Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Asante kwa ufafanuzi
====
Mkuu naweza kupata utaratibu wa kitafiti uliotumiwa kupata takwimu hii ya 2.7 mil kuingia kwenye dimbwi la umaskini? Je. NBS yetu ilihusishwa kwenye utafiti huu?
Nbs sindio wapika takwimu ili kumfurahisha mteuzi?
 
Umeelewa alichoandika Zitto?
 
Muhimu ni wewe kukiri kwamba unapoenda kijijini ukirudi mjini zawadi ni kitu ambacho unatarajia, ina maana wenyeji hadi kufanya ivyo wamezalisha ziada.

Ndio maana uchumi kama somo liko kwenye mpaka wa social science and hard science because human behaviour also dictates the economy.

Ndio ujue sasa hadi wewe kupewa chakula na bibi/shangazi ina maana wamezalisha vya kutosha now that value should be reflected as production lakini aipo kwenye statistics maana yake nini considering GDP is a measure of output na wewe unarudi mjini na debe ambalo alijaesabiwa kwenye gharama za uzalishaji wanachosema mabeberu aki reflect Tanzania.

Nenda Kenya, Rwanda au Burundi uone kama ndugu watakurudisha na debe au gunia la mahindi; wayatoe wapi wakati ardhi ya kulimia ziada awana. That makes land an injection into the economy ni kiasi ganj serikali yetu inagawa kila mwaka?

Asubuhi njema kwako me out; muhimu kukumbuka we are not a poor nation Magu is right sisi ni nchi tajiri tuwakwepe matapeli kama akina Zitto wenye nadharia potofu za kukariri na kutaka kupotosha sisi nchi maskini
 
Uchambuzi mzuri, ila pongezi ziende kwa magufuli kufikia uchumi wa kati
 

Mkuu unachekesha ile mbaya, unaenda kijijini unatoa sio chini ya 50,000, hapo umejibana ile mbaya. Halafu unapewa debe 2 za mahindi ambazo ni chini ya 20,000, achia mbali kubeba ,na ukija hapa mjini hujui hata mashine ya kwenda kusaga. Kama sio wendawazimu ni nini?

Kwa mitazamo yako hii ya mahaba niue, lazima mitazamo mbadala kama ya kina Zito uikatae.
 
Hii inaitwa Surprise!!

Kipindi ambacho Tanzania haikutarajia kuwa ndio imekuwa!!

Tumlaumu Nani Kati ya serikali na WB katika hili?

Hii inaitwa, ondoa uwoga! Sasa wewe umekuwa!!! Tunaogopa nini kwani??

Kwani waliokuwa wametuweka kwenye kundi la nchi masikini zaidi ndio hao tena wametuweka kwenye kundi la nchi zenye Uchumi wa Kati!!

Zitto mbona unaweweseka? Waandikie barua kuzuia hili, la sivyo wewe unatuchosha Tu? Imeshakuwa na imekuwa!
 
Moja, madaraja ya uchumi uliyoyanisha yana walakini sijui kwanini wakati taarifa zipo labda ulipitiwa kama binadamu, madaraja ya world bank ni haya as of 1st July 2019:
*Madaraja ( Kipato cha mtu)*
1. High income countries ($12376 na kwenda juu)
2. Upper Middle income countries ($3996-$12375)
3. Lower Middle income countries ($1026-$3995)
4. Low income countries ( $1025 na kushuka chini).

Kuseme tuko daraja la kati si kosa hata kidogo, japo tumetumia muda mwingi sana kuifikia hii hatua.

2015 kwa kufuata data za World bank Tanzania kipato cha mtu kilikuwa $980 na sio $1060 kama ulivyoainisha

Source:
GNI per capita, Atlas method (current US$) - Tanzania | Data

Mbili, hoja ya kukosa misaada na mikopo yenye riba nafuu kwa kupanda daraja.
-Tuseme uko sahihi maana hujatoa reference na sijaresearch, kwa nchi iliyopata uhuru mwaka 1961 kuwa na viongozi mbadala wenye mawazo ya uoga kama wewe ni aibu kwetu sote, ulitaka tutegemee misaada mpaka lini Ndugu Zitto?
Pia awamu hii wamenyimwa sana misaada lakini watanzania bado wameweza kuishi, kwahiyo hoja yako si ya kustua hata kidogo bali ya kustaajabisha.

Vinginevyo kuhusu dira ya uwekezaji, hii ni kazi yenu wanasiasa, ila kumbukumbuku yangu inaniambia haya yanayofanyika mlikuwa mnayaimba wapinzani wakati wa JK, sasa sijui kwnn sasa yakiwa yanatekelezwa mmeamua kubadili wimbo,

Mwisho nakubaliana na wewe jambo moja sekta ya kilimo itazamwe ili kichochea ukuaji wa haraka zaidi wa uchumi.
 
Huna Raha peke yako! Sisi watz tunashangilia! Etu Raha, hivi Raha ni Nini hasa!? Agenda kwa kweli kabisa mmeishiwa!
 
UNASHEREHEKEA NINI?
WAKATI WEWE HUMILIKI HATA KIBAJAJI?
Kwani Kuna ubaya ukisheherekea jirani kununua bajaji hata Kama hauna? Usiku ukizidiwa so angalau unaweza pata msaada kwa kupitia bajaji ya jirani badala ya kuhangaika kutafuta mbali!? Hebu toeni chuki zenu za kipuuzi dhidi ya jembe letu Magu na mafanikio tunayopata kwa kupitia yy! Kama vipi jitundikeni nyambafu!
 
Ndugu Zitto, jee Unajua kuna wana CCM wengi sana, nikiwa mmoja wapo, ambao haturidhishwi na mwenendo wa chama chetu, na tuna hang in the Air, tuko tayari kuu tilt upande wowote, na wengi wetu ni intelectuals tulio na ushawishi mkubwa na wenzetu wengi.

Ninakushauri tumia mbinu iliyotumiwa na Republicans na campaign ya Trump alipokuwa akishindana na Hilary. Wanachama wengi wa Democratic party walikpigia kura Trump kwa kutoridhika na siasa za Hilary.

Hebu tumieni mbinu ya kutopigania sana ubunge, na piganieni kura za uraisi, ili mshinde uraisi hata mkiwa minority ubunge, itakuwa historia na funzo la ajabu, na linawezekana.

Imagine, upinzani wameshinda Kura za Uraisi, na ubunge CCM 55%, Upinzani 45%.

Am just dreaming but a possible dream.
 
You are missing the point hiyo hela unayoacha kijijini ipo kwenye uchumi rasmi umeipata either kama sehemu ya mshahara au biashara ambayo TRA keshapitia ni sehemu ya outflow and inflow kwenye circular flow ya GDP.

Hizo debe mbili unazopewa hazipo kwenye hesabu za total yield ya kumlima (production) Tanzania idadi ya uzalishaji inahesabiwa kupitia maghala ya chakula tu sio stock ambazo wakulima wanabaki nazo nyumbani; na ndio hapo GDP aitoi picha kamili thamani ya mkulima anayobakiza na income wanazopata kama kuuza maziwa, uuzaji mazao wanaofanya njiani, sokoni as individual sole traders; ukijumlisha yote asilimia kubwa ya wakulima pato lao ni zaidi $1500 to $2000 dollars annually.
 
Zito its too late , magufuli hana mda na propaganda za kijinga. Anafanya kwa vitende na nyie mnanyanyua vidole juu kupinga maendeleo. Watanzania tunawaona mjue
 
Nchi haina maendeleo na pato kwa mwananchi wa chini bado linahesabika kwenye Nchi masikini sana Duniani, misaada itakatwa kwani Tanzania imeonekaa ipo kwenye uchumi wa kati haihitaji msaada
Inawezekana WB na mataifa makubwa yenye michango mikubwa kwenye bank hiyo, wameamua kuanza na hili la kutupandisha ili kutukomoa.

Na hii inatokana na kutoridhishwa na utawala uliopo sasa.

Hii ni sawa na kutuwekea vikwazo vya kiuchumi indirect.
NAwaZa Tu.
 
Wakati huku chini tunalia kilio cha mbwa meno juu!
 
Layman anawezaje kuelewa elimu kubwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…