Watanzania wasema Rais Samia anatosha na hakuna sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais 2025

Teuzi zimeisha pambana na maisha yako
Hii siyo barua ya maombi ya uteuzi Bali Ni andiko linalohusu maoni ya watanzania namna wanavyomkubali Rais Samia na kutoona sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Urais,kwa kuwa Rais Samia Anatosha
 
Kusifu kunazidi kiasi. Unaharibu sasa. Ninyi ndio walewale wa kumwongezea mwendazake miaka ya utawala kutoka 5-7. Sasa ona unataka KATIBA IVUNJWE. Leo familia yako ndio iwawakilishe watanzania wote kweli? Namkubali raisi anajitahidi sana. Lakini hawezi kukubalika na wa-tz wote.
 
Watanzania wapi hao ambao wengine hatuwasikii au unahisi tulihamia Burundi ??
Mamilioni ya watanzania wanahitaji Rais Samia Kuendelea kuwatumikia mpaka 2030, kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi
 
Ndugu zangu watanzania,

sauti za mamilioni ya Watanzania ni kiu Yao ya kuhitaji utumishi wa Rais Samia mpaka 2030, watanzania wengi wameguswa na uchapakazi wa Rais Samia, wametekwa mioyo Yao na kazi za Rais Samia ambazo zimeleta Tabasamu na Taswira mpya ya kimaendeleo katika Taifa letu.

watanzania kwa wingi wao hawaoni sababu ya kupoteza mamilioni ya Fedha kwa ajili ya kuchapisha karatasi za nafasi ya Urais wakati utendaji kazi wa Rais Samia umejibu maswali ya Watanzania na kukata kiu Yao ya muda mrefu ya kuhitaji Rais mchapa kazi, mzalendo, msikivu, Jasiri, imara, madhubuti, shupavu, mwenye maono Sera na ajenda za kugusa maisha Yao.

Watanzania wanajiuliza wamtoe na kumnyima Rais Samia kura ili wampe Nlnani? Aje afanye nini kipya ambacho hajafanya Rais Samia? Aje na ajenda na Sera zipi ambazo Rais Samia hajazigusa katika maisha Yao?

Wanajiuliza kipi ambacho Rais Samia hajatekeleza ama kukigusa katika yote waliyoyahitaji watanzania?

Wanajiuliza kwanini wasimpe muhula wa pili Rais Samia ili aendeleze kazi njema aliyoianza ya kuijenga nchi yetu? Kwanini wamnyime Kura zao wakati muda wote amekuwa akizungumza ajenda zao?

watanzania wanamuona Rais Samia Kama mkombozi wao katika kuwakwamua kiuchumi,wanamuona Rais Samia Kama kiongozi mwenye uthubuti mkubwa Sana na ujasiri wa Hali ya juu katika kusimamia maslahi ya Taifa letu,wanaona namna Rais Samia alivyojitoa na kujitolea kulitumikia Taifa letu kwa moyo wa uzalendo, wanaona juhudi za Rais Samia katika kujenga uchumi jumuishi unaomgusa kila mtanzania pasipo kumwacha yeyote nyumaa,wanaona namna alivyotuvusha katika nyakati ngumu mpaka hapa alipotufikisha ambapo kila mtanzania Anayo matumaini makubwa Moyoni mwake ya kutimiza Ndoto zake.

Ndio sababu ya Watanzania kumhitaji Rais Samia Kuendelea kuwaongoza, Watanzania wanahitaji Rais Samia abakie ikulu Kama Rais wao na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,wanahitaji kuona Rais Samia aliendelea kuwatumikia na hawaoni sababu ya kuona Rais Samia akizunguka mikoani kuomba kura wakati kazi zake kupitia miradi mbalimbali inaonekana kwa kila mtanzania, Hivyo wanaona muda wa kampeni abakie ikulu akichapa kazi na kuwahudumia watanzania kwa kuwapelekea maendeleo yanayogusa maisha yao.

Kazi Iendeleee , mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Akili za UVCCM sijui mlipokonywa uwezo wa kufikiri.
 
Kusifu kunazidi kiasi. Unaharibu sasa. Ninyi ndio walewale wa kumwongezea mwendazake miaka ya utawala kutoka 5-7. Sasa ona unataka KATIBA IVUNJWE. Leo familia yako ndio iwawakilishe watanzania wote kweli? Namkubali raisi anajitahidi sana. Lakini hawezi kukubalika na wa-tz wote.
Nashukuru kuona hata wewe unamkubali na kuungana na mamillion ya watanzania wanaomuunga mkono Rais wetu mpendwa mama Samia,Hakika umechagua upande wa ushindi na upande wa wazalendo wa kweli wa Taifa letu
 
Mamilioni ya watanzania wanahitaji Rais Samia Kuendelea kuwatumikia mpaka 2030, kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi
Ebu punguza mihemko ,hao mamilioni nimekuuliza ni wawapo kwamba unahisi ni wewe tuu uliopo mtaani?? Usipende kueneza na kutapakaa maneno usiyo kubwa na uhakika nayo au kunakitu unakitafuta??
 
Ndugu zangu watanzania,

sauti za mamilioni ya Watanzania ni kiu Yao ya kuhitaji utumishi wa Rais Samia mpaka 2030, watanzania wengi wameguswa na uchapakazi wa Rais Samia, wametekwa mioyo Yao na kazi za Rais Samia ambazo zimeleta Tabasamu na Taswira mpya ya kimaendeleo katika Taifa letu.

watanzania kwa wingi wao hawaoni sababu ya kupoteza mamilioni ya Fedha kwa ajili ya kuchapisha karatasi za nafasi ya Urais wakati utendaji kazi wa Rais Samia umejibu maswali ya Watanzania na kukata kiu Yao ya muda mrefu ya kuhitaji Rais mchapa kazi, mzalendo, msikivu, Jasiri, imara, madhubuti, shupavu, mwenye maono Sera na ajenda za kugusa maisha Yao.

Watanzania wanajiuliza wamtoe na kumnyima Rais Samia kura ili wampe Nlnani? Aje afanye nini kipya ambacho hajafanya Rais Samia? Aje na ajenda na Sera zipi ambazo Rais Samia hajazigusa katika maisha Yao?

Wanajiuliza kipi ambacho Rais Samia hajatekeleza ama kukigusa katika yote waliyoyahitaji watanzania?

Wanajiuliza kwanini wasimpe muhula wa pili Rais Samia ili aendeleze kazi njema aliyoianza ya kuijenga nchi yetu? Kwanini wamnyime Kura zao wakati muda wote amekuwa akizungumza ajenda zao?

watanzania wanamuona Rais Samia Kama mkombozi wao katika kuwakwamua kiuchumi,wanamuona Rais Samia Kama kiongozi mwenye uthubuti mkubwa Sana na ujasiri wa Hali ya juu katika kusimamia maslahi ya Taifa letu,wanaona namna Rais Samia alivyojitoa na kujitolea kulitumikia Taifa letu kwa moyo wa uzalendo, wanaona juhudi za Rais Samia katika kujenga uchumi jumuishi unaomgusa kila mtanzania pasipo kumwacha yeyote nyumaa,wanaona namna alivyotuvusha katika nyakati ngumu mpaka hapa alipotufikisha ambapo kila mtanzania Anayo matumaini makubwa Moyoni mwake ya kutimiza Ndoto zake.

Ndio sababu ya Watanzania kumhitaji Rais Samia Kuendelea kuwaongoza, Watanzania wanahitaji Rais Samia abakie ikulu Kama Rais wao na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,wanahitaji kuona Rais Samia aliendelea kuwatumikia na hawaoni sababu ya kuona Rais Samia akizunguka mikoani kuomba kura wakati kazi zake kupitia miradi mbalimbali inaonekana kwa kila mtanzania, Hivyo wanaona muda wa kampeni abakie ikulu akichapa kazi na kuwahudumia watanzania kwa kuwapelekea maendeleo yanayogusa maisha yao.

Kazi Iendeleee , mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Anakutosha ww
 
Ebu punguza mihemko ,hao mamilioni nimekuuliza ni wawapo kwamba unahisi ni wewe tuu uliopo mtaani?? Usipende kueneza na kutapakaa maneno usiyo kubwa na uhakika nayo au kunakitu unakitafuta??
Makundi yote kuanzia wakulima ambao wanatabasamu baaada y kupewa mbolea za Ruzuku,vijana wa vyuo vikuu baada ya kuongezewa fedha ya kujikimu na kupewa mikopo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa, wafanyabiashara hasa baada ya kuboreshwa mazingira ya biashara,N,k,kila kundi linamkubali Rais Samia,kwa ufupi Ni kuwa Rais Samia ameyateka makundi yote na kupata uungwaji mkono
 
Nimegundua jamaa ndio anafanya utafiti hapa jukwaani sema majibu ni mepesi tu atapata
 
Makundi yote kuanzia wakulima ambao wanatabasamu baaada y kupewa mbolea za Ruzuku,vijana wa vyuo vikuu baada ya kuongezewa fedha ya kujikimu na kupewa mikopo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa, wafanyabiashara hasa baada ya kuboreshwa mazingira ya biashara,N,k,kila kundi linamkubali Rais Samia,kwa ufupi Ni kuwa Rais Samia ameyateka makundi yote na kupata uungwaji mkono
Kwahyo hao ndiyo mamilioni unayo yazungumuzia,unapozungumzia swala la mbolea za ruzuku kunasehemu hata hawajui kama kunakitu kinaitwa mbolea za ruzuku au wewe ndiyo mmoja wa wale watu siku hizi wanao itwa chawa
 
Kawa mkombozi wao katika kuwakwamua kiuchumi kivipi
 
Ushauri wa bure: mnavyotumi nguvu kubwa kuongea hoja zisizo mashiko mnazidisha hasira za wananchi na kumharibia mheshimiwa rais.

Kama uchawi wenyewe ndio huu basi hamna msaada wowote
 
moja katupitisha wakati mgumu upi unaosemea wew
Wakati wa mdororo wa uchumi wa Dunia uliotokana na Corona pamoja na Vita vya ukrein uliyopelekea mfumuko wa Bei Duniani kwote.

Rais Samia alifanya juhudi za makusudi katika wakati huo mgumu ulioitetemesha Dunia
 
Back
Top Bottom