hapo paragraph ya mwisho, kuwa kwa sasa kila mtu anapaswa kuelewa Magufuli anatupeleka wapi!
😂😂😂😂🤣🤣😂Watanzania tunashukuru Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati ndani ya miaka mitano tu
Tukimpa muda zaidi tunaweza kuipiku USA
😂😂😂😂🤣🤣😂Watanzania tunashukuru Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati ndani ya miaka mitano tu
Tukimpa muda zaidi tunaweza kuipiku USA
Muhimu ni wewe kukiri kwamba unapoenda kijijini ukirudi mjini zawadi ni kitu ambacho unatarajia, ina maana wenyeji hadi kufanya ivyo wamezalisha ziada.
Ndio maana uchumi kama somo liko kwenye mpaka wa social science and hard science because human behaviour also dictates the economy.
Ndio ujue sasa hadi wewe kupewa chakula na bibi/shangazi ina maana wamezalisha vya kutosha now that value should be reflected as production lakini aipo kwenye statistics maana yake nini considering GDP is a measure of output na wewe unarudi mjini na debe ambalo alijaesabiwa kwenye gharama za uzalishaji wanachosema mabeberu aki reflect Tanzania.
Nenda Kenya, Rwanda au Burundi uone kama ndugu watakurudisha na debe au gunia la mahindi; wayatoe wapi wakati ardhi ya kulimia ziada awana. That makes land an injection into the economy ni kiasi ganj serikali yetu inagawa kila mwaka?
Asubuhi njema kwako me out; muhimu kukumbuka we are not a poor nation Magu is right sisi ni nchi tajiri tuwakwepe matapeli kama akina Zitto wenye nadharia potofu za kukariri na kutaka kupotosha sisi nchi maskini
UNASHEREHEKEA NINI?Tatizo liko wapi wananchi "kusherehekea"? Nimesoma uzi ndio...
Huna Raha peke yako! Sisi watz tunashangilia! Etu Raha, hivi Raha ni Nini hasa!? Agenda kwa kweli kabisa mmeishiwa!Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?
Tangu jana nimeona shamrashamra kubwa kuhusu kinachoitwa mafanikio ya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Kati. Kuingia Uchumi wa Kati ni hatua nzuri lakini inayohitaji ufafanuzi wa kiuongozi. Hatua hii ikifanyiwa propaganda itaonekana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano wana uhaba wa mafanikio au hawajui wanachoshangilia. Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.
Benki ya Dunia inaitambua nchi kuwa ya Uchumi wa Kati pale ambapo Pato la Wastani la Wananchi wake lipo kati ya Dola za Marekani 1,090 hadi 12,235 kwa mwaka. Katika kundi hili kuna Uchumi wa kati wa chini kabisa, Uchumi wa kati wa chini, Uchumi wa kati kati na Uchumi wa kati wa Juu. Kwa kimombo zinaitwa Lower Middle Income, Low Middle Income, Middle Income, Upper Middle Income.
Hiki kinachoshangiliwa hapa kwetu ni ile hatua ya kwanza, yaani tupo Getini kabisa. Pato la Wastani la kila Mtanzania limevuka Dola za Marekani 1,090 ( taarifa pia zinaonyesha kuwa Benki ya Dunia imeshusha vigezo na hivyo kupanua Goli ).
Hichi kipimo kinachotumika ni nini?
Pato la Wastani (income per capita) ni jumla ya Pato la Taifa (GDP) ukiligawa kwa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo aliyezaliwa leo.
Yaani unachukua mapato ya Watanzania matajiri kama kina Bakhresa, Rostam Aziz, Mohamed Dewji na kadhalika, pamoja na Mapato ya vijana waendesha bodaboda, wakulima wa nyanya Ilula-Iringa na watu wasio na kipato kabisa kisha ugawe kwa kila Mtanzania kwa sawa. Kinachopatikana ndio wastani wa Pato la kila Mtu.
Ni hesabu za nadharia tu. Ni muhimu sana kuelewa nadharia hii kwamba wastani wa Pato la mtu ni Hesabu tu ya kujumlisha na kugawanya lakini sio uhalisia wa Pato la Mtu.
Pato la Taifa la Tanzania kwa bei za mwaka 2019 lilikuwa shilingi Trilioni 139. Mwaka 2019, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na Watu Milioni 54 ambapo Pato la wastani la kila mtu lilifikia shilingi 2,577,967. Kiasi hicho cha pato la wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2019 ni sawa na dola za Marekani 1,096 hivyo kuwa tumevuka kiwango cha Benki ya Dunia cha kuwa na Uchumi wa Kati.
Mwaka 2015, Pato la wastani la Mtanzania lilikuwa limefikia wastani Dola za Marekani 1,060. Kwa hiyo tulikuwa tumepungukiwa Dola za Marekani 30 tu ili kufikia ‘Lower Middle Income’ ambayo ndio tumeifikia sasa. Imetuchukua miaka 5 kuongeza $30 kwa kila Mtanzania kama wastani wa Pato lao.
Kwa wastani kila Mwaka Serikali imeweza kuongeza wastani wa Dola 6 tu kwa Mwaka kwa kila Mtanzania, yaani shilingi 14,000 tu kwa fedha za kitanzania.
Hatujafikia Lengo
Maendeleo ya Tanzania yanaongozwa na Mpango wa Maendeleo ya Taifa. Lengo letu kwenye Mpango huo ni “Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati wa wastani wa Pato la mtu kufika Dola za Marekani 3,000 ifikapo 2025. Kuvuka mpaka na kufikia hatua tuliyofikia ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu.
Kama imetuchukua miaka 5 kuongeza Dola 30, itatuchukua miaka mingapi kuongeza Dola 2,100? Hii maana yake ili kufikia Wastani wa Pato la Mtanzania la Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka, katika miaka 5 ijayo, tunapaswa kuongeza pato letu maradufu. Bado tuna mwendo mrefu kufikia lengo letu la kuwa na Uchumi wa Kati.
Nimeshangaa sana kuona Kuwa Baadhi yetu wakiwemo viongozi wanatamka kuwa Tanzania imefikia lengo la uchumi wa Kati miaka 5 kabla ya muda uliopangwa. Sio kweli kwani lengo tulilojiwekea ni Dola za Marekani angalau 3,000 kama Pato la Wastani la kila Mtu kwa Mwaka. Kusema kuwa tumefikia lengo ni dalili kuwa tuna uhaba wa mafanikio, tena uhaba mkubwa. Lakini pia kuna hatari kubwa ya kutoka kwenye mstari wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa kujidanganya kuwa tayari tumefikia lengo.
Hata kama tungekuwa tumefikia lengo tulilojiwekea bado tunapaswa kupokea habari ya nyongeza ya wastani wa pato kwa kila mtu kwa tahadhari kubwa sana. Kuna faida na hasara ya kupanda daraja hili. Ukiwa ‘under developed low income country’, faida yake ni kupata misaada na mikopo yenye unafuu mkubwa. Ni sawa na mtoto mdogo anayepewa vyakula vya kupondwa pondwa. Hii inatoa ahueni kubwa kwa nchi kujijenga kiuchumi. Ukifaulu na kuingia kwenye kundi la uchumi wa kati hii mbeleko inaondoka. Sasa utapaswa kukopa mikopo ya kibiashara zaidi ambayo riba yake ni kubwa. Kwa lugha nyingine, mikopo inakuwa ghali na misaada inapungua sana. Yaani matarajio ni kuwa sasa umekuwa mkubwa ujitafunie. Mikopo ya Biashara ambayo tayari tumeanza kuchukua kiasi cha kuwa 34% ya Deni la Taifa. Benki ya Dunia imetoa mwanya wa Deni letu la Taifa kuwa kubwa na lenye gharama kubwa kulihudumia.
Faida ya kuwa uchumi wa kati ni kwamba ukomo wa Nchi wa kukopa katika masoko ya Fedha na mitaji inapanuka kuliko sasa. Hivyo unaweza kufanya mambo makubwa zaidi. Hasara yake ni gharama ya mikopo hiyo inaumiza uchumi ambapo mara nyingi sana unakuwa si imara sana kwa kuwa mara nyingi, uchumi huo hubebwa na takwimu tu ambazo zinaweza zisiakisi maisha halisi ya watu.
Mathalan, nchi zenye madini na mafuta, pato la Taifa linaweza kuonekana kubwa lakini vigezo vya hali ya maisha ya watu (Human Development Index) ikawa chini sana. Nchi nyingi za Low Middle Income zinalalamika sana kuomba zifikiriwe upya na mashirika ya kifedha. Baadhi ya Nchi zinaomba kwa Benki ya Dunia zishushwe daraja ili kukwepa hasara hizi. Sisi tunashangilia sana. Nadhani hatujui tunachoshangilia ni nini.
Kwa Nchi kama yetu ni muhimu sana Viongozi kuwa na uwezo mkubwa wa kutofautisha kati ya Uchumi wa Takwimu na Uchumi Halisi wa Wananchi. Uhalisia ni kuwa uchumi wa wananchi ni goi goi sana. Hali ya maisha ya wananchi imeanguka kutokana na kupungua kwa shughuli za uchumi za uzalishaji mali. Katika miaka 5 Serikali ya Awamu ya Tano imetumia Bajeti ya Shilingi Trilioni 162 sawa na wastani wa Dola za Marekani 1,173 ukizigawa kwa kila Mtanzania. Hata hivyo katika miaka hiyo 5 Pato la Mtanzania limeongezeka kwa Dola za Marekani 30 tu. Hii maana yake ni kuwa Matumizi yetu ya Bajeti hayaongezi shughuli za Uchumi za Wananchi wengi.
Kwa mfano, wakati tumetumia Shilingi 1.8 Trilioni kwenye matumizi ya kununua Ndege 11 zinazotumiwa na 5% ya Watanzania, katika miaka 5 tumetumia Shilingi Trilioni Moja tu kwenye matumizi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotegemewa na 67% ya Watanzania. Bajeti hii ya Kilimo ni 0.6% ya Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka 5.
Kutokana na Hali hiyo ya matumizi yasiyozingatia shughuli za uchumi za wananchi, taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania Economic Upadte number 11 ) inaonyesha kuwa jumla ya Watanzania 2.7 milioni wameingia kwenye dimbwi la umasikini Kati ya Mwaka 2017-2019. Unakuwaje Nchi ya Uchumi wa Kati wakati mamilioni ya Wananchi wanakuwa masikini kila mwaka ?
Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa kasi tuliyokuwa nayo kwa miaka 5 iliyopita inatia mashaka ikiwa tutafika lengo letu la Uchumi wa Kati miaka 5 ijayo iwapo tukiendelea na maono haya, fikra hizi na matendo haya. Kuvuka mpaka ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu. Mpango wa Taifa unatutaka tufikia Pato la Kila Mtu la walau Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka ifikapo 2025.
Kufikia lengo hili inakuja na wajibu mkubwa kwa kila mmoja wetu kama Taifa na tunahitaji Uongozi na maono mapya. Tunahitaji Wananchi wawe na Raha na Furaha, wakifanya Kazi kwa bidii na kufurahia matunda ya jasho lao ( #KaziNaBata ).
Lindi, Tanzania
3/7/2020
Kwani Kuna ubaya ukisheherekea jirani kununua bajaji hata Kama hauna? Usiku ukizidiwa so angalau unaweza pata msaada kwa kupitia bajaji ya jirani badala ya kuhangaika kutafuta mbali!? Hebu toeni chuki zenu za kipuuzi dhidi ya jembe letu Magu na mafanikio tunayopata kwa kupitia yy! Kama vipi jitundikeni nyambafu!UNASHEREHEKEA NINI?
WAKATI WEWE HUMILIKI HATA KIBAJAJI?
You are missing the point hiyo hela unayoacha kijijini ipo kwenye uchumi rasmi umeipata either kama sehemu ya mshahara au biashara ambayo TRA keshapitia ni sehemu ya outflow and inflow kwenye circular flow ya GDP.Mkuu unachekesha ile mbaya, unaenda kijijini unatoa sio chini ya 50,000, hapo umejibana ile mbaya. Halafu unapewa debe 2 za mahindi ambazo ni chini ya 20,000, achia mbali kubeba ,na ukija hapa mjini hujui hata mashine ya kwenda kusaga. Kama sio wendawazimu ni nini?
Kwa mitazamo yako hii ya mahaba niue, lazima mitazamo mbadala kama ya kina Zito uikatae.
Inawezekana WB na mataifa makubwa yenye michango mikubwa kwenye bank hiyo, wameamua kuanza na hili la kutupandisha ili kutukomoa.Nchi haina maendeleo na pato kwa mwananchi wa chini bado linahesabika kwenye Nchi masikini sana Duniani, misaada itakatwa kwani Tanzania imeonekaa ipo kwenye uchumi wa kati haihitaji msaada
Wakati huku chini tunalia kilio cha mbwa meno juu!Mkuu ni kweli pesa imeongezeka thamani Kwasababu Rais Magufuli amefuta rushwa, amefuta ufisadi, amekomesha madawa ya kulevy, amekomesha majangili na majizi
Kama ulikuwepo kwenye hiyo cheni lazima pesa ikupige chenga uone maisha magumu
Makundi mengine yanafurahia maisha Kwasababu hawajaathiriwa na kitu chochote, ukizingatia Rais Magufuli anawatetea sana watu wa kipato cha chini
Layman anawezaje kuelewa elimu kubwa?Sasa unakuja kulialia huku jf si upande tu ndege Tena mpaka Kwenye ofisi za hao WB walioitangaza kuwa Imefika Uchumi wa Kati.
Sasa unatuumiza vichwa Sisi ambao hatukuhusika na kutangaza huo Uchumi..
Kama umeishiwa pesa ya karamu na karatasi ya kuandikia barua world bank + nauli ya ndege we anzisha tu Uzi wa kukuchangia uende Tena.
Msaliti mkubwa wewe utaendelea kuweweseka na maombi yako ya mabaya juu ya taifa hili kamwe hayatafua dafu.
Proud to be Tanzanian[emoji1241][emoji1241][emoji1241]