Watanzania walio wengi hawana tatizo na hizo kodi. Tatizo lipo kwa watunzaji wa hizo kodi! Wana ujanja ujanja mwingi.
Maana hao viongozi ndiyo wapigaji wakubwa wa hizo kodi zao, kupitia maisha yao ya kifahari wanayoishi, huku wale watoaji wakiishi maisha ya dhiki kubwa! Wanalazimisha wananchi masikini kulipa hizo kodi, huku wenyewe wakijipa misamaha!
Wamejaza vyeo lukuki kwenye serikali huku vikiwa havina umuhimu/ulazima wowote ule! Mfano Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Mar Das, Ma Ras, Wabunge wa viti maalum, nk!! Hawa wote wanakula mishahara na posho za bure tu! Hivyo serikali inatakiwa kupunguzwa matumizi yake yasiyo ya lazima, na ipunguze vitendo vyakevya rushwa na ufisadi ili wananchi tulipe kodi kwa moyo.
Hawana ubunifu wa kutengeneza vyanzo vipya! Na badala yake wanakata kodi mara mbili, au zaidi kwenye vyanzo vile vile! Nchi ina raslimali za kila aina! Ila karibia zote wamezibinafsisha kwa Mabeberu, halafu mwisho wa siku wanapewa mrabaha mbuzi wa 3%! Na wakati mwingine hawapati chochote!
Katika mazingira ya aina hii, kwa yeyote yule atakayepata nafasi ya kukwepa hizo kodi, akwepe tu! Maana hakuna namna nyingine ya kupata unafuu wa maisha.