Watanzania wasema Rais Samia anatosha na hakuna sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais 2025

Teuzi zimeisha pambana na maisha yako
Hii siyo barua ya maombi ya uteuzi Bali Ni andiko linalohusu maoni ya watanzania namna wanavyomkubali Rais Samia na kutoona sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Urais,kwa kuwa Rais Samia Anatosha
 
Kusifu kunazidi kiasi. Unaharibu sasa. Ninyi ndio walewale wa kumwongezea mwendazake miaka ya utawala kutoka 5-7. Sasa ona unataka KATIBA IVUNJWE. Leo familia yako ndio iwawakilishe watanzania wote kweli? Namkubali raisi anajitahidi sana. Lakini hawezi kukubalika na wa-tz wote.
 
Watanzania wapi hao ambao wengine hatuwasikii au unahisi tulihamia Burundi ??
Mamilioni ya watanzania wanahitaji Rais Samia Kuendelea kuwatumikia mpaka 2030, kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi
 
Akili za UVCCM sijui mlipokonywa uwezo wa kufikiri.
 
Nashukuru kuona hata wewe unamkubali na kuungana na mamillion ya watanzania wanaomuunga mkono Rais wetu mpendwa mama Samia,Hakika umechagua upande wa ushindi na upande wa wazalendo wa kweli wa Taifa letu
 
Mamilioni ya watanzania wanahitaji Rais Samia Kuendelea kuwatumikia mpaka 2030, kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi
Ebu punguza mihemko ,hao mamilioni nimekuuliza ni wawapo kwamba unahisi ni wewe tuu uliopo mtaani?? Usipende kueneza na kutapakaa maneno usiyo kubwa na uhakika nayo au kunakitu unakitafuta??
 
Anakutosha ww
 
Ebu punguza mihemko ,hao mamilioni nimekuuliza ni wawapo kwamba unahisi ni wewe tuu uliopo mtaani?? Usipende kueneza na kutapakaa maneno usiyo kubwa na uhakika nayo au kunakitu unakitafuta??
Makundi yote kuanzia wakulima ambao wanatabasamu baaada y kupewa mbolea za Ruzuku,vijana wa vyuo vikuu baada ya kuongezewa fedha ya kujikimu na kupewa mikopo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa, wafanyabiashara hasa baada ya kuboreshwa mazingira ya biashara,N,k,kila kundi linamkubali Rais Samia,kwa ufupi Ni kuwa Rais Samia ameyateka makundi yote na kupata uungwaji mkono
 
Nimegundua jamaa ndio anafanya utafiti hapa jukwaani sema majibu ni mepesi tu atapata
 
Kwahyo hao ndiyo mamilioni unayo yazungumuzia,unapozungumzia swala la mbolea za ruzuku kunasehemu hata hawajui kama kunakitu kinaitwa mbolea za ruzuku au wewe ndiyo mmoja wa wale watu siku hizi wanao itwa chawa
 
moja katupitisha wakati mgumu upi unaosemea wew
 
kawa jasiri katika kufanya nn ambayo yameshitua umma watanzania
 
Kawa mkombozi wao katika kuwakwamua kiuchumi kivipi
 
Ushauri wa bure: mnavyotumi nguvu kubwa kuongea hoja zisizo mashiko mnazidisha hasira za wananchi na kumharibia mheshimiwa rais.

Kama uchawi wenyewe ndio huu basi hamna msaada wowote
 
moja katupitisha wakati mgumu upi unaosemea wew
Wakati wa mdororo wa uchumi wa Dunia uliotokana na Corona pamoja na Vita vya ukrein uliyopelekea mfumuko wa Bei Duniani kwote.

Rais Samia alifanya juhudi za makusudi katika wakati huo mgumu ulioitetemesha Dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…