ngalelefijo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2012
- 3,966
- 2,596
Usipodhibitiwa wewe, utaleta madhara ki utani utani hivi hivi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena ya bunuasi🤠🤠🤠
Wewe hunaga akili ! Sasa tu simu anatopiga Makonda uto tayari umeshaona anafaa kuwa Rais!Ndugu zangu Watanzania, uchapakazi wa Mheshimiwa Makonda, ujasiri wake, uzalendo wake, kujitoa kwake kutetea wanyonge, ushupavu na umadhubuti wake umewakosha na kukonga mioyo ya Watanzania mitaani.
Ambao kwa sasa wana kiu ya kutaka kuona Paul Makonda anagombea urais na kuchaguliwa kwa kishindo kumpokea kijiti cha urais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan mwaka 2030.
Sauti zinaendelea kupazwa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, sauti za wananchi vilingeni na magengeni kuona kuwa siku moja Taifa hili linawekwa mikononi mwa Paul Makonda kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu wetu.
Kutokana na kuona namna anavyochapa kazi bila kuchoka wala kupumzika, wala kupata hata muda wa kula chakula cha mchana. Muda wote yupo kazini kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana na kuchukua hatua papo kwa papo kwa kuwaita watu wa serikali kutoa majibu.
Nami naunga mkono kuwa ili kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Rais ziwe na muendelezo mzuri na kuendelea kwa kasi hii hii, basi ni vema mwaka 2030 kumpa ushirikiano na kumuunga mkono Paul Makonda kushika nchi.
Kwa hakika ndugu zangu, nawaambieni ya kuwa kwa huyu mwamba na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la Sahara, hakika nchi itakwenda mchaka mchaka katika maendeleo.
Maendeleo yatakimbia kwa kasi na kukimbizwa kama mashindano ya mbio ndefu, watumishi wa umma watachapa kazi kama nyuki, cheo kitakuwa dhamana na wananchi watabaki mabosi huku kila mtu akifurahia kuzaliwa Tanzania kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa Rais Wetu Mpendwa, Kipenzi cha Watanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.
Jiulize kama leo ni Mwenezi wa Chama anaitetemesha na kuiteka nchi kiasi hiki kwa uchapakazi wake, vipi tukimpa Urais ili aendeleze pale alipoishia mama yetu mpendwa na mchapa kazi aliyetukuka? Kwa sababu ni lazima anapotoka mchapa kazi kama Mama Samia, tukakikishe nchi inakwenda katika mikono ya mchapa kazi na jasiri aina ya Makonda ili kazi zisisimame na kusua sua.
Tanzania inamhitaji sana Mheshimiwa Paul Makonda 2030 kuliko wakati mwingine wowote ule. Ndio maana jana nilisema alindwe kwa nguvu zote na gharama zozote zile ili aje kutupatia matokeo makubwa na chanya Watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema tu.
Ni lazima Makonda aandaliwe na kuwekwa tayari kwa nafasi za juu, maana amejaliwa kipawa na kalama ya uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nyote mnajionea namna kifua chake kilivyojaa ujasiri wa hali ya juu.
Angalieni namna mchaka mchaka unavyopigwa huko kwenye ziara zake, angalieni namna watu nyuso zao zilivyo na tabasamu zimuonapo Paul Makonda, angalieni namna watu wanalivyo na imani na matumaini na Mheshimiwa Makonda. Hapo hata mwaka mmoja tu hajamaliza ofisini.
Vipi akipewa miaka kumi kama Rais wa nchi? Mnafikiri Tanzania hii ya Rais wetu mpendwa Mama Samia itakuwa wapi? Ikumbukwe kwanza atakuta kazi kubwa imefanywa na Mheshimiwa Rais Mama Samia, ambapo atakuta umeme ni wa uhakika baada ya kuwa tayari bwawa la Mwalimu Nyerere limeshakamilika.
Mnafikiri nani ataipita kiuchumi Tanzania hii yenye rutuba nzuri ya kutosha na yenye kukubali kila aina ya mazao, yenye mlima mrefu barani Afrika, yenye mbuga za wanyama wa kila aina, yenye madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee, yenye madini ya kutosha karibu kila ukanda, yenye rasilimali watu ya kutosha, yenye mito, maziwa na bahari kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na hata usafiri wa majini.
Yenye bandari kila kanda, yenye faida ya kuzungukwa na nchi zaidi ya saba ambazo zinategemea kupitishia mizigo yao katika bandari yetu, yenye misitu mingi kwa ajili ya kutengenezea vitu vya aina mbalimbali badala ya kuagiza nje na hivyo kupunguza hazina ya pesa za kigeni. Mnafikiri Tanzania ya kijana jasiri na imara mwamba Paul Makonda itakuwaje?
Mnafikiri Tanzania ya Makonda yenye utajiri wa makaa ya mawe ya kutosha, vivutio vya utalii, kimondo cha pili kwa ukubwa duniani baada ya kile cha Marekani, hamuoni Tanzania hiyo itatiririsha maziwa na asali katika mabomba yake kwa kila kaya? Kumbuka, kwa sasa anachofanya Rais Samia ni kuweka misingi mizuri ya kiuchumi, ambapo ni wakati huo wa Urais wa Makonda miradi ya kimkakati itakuwa imeanza kutoa na kuleta faida.
Tujiandae kumpa nchi Mheshimiwa Paul Makonda mwaka huo wa 2030 ili dunia ikae chini na kuishangaa Tanzania ikipaa kama ndege vita kiuchumi, na kupokea wageni watakao kuwa wanapanga foleni na kupishana pale airport wakija kuitembelea Tanzania na kujifunza.
Paul Makonda, chapa kazi sana kaka yangu. Mama amekuamini na anaimani na matarajio makubwa sana kutoka kwako. Chama tunakuamini sana na tuna matarajio makubwa sana kutoka kwako.
Chapa kazi na kila upitapo waambie wananchi na Watanzania mambo makubwa aliyoyafanya mama yetu na Rais wetu Mama Samia. Waeleze mabilioni aliyoyapeleka katika maeneo yao. Waambie kila mwezi mama yao na Rais wao anatoa zaidi ya bilioni 33 ili watoto wao wasome bure.
Waambie Rais wao ametiririsha zaidi ya trilioni sita katika sekta ya afya pekee, waambie Rais wao ameongeza bajeti ya kilimo kufikia bilioni mia tisa tisini ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nzuri, waambie mama yao ameagiza zaidi ya tani laki moja za sukari kuja kuingiza sokoni, waambie mama yao anawapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu wenye sifa bila ubaguzi.
Waambie mama yao ametoa maelfu ya ajira kwa vijana na muda siyo mrefu anakwenda kumwaga mitaani zaidi ya elfu ishirini na tatu katika sekta ya elimu na afya.
Waambie watumishi wa umma wachape kazi, maana mama yao yupo pamoja nao na ataendelea kuwaongeza mishahara na kuwalipa madai yao, lakini nao wahakikishe kuwa wanachapa kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na wasifanye kazi kwa mazoea. Waambie mama amefanya mengi ambayo huwezi kumaliza kuyataja.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Vipi unyonge utaisha lini au ni foreverWatanzania wanahitaji mtetezi wao.kama alivyo mama Samia .Na sasa wanataka Rais samia anapomaliza muhula wake wa pili aliache Taifa mikononi mwa mchapa kazi na mwenye kuwajali wanyonge ambaye ni Mheshimiwa Makonda
Rais wa jamuhuri ya muungano wa TanzaniaRaisi wa Kolomije?
Bila shaka una matatizo ya akili.Wewe hunaga akili ! Sasa tu simu anatopiga Makonda uto tayari umeshaona anafaa kuwa Rais!
Elimu duni ya Tanzania imezalisha watu wenye akili kama za misukule!
Huyu Lucas Mshamba ni jitu Kilaza sana!
Kwenda zako huko shetani mkubwa wewe.Usipodhibitiwa wewe, utaleta madhara ki utani utani hivi hivi
Acha ujinga weweHuyu jamaa kuna nchi ni wanted kama jangili
Akipita yeye na Mungu akampa kibali na kumuinua wala haina shida ya aina yoyote ile. Lakini ningependa kukujibu ya kuwa ndani ya chama chetu cha CCM hakuna kiongozi mwenye Damu mikononi mwake. Ndio maana hakuna mashitaka ya aina hiyo katika mahakama ya aina yoyote ile na ngazi yoyote ile hapa nchini.We chawa Lucas mwashambwa 2030 rais Ni January Yusuph Makamba. Kijana asiye na damu mkononi Wala doa lolote.
Kijana msomi mwenye busara na asiye na makuu au kujipendekeza.
Tuombe uzima tuTena ya bunuasi🤠🤠🤠
Mimi nilipofikia sihitaji chochote kwa yeyote,Wewe unataka wote tufikiri kama wewe nyumbu! Siku inafika ndo ujinga gani? Hao wote wasaka maisha tu pambana kivyako!
Hakuna siku Mbowe atakusaidia chochote zaidi ya familia yake na marafiki zake! Kwa hiyo usijisahau sana maana nyinyi nyumbu mnaamini kila mtu hata kama Jizi kama Mbowe!
Unaelewa maana ya mnyonge?Ukiona unaitwa mnyongeee kaaa mguu sawa
Ova
Wewe ndiye unayedharaulika.Ila nimegundua kwanin dunia inatudharau waTanzania