Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati? - Zitto Kabwe
...
Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu.
...
Nimalizie kwa kusema kuwa, kwa kasi tuliyokuwa nayo kwa miaka 5 iliyopita inatia mashaka ikiwa tutafika lengo letu la Uchumi wa Kati miaka 5 ijayo iwapo tukiendelea na maono haya, fikra hizi na matendo haya. Kuvuka mpaka ni hatua muhimu na ya kufurahisha lakini bado hatujafika safari yetu. Mpango wa Taifa unatutaka tufikia Pato la Kila Mtu la walau Dola za Marekani 3,000 kwa Mwaka ifikapo 2025.
Kufikia lengo hili inakuja na wajibu mkubwa kwa kila mmoja wetu kama Taifa na tunahitaji Uongozi na maono mapya. Tunahitaji Wananchi wawe na Raha na Furaha, wakifanya Kazi kwa bidii na kufurahia matunda ya jasho lao ( #KaziNaBata ).
Lindi, Tanzania
3/7/2020
Mh Zitto, wewe unajinasibu ni mchumi, umefanya uchambuzi wa kina kuhusu namna Pato la Taifa linavyototolewa, lakini unahitimisha kinadharia nyuma yake ukiwa na malengo binafsi na ya kisiasa.
Kama unakiri kumekuwa na ongezeko la $3 kila mwaka katika awamu hii ya utawala; kama unakubali utawala umetumia fedha nyingi katika km kununua ndege na kuwekeza katika miradi mikubwa, kwa nini huoanisha uwekezaji huo kama kichocheo cha kukua kwa uchumi?
Kwamba kwako wewe hiyo fedha ungewekeza kwenye kilimo wakati unajua bayana kilimo pasipo kuwa na soko, miundo mbinu imara ya usafirishaji na mazingira rafiki kwa mkulima kuongeza tija katika kilimo, ni sawa na ndoto za mchana.
Labda unajisahaulisha au kukwepa, kwa makusudi, kwamba pamoja na kuwa Mbunge kwa kipindi kirefu hukuweza kuinua kilimo cha Michikichi jimboni kwako kama zao kuu la biashara hadi Serikali iliyoko madarakani kufanya hivyo. Na hata vile badala ya kushirikiana nayo umekuwa ukiilaumu kuhusu zao la korosho ambalo si zao la jimbo lako (charity begins at home)
Unajua, kama mchumi, na ndicho kinachofanywa na Serikali iliyoko madarakani, kujenga mifumo imara (huduma za jamii) na kuimarisha miundo mbinu, kunachochea kukua kwa uchumi na hatimaye kupanua wigo wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi wake mwenyewe na wa Taifa.
Kwa hoja hiyo natoa mfano wa mkulima (umependa kuzungumzia kilimo):-
√ Kuwepo kwa usafiri wa uhakika wa majini, ardhini na angani, kunamhakikisha kufikisha mazao yake ya kilimo (japo kidogo anachozalisha) kwenye masoko yaliyo mbali. Kama si yeye wataenda wafanyabiaashara wa mazao kununua;
√ Kuwepo kwa viwanda kunamwongezea mkulima huyo soko la mazao yake ya kilimo; na
√ Kwamba Serikali inaboresha na kupanua huduma za jamii, kunaimarisha na kuongeza uwezo wake mkulima kiafya na kiakili kumudu changamoto za maendeleo yake mwenyewe.
IWEJE UPOTOSHE MAANA YA KUONGEZEKA KWA PATO LA TAIFA.
Natumaini, wakati tukielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, chama chako kitaweka hadharani Sera na Mikakati mbadala ya maendeleo ambayo itaendeleza yaliyofanywa na Serikali iliyoko madarakani, kama ulivyokiri, nanukuu
Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu
Unahitimisha andiko lako, lililojaa kebehi tupu, kwa kuaminisha WaTz kuwa mkiingia madarakani ni
#KaziNaBata, pasipo kueleza ni kazi zipi za kumpata huyo Bata?
HapaKazi Tu# angalau imewezesha kipato kuongezeka kwa $3 ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa kwenye vichocheo vya maendeleo.