Nenda kasome tena uchumi na maswala ya kodi..kwa kifupi serikali inatakiwa itengeneze mazingira mazuri ya kufanya biashara watu wawekeze yenyewe ije kuchukua kodi..sasa shida inaanzia hapa serikali inataka ichukue kiasi sawa na aliefanya uwekezaji.
1. Kwenye miamala ya simu service prodiver (Tigo,Vodacom, Airtel) wao wameshafanya uwekezaji kwenye infrastructure, minara,manpower etc. Kwaio wao warudishe gharama zao wameanzisha huduma kadha wa kadha i.e kutuma na kupokea hela sasa kwa kuangalia gharama walizotumia wameweka kiwango fulani cha ili kufikisha gharama hizo husika kwa mtumiaji wa mwisho.
2. Shida inaanzia hapa i.e kutuma kiasi fulani ni 400 tsh na kiasi cha kutolea ni 300 tshs...tukumbuke kwamba hio kampuni ya simu baada ya kutoa mapato na matumizi yake faida iliopatikana inatozwa 30% (corporate tax) pia inalipa PAYE kutoka kwa income tax kitu kisichoeleweka ni kutaka serikali nayo ichukue hela toka kwenye hizo gharama za kutuma na kutolea wakati baadae inakuja kukata kodi katika mahesabu ya mwisho wa mwaka hicho ndo hakikubaliki maana mzigo wote anasukumiziwa mlaji wa mwisho(mtuma hela)
3. Porojo za kujenga madaraja, mashule, mahospitali hazina uzito sababu hayo majengo sio kwamba yameanza kujengwa baada ya tozo kuanzishwa serikali imekua ikikusanya kodi toka sehemu mbali mbali tangu kupatwa kwa uhuru sasa iweje ndo useme kwamba tozo hizi ni za kufanyia hivyo vitu,kodi zingine zinaenda kufanyia vitu gani? Hapo unakuta kuta LC200 na Lc300 zinanunualiwa kwenye misafara etc isio kua na tija
4. Kwanza kabisa kujenga barabara,mahospitali, mashule hayo ni majukumu ya serikali sio fadhila..siku watu watakapo amka na kujua majukumu ya serikali na wajibu wake kwa wanachi ni upi ndio tutaelewena..hakika hio siku itafika hapo waongo waongo ndo watakapo kua wamefikia mwisho.
Principles zipi za taxation zinazotumika kutoza kitu mara mbili mbili?