Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,897
HOTUBA YA NDG. ZITTO KABWE, KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KATIKA HAFLA YA KUPOKEA WANACHAMA WAPYA WALIOKUWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 20 JUNI, 2020.
Ndugu Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo;
Ndugu Wanachama wenzangu wa ACT Wazalendo;
Ndugu Wanahabari;
Mabibi na Mabwana;
Assalaam Alleykum!
UTANGULIZI
Ndugu zangu;
Leo ni siku ya furaha sana kwetu sisi wana ACT- Wazalendo, ni siku ambayo jitihada zetu za kujenga Chama imara, mbadala na kimbilio la wapenda demokrasia zimeanza kuzaa matunda!.
Zikiwa ni siku chache baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na siku chache baada ya kuwa tumempokea Mwamba wa Kusini Mheshimiwa Suleiman Bungara, almaarufu Bwege, tunakutana kuwapokea waliokuwa Waheshimiwa Wabunge 20 katika Bunge lililovunjwa hivi karibuni.
Hii ni heshma kubwa kwa Chama chetu na uthibitisho kwamba Chama chetu kinazidi kuimarika, kuaminika na kushamiri miongoni mwa wapenda maendeleo wa nchi hii. Kutokana na ukubalifu wa ACT Wazalendo, magwiji wengine 20 tena waliokuwa Wabunge katika kipindi ambacho tulishuhudia baadhi ya Wabunge wakiuza utu wao na iman waliyopewa na wananchi, kwa kile kilichoitwa kuunga mkono juhudi!.
Kwa niaba ya Wanachama wenzangu, ninawashukuru sana kwa imani kubwa mliyoionesha kwa Chama chetu na kuwakaribisha sana kwenye Mabadiliko ya kweli!. Karibuni sana, na kazi iendelee!.
KWA NINI TUMEWAPOKEA?
Ndugu zangu;
Pengine mnajiuliza kwa nini imekuwa rahisi kuwapokea wanachama hawa wapya. Jibu ni rahisi sana, kwanza, Chama chetu kiko wazi kwa kila Mtanzania mwenye nia njema na nchi yetu kujiunga nasi; pili, wanachama hawa wapya kama walivyo Watanzania wengine wengi wamekuwa nasi bega kwa bega wakati wote bila hata kuwa Wanachama rasmi; tatu hawa ni miongoni mwa Wabunge makini walioendelea kusimama imara kusemea kero za wananchi na hivyo kuongeza sauti ya ACT Wazalendo Bungeni katika kupambania haki za kiraia na haki za kiuchumi kwa wananchi wote.
Baada ya kujiridhisha na mwenendo wa Chama chetu, umadhubuti wa Sera zetu katika kuleta mabadiliko ya kweli na ukuaji wa kasi wa chama chetu, ndugu zetu hawa, wameona huu ni wakati muafaka wa kujiunga Rasmi na Chama kinachokua kwa kasi kubwa nchini na kilichojipatia ukubalifu mkubwa miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii.
Ninapenda kutumia fursa hii kuwakaribisha watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii kujiunga na ACT Wazalendo na kuiunga mkono katika harakati zake za kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili.
JUKUMU KUU MBELE YETU
Ndugu wanachama wetu wapya,
Baada ya kujiunga rasmi na ACT Wazalendo, mko huru na mnazo haki zote kama mwana ACT Wazalendo mwingine yoyote. Kwetu hakuna mwenye Chama!, hiki ni chama cha wanachama wote na ni chama cha umma wote wa Watanzania.
Hivyo, kuanzia leo, mnalo jukumu moja kubwa, nalo ni kuhakikisha tunashinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar na tunaulinda na kuhami ushindi wetu. Vilevile, tunalojukumu la kuhakikisha tunang’oa mizizi ya chama dhalimu nchini kwetu na hivyo kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano ili kuleta furaha kwa Watanzania.
MATUMAINI MAKUBWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Ndugu wananchi;
Tunazo sababu nyIngi za kujivunia waliokuwa wabunge kujiunga na ACT Wazalendo na bado milango ipo wazi kwa wanaotaka kujiunga kwenye jukwaa la uhakika wa mabadiliko. Tunajivunia Wabunge ambao walitumia muda wao kufanya kazi ya kuisimamia Serikali na kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano ili Tanzania iwe na Muungano ulio sawa, wa haki na kuheshimiana.
Licha ya kwamba walikuwa wanaisimamia Serikali tukutu, isiyosikia na isiyo jali, lakini wanao uzoefu mkubwa wa kukabiliana na mikingamo, dhoruba na mapito mazito. Ni watu wasioyumba na ambao walidharau ukandarasi wa kununua utu wa watu kwa kinachoitwa kuunga mkono juhudi!.Ttunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kihistoria, tukiwa na watu wa aina hii, tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na matumaini makubwa sana, na tunaomba Wananchi mtuunge mkono!.
Wabunge hawa wastaafu wanahitajika zaidi katika miaka mitano ijayo ambapo mambo ya msingi ya Muungano ambayo hayaleti usawa, haki na kuheshimiana vinatakiwa kuzikwa kwenye kaburi la sahau. Ni miaka mitano ya kudai Tume ya Pamoja ya Fedha za Muungano, kuondoa unyonyaji, ukandamizwaji na kudogoshwa kwa sehemu moja ya Muungano. Ni miaka ya kuirudisha nchi kwenye misingi!.
Sina mashaka, wanachama wetu hawa wapya na wengine watakaojiunga hivi kaibuni wataendeleza ukali wa hoja hizi wakiwa ACT Wazalendo na kwa uwezo wake Mola mwaka huu tutakapounda Serikali zote mbili tutaanza hatua muhimu ya kurekebisha muundo wa Muundo wa Muungano na maboresho makubwa ya kiuchumi.
KAZI NA BATA DHIDI YA KAZI TU!
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu;
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 sisi ACT Wazalendo tumedhamiria kuijenga Tanzania inayopaa kiuchumi, tukibuni na kutekeleza sera zitakazohakikisha Uchumi Shirikishi unaozalisha AJIRA.
Chama chetu kitaongoza Serikali zitakazovutia uwekezaji kutoka nje (FDI) ili kuongeza mitaji nchini na kupanua shughuli za uzalishaji mali. Nataka kuongoza Serikali itakayotumia nafasi yetu ya Kijiografia ya kuzungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari kufaidika kiuchumi na kuhudumia nchi nyengine kwa kuifanya Tanzania kuwa Kituo Kikuu cha Usafirishaji na Biashara katika eneo la Maziwa Makuu.
Tutawekeza zaidi kwenye shughuli za wananchi wengi, haususan kilimo Kwa kuongeza eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na ufugaji, lengo la yote haya likiwa ni kuongeza shughuli za kiuchumi kwa Watu. Uchumi wa watu ndio unaojenga Taifa imara na sio Uchumi wa Serikali. ACT Wazalendo inataka kujenga Uchumi wa WANANCHI kupitia Vyama vya Ushirika, Jumuiya za Wafanyabishara na Vyama vya Wafanyakazi.
Tanzania ya ACT Wazalendo itakuwa ni Tanzania yenye huduma bora za kijamii, tukitoa elimu bora na inayokwenda na wakati, inayozalisha wahitimu wenye weledi, ubunifu na uwezo katika nyakati hizi za Sayansi na Teknolojia, Tanzania yenye wakufunzi wa kutosha, madarasa na vitendea kazi, huku mkazo ukiwekwa zaidi kwenye elimu ya ufundi.
Lengo letu ni kuwa na huduma bora na nafuu za afya, inayojikita kwenye kuwakinga na kuwatibu wananchi, kwa kuwa na Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za kutosha, zenye watendaji wenye sifa, vitendea kazi na vifaa tiba vya kutosha. Huduma ya uhakika ya maji safi na salama ikiwa ni kipaumbele chetu ili kupunguza maradhi yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo salama (ambayo hugharimu nusu ya Bajeti ya Dawa nchini).
Tutajenga mifumo imara ya utoaji haki nchini (Justice System) kwa kujenga uwezo wa kupambana na rushwa kwa haki na si kwa kukomoa, kuhakikisha watu wote walioonewa katika kipindi cha miaka hii mitano kwa kubambikiwa kesi kwanza wanaachiwa huru, na wale waliohukumiwa adhabu mbalimbali wakifutiwa rekodi zao za adhabu. Kwa kiasi kikubwa Tanzania hiyo ya ndoto yetu ACT Wazalendo ndiyo mahitaji ya Wananchi wengi - Tanzania yenye MAISHA ya RAHA na FURAHA (Yaani #KaziNaBata).
SABABU ZA KUKING’OA CHAMA DHALIMU
Ndugu zangu;
Miaka mitano tunayomaliza ni miaka mitano ya ukandamizaji, unyanyasaji, ukatili, chuki na umasikini mkubwa wa Wananchi. Ni miaka mitano ambayo Wananchi wamekuwa na maisha magumu kwa ujumla.
Wakulima wameshuhudia kipato chao kikianguka,; wavuvi wakiharibiwa nyenzo zao za kazi; Wafugaji wakiondolewa kwa nguvu maeneo ya malisho ya mifugo yao, Wafanyakazi wakinyimwa nyongeza halali na za kisheria za mishahara yao; Wafanyabiashara wakilazimika kufunga biashara zao au kuhamisha biashara zao, Waandishi wa habari wakipotea, wakifungwa jela kwa kubambikiwa kesi na vyombo vyao vya habari kufungiwa na Wanasiasa wa vyama vya upinzani wakihamishia ofisi zao kwenye korido za mahakama, jela au hospitalini..
Ni miaka mitano ya mateso makubwa ambayo yamewajaza wananchi wengi hasira na kisirani muda mwingi. Ni wajibu wetu kurejesha nyuso za furaha kwa Wananchi hawa kwa kuunda Serikali itakayojenga Tanzania inayopaa na yenye Watu wenye Raha na Furaha. Tunazo sababu zaidi ya elfu moja za kuing’oa CCM, na kwa hakika CCM ni lazima ing’oke ili nchi irudi katika misingi.
Tulipokuwa tunakusanya maoni kwa ajili ya kuandika Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2020 tulikutana na Wananchi katika shughuli zao za kila siku. Siku moja tulikwenda kukutana na wauza madafu mtaani. Walitueleza kuwa kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani muuzaji mmoja alikuwa anaweza kutembea mji mzima kwa siku na kuuza madafu ya wastani wa shilingi 80,000 yaani madafu 80. Tangu mwaka 2017 siku akiuza madafu 20, yaani shilingi 20,000 ni siku ya bahati sana. Mnaweza kuona namna ambavyo Sera mbovu zinazominya uchumi wa watu wa kati zinavyoweza kuathiri mwananchi wa chini kabisa.
Ninafahamu kwamba, Serikali ya CCM imebobea kwa ulaghai na uongo, tunatambua takwimu zao za kubumba zilizotolewa juzi wakati wa kuahirisha Bunge, tunao uchambuzi makini na wakati wa kampeni za uchaguzi tutauanika hadharani, ili wananchi wajiridhishe zaidi kwamba CCM haistahili kuongezewa hata siku moja kuongoza Tanzania.
HITIMISHO
Nihitimishe kwa kuwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge wastaafu, ambao tuna imani miezi michache ijayo watarudi Bungeni kwa kishindo chini ya Serikali itakayokuwa imeundwa na ACT Wazalendo ama Zanzibar au Serikali ya Muungano au Serikali zote mbili.
Ninawakaribisha wanachama wetu wapya na ninawahakikishia ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha kuwa tunaleta MABADILIKO YA UHAKIKA kwa Watanzania. Watanzania wanataka Mabadiliko, ni Wajibu wetu kuwapa mabadiliko.
Asanteni sana na karibuni sana!