Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Waziri Mkuu wa Uingereza, Margaret Thatcher aliwahi kusema, serikali haina duka wala biashara au shamba. Serikali inaendeshwa kwa kodi zinazotozwa kwa wananchi wake.
Wananchi hawakupenda sana kauli hiyo, lakini akawaambia hivyo ndiyo ilivyo kwenye free market economy.
Hivyo ndivyo ilivyo duniani pote. Serikali haifanyi biashara wala kuwekeza.
Serikali makini duniani kote zinatengeneza mazinira ya uwekezaji kwa WANANCHI WAKE ili waweze kupata kodi kutokana na biashara zao. Huo lazima uwe msingi wa nmna ya kupata kodi.
Sasa hapa kwetu Mwalimu alijaribu kuitumia serikali kuwekeza katika mashirika mengi ya Umma. Mashirika haya karibu yoote yalikufa, pamoja na uwekezaji mkubwa wa serikali.
Mwinyi alipoingia, aliingiza sera za kulegeza sharti ya biashara na kuiondoa serikali kwenye biashara.
Mkapa alijiongeza kwa kutengeza taratibu za ukusanyaji kodi na usimamizi mzuri kiserikali katika miradi yake(mfano TANROADS).
Tatizo kubwa ka wananchi walio wengi wa Tanzania ni kufikiri kuwa serikali ndio ikope kwa mjomba fulani huko nje ili wananchi wapate kazi, wapate fedha na waishi maisha mazuri.
Watu hawajifikirii kuanzisha miradi, biashara uwekezaji na kutafuta mitaji kwa ajili hiyo.
Mbaya zaidi watu wanafikiri hela yao ni yao, isiguswe na mtu yeyote lakini waendelee kupata huduma za bure toka serikalini.
Hili suala la TOZO ni la kulitazama kwa jicho la tatu.
Uko sahihi, je zile raslimali mnazosema tunazo mpaka wazungu watuonea wivu ziko wapi, kwanini zisiuzwe ili kutupatia fedha?
Unashangaa watu kutaka serikali itoe huduma zote, wakati kila hela za kodi zikitolewa na wananchi zinaitwa ni fedha za rais? Kwanini zisiitwe kodi za wananchi ili watu wasione Serekali ndio yenye hizo fedha?
Tozo za nini wakati viongozi wanatumia fedha za wananchi bila huruma? Kama rais alienda huko nje ambako hajapigiwa kura, akapikizwa basi na hakufa, kwanini hapa ambapo amepigiwa kura atembee na misururu mirefu ya magari kwa kisingizio cha kulinda usalama wake?