Nmesema uandishi wenu wa Kiswahili huwa majanga, soma mada nyingi humu jinsi wengi huwa mnaandika, halafu zingatia kwamba huyo mwandishi ni Mtanzania wa kawaida ambaye sote tunafahamu hajui kuongea lugha yake ya asili na pia Kingereza hakijui. Ni jambo la maana na muhimu kuhakikisha upo vizuri kwa walau lugha mbili, sio uwe mbumbumbu uliyefungiwa ndani ya lugha moja.
Halafu hapo umesema Kenya, nafikiri ulidanganywa, labda ukute mzee wa zamani sana kijijini ndiye hajui Kiswahili, lakini wengi wanakijua ila pia wanaenzi lugha zao za asili. Ukiona rais amekwenda sehemu na kumtumia mtu wa pale kuzungumza nao, sio kwamba hawatamuelewa akiongea Kiswahili, lakini utakuta huyo anayetumiwa anayo umaarufu fulani kwa watu wa pale, na pia akiongea nao kwa lugha yao ya asili wanapata ushawishi mkubwa.
Lugha ni muhimu katika kuunganisha watu, na ndio maana kingereza kimesaidia pakubwa duniani katika mawasiliano ya kibiashara baina ya watu wa kutokea asilia tofauti. Kipindi fulani nilikua na mradi hapo Tanzania ambapo timu yetu ilikua na wahandisi Wachina, Wamarekani, Mnigeria, Watanzania na Wahindi lakini tuliwasiliana kikazi kwa kutumia Kingereza, kilituleta pamoja.
Sasa leo mkijifanya wajuaji eti mnaogopa Kingereza kisa kinawashinda, hadi viongozi wenu wanaogopa kutoka na kusingizia matumizi, mtaendelea kubaki nyuma kwenye umaskini licha ya nchi yenu kuwa na kila kitu, mnajikuta madini kama Tanzanite hayahusishwi na Tanzania hata mkiweka ukuta unaofika binguni.