eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Umetumia maneno mengi kueleza kitu kidogo sana, na humo ndani umenilisha maneno.
Kwanza kabisa uandishi wa Kiswahili haupimwi kwenye magazeti maana yanahaririwa, nazungumza kuhusu uandishi wa wengi wenu kwenye shughuli za kawaida hata huku kwenye mitandao, au hata barua za kawaida tu na jumbe zingine.
Halafu kwetu hakuna asiyezungmza Kiswahili, labda mababu wa enzi zilee vijijini, wewe hapo labda unawakatalia kwa kupima wanavyo ongea kwa lafudhi/accent zao, mtu kuongea Kiswahili au Kingereza kwa lafudhi ya asilia yake sio kipimo tosha kwamba hajui hiyo lugha husika. Hili lipo hata kwa Warusi au Wajerumani wakati wanaongea Kingereza, lazima utamskia akiongea kwa kingereza kizuri lakini kwa lafudhi ya kwao. Hata Watanzania ukiwaskia Kingereza huwa wanachomekea ZE ZE ZE nyingi.
Hapo nilisema Kingereza kinaunganisha dunia sikumaanisha ndicho kinatumika kwenye kila nchi, bali ndicho kinawezesha mazungumzo baina ya watu wa matabaka mbali mbali, nikakupa mfano hapo Bongo nilikua na mradi uliowahusu Wamarekani, Mnigera, Wachina, Wahindi, Watanzania hata jamaa kutokea Mauritius na Wasouth-Afrika Kusini lakini hatukutumia Kifaransa wala Kijerumani au Kiswahili ila Kingereza kilituleta pamoja.
Hao Waturuki wanaowafungia reli hamuwasiliani nao kwa Kituruki au Kiswahili ila Kingereza, hata Wachina wanaochimba gesi, wote hamna jinsi ila Kingereza. Kwa hivyo kwako wewe kuwahadaa Watanzania wenzako wakomae na Kiswahili bila kujifunza Kingereza ni kwa manufaa yako binafsi lakini sio hiyo zuga ya uzalendo.
Punguza hisia katika kujenga hoja kama hizi. Ebu jaribu kutumia vizuri uwezo wako wa kufikiri.
Hivi Uzungumzaji na uandishi wa kiswahili wa mwananchi wa kawaida wa Tanzania unaweza kulinganisha na ncgi yoyote katika ukanda huu au hata Afrika na dunia kwa ujumla? Unadiriki kusema majanga wakati Kenya ambao ni moja ya lugha yao ya taifa wanaongea na kuandika kiswahili kibovu sijapata kuona. Ukweli ni kuwa licha ya mapungufu yaliyopo kwenye uandishi na uongeaji wa kiswahili, Tanzania niyo mfadhili na mmiliki wa lugha adhimu ya kiswahili.