Watanzania Wasema wangeandamana na kugoma kabisa Kushiriki Uchaguzi kama CCM isingempitisha Rais Samia Kugombea Urais.

Watanzania Wasema wangeandamana na kugoma kabisa Kushiriki Uchaguzi kama CCM isingempitisha Rais Samia Kugombea Urais.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni Maneno yanayotamkwa Kwa Sauti kubwa na watanzania wote huku Mitaani ya kuwa wangegoma kabisa kushiriki Katika Uchaguzi na kufanya maandamano Makubwa sana ikiwa CCM isingempitisha Rais Samia kugombea Urais Mwaka huu.

Wanasema kwa kuwa Ni Rais Samia pekee ndiye aliyeonekana kukidhi vigezo na kukata kiu ya watanzania waliyokuwa nayo juu ya aina ya kiongozi waliyekuwa wanamhitaji. Wanasema ya kuwa Rais Samia amekidhi matarajio yao na kwamba ndiye kiongozi wa ndoto yao na amekuja kwa wakati muafaka.

Watanzania wanasema ya kuwa wamejionea namna serikali ya Rais Samia ilivyo wawezesha kuinuka kiuchumi na Kugusa Maisha ya kila mmoja. Wanasema ya kuwa serikali ya Rais Samia imemshika mkono kila mtanzania pasipo kumuacha Mtu nyuma.

Wanasema serikali ya Rais Samia imekuwa sikivu kwa watanzania na yenye kuwajali watu. Wanasema ya kuwa imekuwa ni serikali inayowatumikia watu muda wote. Wanasema ya kuwa serikali ya Rais Samia imekuwa karibu na wananchi na wakati wote imeshuka kwa watu kuwatumikia na kuwapatia majawabu sahihi kwa kila kitu.

Wanasema pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza mbele yetu kama Taifa. Lakini wamejionea wao wenyewe kwa Macho yao juhudi za serikali yao katika kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye Kumaliza kila changamoto inayojitokeza mbele yetu kama Taifa.

Wakakumbushia na kueleza kwa kina namna serikali yao ilivyopambana na kutatua changamoto ya kupanda kwa bei ya pembejeo hususan mbolea, kupanda kwa mafuta ,ukosefu wa ajira kwa vijana ,mishahara na maslahi ya watumishi wa umma,mikopo na pesa za kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu ya juu,suala la nishati ya umeme vijijini, demokrasia Nchini na mengine mengi sana.

Wanasema waliona juhudi za serikali yao kwa kuanza kushughulikia changamoto hizo kwa weledi mkubwa sana. Ndio Maana wanasema ya kuwa ni Rais Samia pekee aliyekuwa na anetebakia kuwa chaguo lao watanzania katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika mwishoni mwa mwaka huu Mwezi Oktoba.

Kwa hakika Rais Samia ni kipenzi cha watanzania ,ni kiongozi wa watu,ni chaguo la Mungu,ni chaguo la watanzania wote na kiongozi anayetosha na kustahili kuliongoza Taifa letu.
Screenshot_20250828-175337_1.jpg
Screenshot_20250831-205923_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom