Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.
Hili ndilo mnalotakiwa kuwafafanulia wananchi walielewe pasipo shaka.

Propaganda za awamu ya tano ziko wazi hazijifichi na Mweyewe hafichi kwamba mafanikio haya yote ni juhudi zake, na asipochaguliwa tena haya yote yatapotea. Si anayasema haya, kwani anaficha?

Na unashangaa watu na akili zao wanaamini.
 
Zitto wewe ni mbabaishaji tuu, yaani hua sikuelewi upo katika kingdom ipi, animalia, plantaé au N'dudu tuu wewe...
 
Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati? - Zitto Kabwe

Tangu jana nimeona shamrashamra kubwa kuhusu kinachoitwa mafanikio ya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Kati. Kuingia Uchumi wa Kati ni hatua nzuri lakini inayohitaji ufafanuzi wa kiuongozi. Hatua hii ikifanyiwa propaganda itaonekana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano wana uhaba wa mafanikio au hawajui wanachoshangilia. Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.

Benki ya Dunia inaitambua nchi kuwa ya Uchumi wa Kati pale ambapo Pato la Wastani la Wananchi wake lipo kati ya Dola za Marekani 1,090 hadi 12,235 kwa mwaka. Katika kundi hili kuna Uchumi wa kati wa chini kabisa, Uchumi wa kati wa chini, Uchumi wa kati kati na Uchumi wa kati wa Juu. Kwa kimombo zinaitwa Lower Middle Income, Low Middle Income, Middle Income, Upper Middle Income.

Hiki kinachoshangiliwa hapa kwetu ni ile hatua ya kwanza, yaani tupo Getini kabisa. Pato la Wastani la kila Mtanzania limevuka Dola za Marekani 1,090 ( taarifa pia zinaonyesha kuwa Benki ya Dunia imeshusha vigezo na hivyo kupanua Goli ).

Hichi kipimo kinachotumika ni nini ?

Pato la Wastani (income per capita) ni jumla ya Pato la Taifa (GDP) ukiligawa kwa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo aliyezaliwa leo.

Yaani unachukua mapato ya Watanzania matajiri kama kina Bakhresa, Rostam Aziz, Mohamed Dewji na kadhalika, pamoja na Mapato ya vijana waendesha bodaboda, wakulima wa nyanya Ilula-Iringa na watu wasio na kipato kabisa kisha ugawe kwa kila Mtanzania kwa sawa. Kinachopatikana ndio wastani wa Pato la kila Mtu.

Ni hesabu za nadharia tu. Ni muhimu sana kuelewa nadharia hii kwamba wastani wa Pato la mtu ni Hesabu tu ya kujumlisha na kugawanya lakini sio uhalisia wa Pato la Mtu.

Pato la Taifa la Tanzania kwa bei za mwaka 2019 lilikuwa shilingi Trilioni 139. Mwaka 2019, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na Watu Milioni 54 ambapo Pato la wastani la kila mtu lilifikia shilingi 2,577,967. Kiasi hicho cha pato la wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2019 ni sawa na dola za Marekani 1,096 hivyo kuwa tumevuka kiwango cha Benki ya Dunia cha kuwa na Uchumi wa Kati.

Mwaka 2015, Pato la wastani la Mtanzania lilikuwa limefikia wastani Dola za Marekani 1,060. Kwa hiyo tulikuwa tumepungukiwa Dola za Marekani 30 tu ili kufikia ‘Lower Middle Income’ ambayo ndio tumeifikia sasa. Imetuchukua miaka 5 kuongeza $30 kwa kila Mtanzania kama wastani wa Pato lao.

Kwa wastani kila Mwaka Serikali imeweza kuongeza wastani wa Dola 6 tu kwa Mwaka kwa kila Mtanzania, yaani shilingi 14,000 tu kwa fedha za kitanzania.

Hatujafikia Lengo

Maendeleo ya Tanzania yanaongozwa na Mpango wa Maendeleo ya Taifa. Lengo letu kwenye Mpango huo ni “Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati wa wastani wa Pato la mtu kufika Dola za Marekani 3,000 ifikapo 2025. Kuvuka mpaka na kufikia hatua tuliyofikia ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu.

Kama imetuchukua miaka 5 kuongeza Dola 30, itatuchukua miaka mingapi kuongeza Dola 2,100? Hii maana yake ili kufikia Wastani wa Pato la Mtanzania la Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka, katika miaka 5 ijayo, tunapaswa kuongeza pato letu maradufu. Bado tuna mwendo mrefu kufikia lengo letu la kuwa na Uchumi wa Kati.

Nimeshangaa sana kuona Kuwa Baadhi yetu wakiwemo viongozi wanatamka kuwa Tanzania imefikia lengo la uchumi wa Kati miaka 5 kabla ya muda uliopangwa. Sio kweli kwani lengo tulilojiwekea ni Dola za Marekani angalau 3,000 kama Pato la Wastani la kila Mtu kwa Mwaka. Kusema kuwa tumefikia lengo ni dalili kuwa tuna uhaba wa mafanikio, tena uhaba mkubwa. Lakini pia kuna hatari kubwa ya kutoka kwenye mstari wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa kujidanganya kuwa tayari tumefikia lengo.

Hata kama tungekuwa tumefikia lengo tulilojiwekea bado tunapaswa kupokea habari ya nyongeza ya wastani wa pato kwa kila mtu kwa tahadhari kubwa sana. Kuna faida na hasara ya kupanda daraja hili. Ukiwa ‘under developed low income country’, faida yake ni kupata misaada na mikopo yenye unafuu mkubwa. Ni sawa na mtoto mdogo anayepewa vyakula vya kupondwa pondwa. Hii inatoa ahueni kubwa kwa nchi kujijenga kiuchumi. Ukifaulu na kuingia kwenye kundi la uchumi wa kati hii mbeleko inaondoka. Sasa utapaswa kukopa mikopo ya kibiashara zaidi ambayo riba yake ni kubwa. Kwa lugha nyingine, mikopo inakuwa ghali na misaada inapungua sana. Yaani matarajio ni kuwa sasa umekuwa mkubwa ujitafunie. Mikopo ya Biashara ambayo tayari tumeanza kuchukua kiasi cha kuwa 34% ya Deni la Taifa. Benki ya Dunia imetoa mwanya wa Deni letu la Taifa kuwa kubwa na lenye gharama kubwa kulihudumia.

Faida ya kuwa uchumi wa kati ni kwamba ukomo wa Nchi wa kukopa katika masoko ya Fedha na mitaji inapanuka kuliko sasa. Hivyo unaweza kufanya mambo makubwa zaidi. Hasara yake ni gharama ya mikopo hiyo inaumiza uchumi ambapo mara nyingi sana unakuwa si imara sana kwa kuwa mara nyingi, uchumi huo hubebwa na takwimu tu ambazo zinaweza zisiakisi maisha halisi ya watu.

Mathalan, nchi zenye madini na mafuta, pato la Taifa linaweza kuonekana kubwa lakini vigezo vya hali ya maisha ya watu (Human Development Index) ikawa chini sana. Nchi nyingi za Low Middle Income zinalalamika sana kuomba zifikiriwe upya na mashirika ya kifedha. Baadhi ya Nchi zinaomba kwa Benki ya Dunia zishushwe daraja ili kukwepa hasara hizi. Sisi tunashangilia sana. Nadhani hatujui tunachoshangilia ni nini.

Kwa Nchi kama yetu ni muhimu sana Viongozi kuwa na uwezo mkubwa wa kutofautisha kati ya Uchumi wa Takwimu na Uchumi Halisi wa Wananchi. Uhalisia ni kuwa uchumi wa wananchi ni goi goi sana. Hali ya maisha ya wananchi imeanguka kutokana na kupungua kwa shughuli za uchumi za uzalishaji mali. Katika miaka 5 Serikali ya Awamu ya Tano imetumia Bajeti ya Shilingi Trilioni 162 sawa na wastani wa Dola za Marekani 1,173 ukizigawa kwa kila Mtanzania. Hata hivyo katika miaka hiyo 5 Pato la Mtanzania limeongezeka kwa Dola za Marekani 30 tu. Hii maana yake ni kuwa Matumizi yetu ya Bajeti hayaongezi shughuli za Uchumi za Wananchi wengi.

Kwa mfano, wakati tumetumia Shilingi 1.8 Trilioni kwenye matumizi ya kununua Ndege 11 zinazotumiwa na 5% ya Watanzania, katika miaka 5 tumetumia Shilingi Trilioni Moja tu kwenye matumizi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotegemewa na 67% ya Watanzania. Bajeti hii ya Kilimo ni 0.6% ya Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka 5.

Kutokana na Hali hiyo ya matumizi yasiyozingatia shughuli za uchumi za wananchi, taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania Economic Upadte number 11 ) inaonyesha kuwa jumla ya Watanzania 2.7 milioni wameingia kwenye dimbwi la umasikini Kati ya Mwaka 2017-2019. Unakuwaje Nchi ya Uchumi wa Kati wakati mamilioni ya Wananchi wanakuwa masikini kila mwaka ?

Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa kasi tuliyokuwa nayo kwa miaka 5 iliyopita inatia mashaka ikiwa tutafika lengo letu la Uchumi wa Kati miaka 5 ijayo iwapo tukiendelea na maono haya, fikra hizi na matendo haya. Kuvuka mpaka ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu. Mpango wa Taifa unatutaka tufikia Pato la Kila Mtu la walau Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka ifikapo 2025.

Kufikia lengo hili inakuja na wajibu mkubwa kwa kila mmoja wetu kama Taifa na tunahitaji Uongozi na maono mapya. Tunahitaji Wananchi wawe na Raha na Furaha, wakifanya Kazi kwa bidii na kufurahia matunda ya jasho lao ( #KaziNaBata ).

Lindi, Tanzania

3/7/2020
Kwanza kabisa, ni vyema kufahamu kwamba kulingana na tarakimu zilizo tolewa na benki ya dunia, nchi ya uchumi wa kati inatakiwa kuwa na Gross national index per capita (GNI per capita) ya dola za Ki Marekani 1,036-12,535. Ambapo 1,036-4,045 ni lower middle income na 4,046-12,535 ni upper middle income. Kwa mujibu wa ripoti ya benki ya dunia, tarehe moja mwezi wa saba mwaka 2020, Tanzania ina GNI per Capita ya dola za Ki Marekani 1,080.

GNI ni tofauti kidogo na GDP (Gross Domestic product), vile vile per capita income ni tofauti kidogo na GNI per capita ila benki ya dunia inatumia GNI per capita ku orodhesha nchi katika vigezo hivyo kama nchi ya kipato cha chini, Kipato cha kati, na kipato cha juu. GDP ni kipato cha nchi kwa mwaka, GNI ni kipato cha nchi kwa mwaka uki jumlisha na vipato kutoka nchi zingine (yaani GDP kwa mwaka + Vipato kutoka nchi zingine kwa mwaka). Per capita income ni GDP kwa mwaka iki gawanywa kwa idadi ya watu kwenye nchi. Hii inasaidia kufahamu kwamba kama unge amua kugawanya kipato cha nchi kwa kila mtanzania, kila mtu ange pata shilingi ngapi. Vile vile GNI per capita ni GDP kwa mwaka + Kipato kutoka nchi zingine kwa mwaka uki gawia idadi ya watu kwenye nchi. GDP sio kiashiria kizuri cha ukuaji wa uchumi wa nchi lakini per capita na GNI per capita ni tarakimu zinazo weza kuku eleza zaidi kuhusu hali ya nchi. Kwa mfano tuki angalia GDP ya nchi kama Nigeria, utagundua kuwa inaweza kuwa kubwa kuliko nchi karibia zote za Afrika lakini kulingana na population yao, per capita income sio kubwa sana. Viwango vya GNI per capita vya kila kundi la nchi (low income, middle income na high income) vina badilika kila mwaka kwasababu ya inflation, exchange rate na vitu vingine. Benki ya dunia huwa ina ripoti mabadiliko hayo kila mwaka.

New World Bank country classifications by income level: 2020-2021
New country classifications by income level: 2019-2020

Uki angalia link nilizo weka hapo juu kitu cha kwanza utakacho gundua ni kwamba ili kuingia kwenye nchi ya uchumi wa kati GNI per capita ime badilika kila mwaka. 2018-$996, 2019-$1,026, 2020-$1,036, kwa hiyo imepanda kila mwaka kwa sababu nilizo orodhesha hapo juu kwa hiyo hawaja tanua wigo. GNI per capita ya Tanzania mwaka 2020 ni 1,080. Haijawahi kufika 1,096 kama ulivyo andika na Tanzania haijawahi kutangazwa kuwa nchi ya uchumi wa kati. Vile vile GNI per capita ya Tanzania mwaka 2015 ilikuwa Dola za ki Marekani 948. Ina maanisha ongezeko ndani ya miaka mitano ni kutoka 948 mpaka 1,080. Nina kubaliana na wewe unaposema kwamba ni too ambitious kufikia GNI per capita ya $3000 mwaka 2025 na inahitaji nguvu za ziada kuvuka daraja na ku orodheshwa kama upper middle income country. Ni vyema ku fahamu pia kwamba tarakimu hizo zinaweza zisikupe picha halishi kwasababu ni wastani ya watu wote waliopo Tanzania. GNI per capita ya $1,080 ina maanisha kwamba kila mtanzania anatakiwa kuwa na kipato hicho kwa mwaka. Hio sio uhalisia. Jambo lingine la kutambua ni kazi kubwa ambayo lazima ifanyike ilikufikia malengo ya kuongeza GNI per capita. Kwa mfano, GNI per capita ya Tanzania mwaka 2015 ilikuwa $948 na 2020 ni $1,080. Hii ina maanisha kwamba katika miaka mitano kumekuwa na ongezeko la $132 kwa kila mtu ambayo ni sawa sawa na $132* watu 54,000,000. Ongezeko la kipato cha serikali kwa 7,128,000,000 ndani ya miaka mitano sio mchezo, hata kama fedha hizo zinaweza zisiwe mikononi mwa wananchi.

Tanzania, Benin, Mauritius move up World Bank income rankings | Africanews
Tanzania GDP Per Capita 1988-2020

Kuwa nchi ya uchumi wa kati kunaweza ku maanisha ongezeko la riba kwenye mikopo lakini hivyo ndio vitu ambavyo tuna paswa kufikiri kuachana navyo.

Human development index(HDI) inahusisha vitu vitatu - life expectancy, elimu na GNI per capita. Nchi inayo pata score nzuri ya HDI inatakiwa kuwa na viashiria vizuri vya life expectancy, literacy rate na GNI per capita. HDI yenyewe inaweza isikupe picha halisi ya maendeleo na hali ya nchi.

Naku baliana na wewe unaposema kwamba kidogo kumekuwa na misplaced priorities kwenye serikali ya awamu ya tano lakini ni vyema kutambua kwamba hata kufikia hatua tuliyo fika lazima kazi nzito imefanyika. Tuji vunie kuwa nchi ya uchumi wa kati, tu sherehekee, mambo mazuri zaidi yana kuja.
 
Watanzania tunashukuru Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati ndani ya miaka mitano tu

Tukimpa muda zaidi tunaweza kuipiku USA
naona ushatimiza wajibu wako wa kuwa wa kwaanza kbs kumsifu yesu wa Kangi Lugola...hongera!.
 
aise nimegain kitu! thx much bro!
umeona eeh...na watawala wetu ni ama nao hawaelewi kitu juu ya dhana nzima ya uchumi wa kati au wanapiga propaganda kuwaaminisha wananchi wasiodadisi kupata ukweli kujua kipi ni kipi.
 
Inategemea ni maendeleo gani kwa hiyo hela? Kwa tafsiri finyu ya maendeleo ndiyo hiyo uliyoitaja

Ukishakuwa na fedha ni lazima utakuwa na maendeleo, utamzidi nani na nani, that is another case.
 
Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati? - Zitto Kabwe

Tangu jana nimeona shamrashamra kubwa kuhusu kinachoitwa mafanikio ya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Kati. Kuingia Uchumi wa Kati ni hatua nzuri lakini inayohitaji ufafanuzi wa kiuongozi. Hatua hii ikifanyiwa propaganda itaonekana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano wana uhaba wa mafanikio au hawajui wanachoshangilia. Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.

Benki ya Dunia inaitambua nchi kuwa ya Uchumi wa Kati pale ambapo Pato la Wastani la Wananchi wake lipo kati ya Dola za Marekani 1,090 hadi 12,235 kwa mwaka. Katika kundi hili kuna Uchumi wa kati wa chini kabisa, Uchumi wa kati wa chini, Uchumi wa kati kati na Uchumi wa kati wa Juu. Kwa kimombo zinaitwa Lower Middle Income, Low Middle Income, Middle Income, Upper Middle Income.

Hiki kinachoshangiliwa hapa kwetu ni ile hatua ya kwanza, yaani tupo Getini kabisa. Pato la Wastani la kila Mtanzania limevuka Dola za Marekani 1,090 ( taarifa pia zinaonyesha kuwa Benki ya Dunia imeshusha vigezo na hivyo kupanua Goli ).

Hichi kipimo kinachotumika ni nini ?

Pato la Wastani (income per capita) ni jumla ya Pato la Taifa (GDP) ukiligawa kwa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo aliyezaliwa leo.

Yaani unachukua mapato ya Watanzania matajiri kama kina Bakhresa, Rostam Aziz, Mohamed Dewji na kadhalika, pamoja na Mapato ya vijana waendesha bodaboda, wakulima wa nyanya Ilula-Iringa na watu wasio na kipato kabisa kisha ugawe kwa kila Mtanzania kwa sawa. Kinachopatikana ndio wastani wa Pato la kila Mtu.

Ni hesabu za nadharia tu. Ni muhimu sana kuelewa nadharia hii kwamba wastani wa Pato la mtu ni Hesabu tu ya kujumlisha na kugawanya lakini sio uhalisia wa Pato la Mtu.

Pato la Taifa la Tanzania kwa bei za mwaka 2019 lilikuwa shilingi Trilioni 139. Mwaka 2019, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na Watu Milioni 54 ambapo Pato la wastani la kila mtu lilifikia shilingi 2,577,967. Kiasi hicho cha pato la wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2019 ni sawa na dola za Marekani 1,096 hivyo kuwa tumevuka kiwango cha Benki ya Dunia cha kuwa na Uchumi wa Kati.

Mwaka 2015, Pato la wastani la Mtanzania lilikuwa limefikia wastani Dola za Marekani 1,060. Kwa hiyo tulikuwa tumepungukiwa Dola za Marekani 30 tu ili kufikia ‘Lower Middle Income’ ambayo ndio tumeifikia sasa. Imetuchukua miaka 5 kuongeza $30 kwa kila Mtanzania kama wastani wa Pato lao.

Kwa wastani kila Mwaka Serikali imeweza kuongeza wastani wa Dola 6 tu kwa Mwaka kwa kila Mtanzania, yaani shilingi 14,000 tu kwa fedha za kitanzania.

Hatujafikia Lengo

Maendeleo ya Tanzania yanaongozwa na Mpango wa Maendeleo ya Taifa. Lengo letu kwenye Mpango huo ni “Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati wa wastani wa Pato la mtu kufika Dola za Marekani 3,000 ifikapo 2025. Kuvuka mpaka na kufikia hatua tuliyofikia ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu.

Kama imetuchukua miaka 5 kuongeza Dola 30, itatuchukua miaka mingapi kuongeza Dola 2,100? Hii maana yake ili kufikia Wastani wa Pato la Mtanzania la Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka, katika miaka 5 ijayo, tunapaswa kuongeza pato letu maradufu. Bado tuna mwendo mrefu kufikia lengo letu la kuwa na Uchumi wa Kati.

Nimeshangaa sana kuona Kuwa Baadhi yetu wakiwemo viongozi wanatamka kuwa Tanzania imefikia lengo la uchumi wa Kati miaka 5 kabla ya muda uliopangwa. Sio kweli kwani lengo tulilojiwekea ni Dola za Marekani angalau 3,000 kama Pato la Wastani la kila Mtu kwa Mwaka. Kusema kuwa tumefikia lengo ni dalili kuwa tuna uhaba wa mafanikio, tena uhaba mkubwa. Lakini pia kuna hatari kubwa ya kutoka kwenye mstari wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa kujidanganya kuwa tayari tumefikia lengo.

Hata kama tungekuwa tumefikia lengo tulilojiwekea bado tunapaswa kupokea habari ya nyongeza ya wastani wa pato kwa kila mtu kwa tahadhari kubwa sana. Kuna faida na hasara ya kupanda daraja hili. Ukiwa ‘under developed low income country’, faida yake ni kupata misaada na mikopo yenye unafuu mkubwa. Ni sawa na mtoto mdogo anayepewa vyakula vya kupondwa pondwa. Hii inatoa ahueni kubwa kwa nchi kujijenga kiuchumi. Ukifaulu na kuingia kwenye kundi la uchumi wa kati hii mbeleko inaondoka. Sasa utapaswa kukopa mikopo ya kibiashara zaidi ambayo riba yake ni kubwa. Kwa lugha nyingine, mikopo inakuwa ghali na misaada inapungua sana. Yaani matarajio ni kuwa sasa umekuwa mkubwa ujitafunie. Mikopo ya Biashara ambayo tayari tumeanza kuchukua kiasi cha kuwa 34% ya Deni la Taifa. Benki ya Dunia imetoa mwanya wa Deni letu la Taifa kuwa kubwa na lenye gharama kubwa kulihudumia.

Faida ya kuwa uchumi wa kati ni kwamba ukomo wa Nchi wa kukopa katika masoko ya Fedha na mitaji inapanuka kuliko sasa. Hivyo unaweza kufanya mambo makubwa zaidi. Hasara yake ni gharama ya mikopo hiyo inaumiza uchumi ambapo mara nyingi sana unakuwa si imara sana kwa kuwa mara nyingi, uchumi huo hubebwa na takwimu tu ambazo zinaweza zisiakisi maisha halisi ya watu.

Mathalan, nchi zenye madini na mafuta, pato la Taifa linaweza kuonekana kubwa lakini vigezo vya hali ya maisha ya watu (Human Development Index) ikawa chini sana. Nchi nyingi za Low Middle Income zinalalamika sana kuomba zifikiriwe upya na mashirika ya kifedha. Baadhi ya Nchi zinaomba kwa Benki ya Dunia zishushwe daraja ili kukwepa hasara hizi. Sisi tunashangilia sana. Nadhani hatujui tunachoshangilia ni nini.

Kwa Nchi kama yetu ni muhimu sana Viongozi kuwa na uwezo mkubwa wa kutofautisha kati ya Uchumi wa Takwimu na Uchumi Halisi wa Wananchi. Uhalisia ni kuwa uchumi wa wananchi ni goi goi sana. Hali ya maisha ya wananchi imeanguka kutokana na kupungua kwa shughuli za uchumi za uzalishaji mali. Katika miaka 5 Serikali ya Awamu ya Tano imetumia Bajeti ya Shilingi Trilioni 162 sawa na wastani wa Dola za Marekani 1,173 ukizigawa kwa kila Mtanzania. Hata hivyo katika miaka hiyo 5 Pato la Mtanzania limeongezeka kwa Dola za Marekani 30 tu. Hii maana yake ni kuwa Matumizi yetu ya Bajeti hayaongezi shughuli za Uchumi za Wananchi wengi.

Kwa mfano, wakati tumetumia Shilingi 1.8 Trilioni kwenye matumizi ya kununua Ndege 11 zinazotumiwa na 5% ya Watanzania, katika miaka 5 tumetumia Shilingi Trilioni Moja tu kwenye matumizi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotegemewa na 67% ya Watanzania. Bajeti hii ya Kilimo ni 0.6% ya Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka 5.

Kutokana na Hali hiyo ya matumizi yasiyozingatia shughuli za uchumi za wananchi, taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania Economic Upadte number 11 ) inaonyesha kuwa jumla ya Watanzania 2.7 milioni wameingia kwenye dimbwi la umasikini Kati ya Mwaka 2017-2019. Unakuwaje Nchi ya Uchumi wa Kati wakati mamilioni ya Wananchi wanakuwa masikini kila mwaka ?

Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa kasi tuliyokuwa nayo kwa miaka 5 iliyopita inatia mashaka ikiwa tutafika lengo letu la Uchumi wa Kati miaka 5 ijayo iwapo tukiendelea na maono haya, fikra hizi na matendo haya. Kuvuka mpaka ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu. Mpango wa Taifa unatutaka tufikia Pato la Kila Mtu la walau Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka ifikapo 2025.

Kufikia lengo hili inakuja na wajibu mkubwa kwa kila mmoja wetu kama Taifa na tunahitaji Uongozi na maono mapya. Tunahitaji Wananchi wawe na Raha na Furaha, wakifanya Kazi kwa bidii na kufurahia matunda ya jasho lao ( #KaziNaBata ).

Lindi, Tanzania

3/7/2020
Tatizo nilionalo hapa ni "Wivu wa Kimapenzi" na "upigaji" hivyo ulinzi wa Raisi uongezwe
 
Ni juzi tu Walikuwa wanatuambua watanzania ni maskini tunabangaiza hivyo lockdown itatuua,mwezi mmoja ghafla tumekuwa matajiri Kama laizer
 
Ukishakuwa na fedha ni lazima utakuwa na maendeleo, utamzidi nani na nani, that is another case.
Kwa tafsiri hiyo unapingana na wanaodai kuna maendeleo ya vitu na watu, au?
 
Asante kwa ufafanuzi
====
Mkuu naweza kupata utaratibu wa kitafiti uliotumiwa kupata takwimu hii ya 2.7 mil kuingia kwenye dimbwi la umaskini? Je. NBS yetu ilihusishwa kwenye utafiti huu?

NBS imehusishwa kutangaza uchumi wa Kati? Kama mnapenda Benki ya Dunia kuwatangaza kuwa Uchumi wa Kati, mpende pia wanaposema kuwa Watu masikini wameongezeka
 
Mkuu ni kweli pesa imeongezeka thamani Kwasababu Rais Magufuli amefuta rushwa, amefuta ufisadi, amekomesha madawa ya kulevy, amekomesha majangili na majizi

Kama ulikuwepo kwenye hiyo cheni lazima pesa ikupige chenga uone maisha magumu

Makundi mengine yanafurahia maisha Kwasababu hawajaathiriwa na kitu chochote, ukizingatia Rais Magufuli anawatetea sana watu wa kipato cha chini
Rushwa ipo ya kutisha, waulize madereva wa malori watakupa issue zote
 
Contrary to the fact ndio maana kuna nchi zimedai economic rebase to reflect activities of their sorrounding.

Asilimia kubwa ya watu wa mjini including yourself wakienda kutembea vijijini wakirudi mjini wengi wanarudi kwa kupewa zawadi za nafaka kama sio gunia basi debe au mfugo au ata wakinunua masokoni ni way cheaper kushinda wanapoishi.

Tatizo la ugumu wa vijijini ni kuweza kupata masoko ya uzalishaji kitu ambacho Magufuli anawapigania.

Sijui wewe mimi binafsi nikienda huko kijijini kwetu Nyabula hizo zawadi ni kushinda unachowapa wao.

Magu anapigana kuwapatia hawa access ya masoko mkuu tumuunge mkono. It’s about social utility (we have to look at the bigger picture) pamoja na weakness zake.

Watu kama Zitto wapo kwa ajili ya kuvunja jitihada kwa sababu awaelewi malengo ya Magufuli.

Kuna wakati wa kusikiliza upuuzi wa Zitto hila sio kipindi hiki for now kila mtu anatakiwa kuelewa Magufuli anataka kutupeleka wapi.

Nikishaona mtu anazungumzia maendeleo/uchumi kisha matarajio yake yakawa ni mtu nachafukwa kabisa. Haya maendeleo ya kutegemea mtu mmoja ndio yalitukwamisha wakati wa Nyerere. Tulikwenda vizuri sana mwanzo, lakini mwisho wake tukaishia kuvaa viraka na kugeuka masikini wa kutupwa.

Unasema kuwa huko vijijini kuwa ukienda unapewa zawadi kadhaa kama mahindi nk. Hilo ni kweli kabisa, lakini kwenye utoaji wao, wanatoa kwakuwa wametosheka au wako nje ya poverty circle? Ninachoona huwa wanatoa kwa sababu ya upendo, na mazoea yetu waafrika ya kumkirimu mgeni. Hayo masoko anayowapigania ni kama kilichotokea kwenye korosho?

Wakati wa Nyerere tulikwama, maana watu kama akina Zito wenye mitazamo mbadala walionekana maadui, na mawazo ya mtu mmoja tu yakawa ndio sahihi! Na ww hapa naona unaelekea kulekule kuwa Magufuli yuko sahihi, na michango ya kina Zito ndio inamkwamisha Magufuli ambaye unajua atakutoa ulipo kwa mawazo yake sahihi! Hapa naona unaoongozwa na mahaba niue zaidi. Nimecheka sana hapo paragraph ya mwisho, kuwa kwa sasa kila mtu anapaswa kuelewa Magufuli anatupeleka wapi!
 
Kwa tafsiri hiyo unapingana na wanaodai kuna maendeleo ya vitu na watu, au?

Kaka niwe mkweli tu, hapa ninaona sentensi ya kiswahili inayoishia na alama ya kuuliza, lakini unataka kuniuliza nini, nimekwama. Huenda una swali au hoja nzuri, ila unapungukiwa na maneno sahihi ya kuyaweka.
 
Back
Top Bottom