Watanzania wapigwa tena na Kampuni ya Upatu ya "Best Capital Management" zaidi ya Bilioni 15

Hii michezo huwezi kuelewa kwa vile hakuna close monitoring na watanzania wengi hawana ufahamu.

Mfano serikali inaweza kuwapa vibali ila mnajua vibali gani? kama ni financial ishu lazima wawe subjected to finance act ili wapete vibali kutoka BOT .

sasa wengi mnaonyesha usajili wa kampuni sijui brela na zile namba pale chini hmafuatilii ndo maana bongo cheti ndo kinatambulisha uwezo wa mtu hata kama kichwani ni zero.

unaweza kuta kampuni imesajili kufanya shughuli zake binafsi wakachomekea uwekezaji kwa nia ya kutapeli lazima mpigwe tu😂😂.

Mambo ya uwekezaji yanahitaji kusoma sana sio kukurupuka wacha wapigwe
 
Hizi kampuni huwa wanashirikiana na watumishi wa umma. Kuna kibosile mmoja somebody Katembo naam, kahusika sana hizi mambo.
Wanajua watz wanapenda dezo na wavivu wa maarifa. Nchi hii kupiga ni rahisi sana.
 
Sifa kubwa ya sisi wadanganyika ni Ujinga,ubishi na ujuaji.Kwenye hizo sifa lazima tamaa na kukurupuka havikosekani.Kwahiyo unaposikia kua nchi ina wajinga wengi uelewe.
 
Afya ya akili
 
Hapo ngoma droo maana hata hao Viongozi wa dini, kazi yao kuwapiga sadaka waumini wao
 
Wacha wapigwe tu mana kila siku watu wanaambiwa lakini hawasikii
 
Ongezea na viongozi wa dini
Huko nako kunakupigwa kama kawaida
 
Hao wanaoweka billion ndio wez wenyewe bro stuka. Anaweka kama wewe kumbe yuko nao wanatengeneza mazingira ya kuaminika. Nasema kila cku hii nchi ng'ombe ni wengi kuliko unavyofikiri.
 
Mkuu hii nchi hata ambao unaona wanaakili wanapigwa kizembe mnoo. Kuna wanajeshi flani hivi walipigwa hela Kama milioni kumi hivi kwa haya maswala ya upatu. Ila hata maprofesa na mawaziri wanalizwa Sana pesa na matapeli kwa tamaa zao. Usiwaone wanavaa matai na suti hamna kitu vichwani. Ndoo maaana mkiwatukanaga walimu humu kuwa ni kada ya watu wasiojielewa huwa na cheka Sana. Watanzania wengi uelewa Mdogo Sana.
 
Hahaaa hata mi nachekaga sana watu wakitukana walimu eti hawajielewi wakati suala la kutokujielewa ni la watanzania bila kujali kada ,kuna mkurugenzi mmoja wa halmashauri moja ya Dsm aliuziwaga madini feki huku Tanga nikikumbuka nacheka sana
 
Hivi GNLD na FOREVER LIVING bado yapo
Imeshawahi kufanya mfanyakazi mwenzangu akaacha kazi baada ya muda akawa anaishi kwa msoto mkubwa mno.
Haya sio makampuni ya upatu isipokuwa ni makampuni ya kuuzwa madawa ya virutubisho au supplements
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…