Kazi ya serkali ni kubuni vyanzo vya kodi kwa kutumia rasilimali zake
Kazi ya serikali ni kuendesha taasisi zake zote ikiwemo wizara ya Elimu na Afya. Kujenga madarasa na Vituo vya Afya ni wajibu siyo 'favour' wala haiwezi kusemwa ni mafanikio! Ni wajibu wa serikali iliyopo madarakani
Watanzania wanalipa kodi kwa bidhaa zote na huduma wanazotumia.
Kukusanya kodi ni sehemu tu, matumizi ya kodi ni sehemu nyingine
Mafanikio ya kodi yanatokana na mambo mawili, kukusanya na matumizi yake. Katika nchi yetu matumizi ya hovyo yasiyo na ulazima yanagharimu serikali na mzigo huo anautwisha mwananchi kwa jina la TOZO
Waziri Nchemba kasema kuna watu 500 wanalipwa mishahara ya scale ile ile ya kuteuliwa na Rais ingawa hawafanyi kazi hizo. Haya ni matumizi mabaya ya kodi yanayolazimisha ukusanyaji kwa njia ya Tozo
Matumizi ya serikali na taasisi zake ni makubwa sana. Mbunge anajua kituo chake cha kazi ni Dodoma, ana nyumba lakini bado analipwa pesa nyingi kila akikaa Bungeni mbali ya mshahara mnono.
Ukitaka kujua kuna tatizo, piga hesababu za Taasisi ya Bunge kwa siku moja tu halafu zidisha mara vikao
Kwanini mkoa mmoja una RC mmoja, mkoa huo huo una Wabunge 7 etc?
Kama tunahitaji kodi kwanini hatupunguzi vikao vya 'Bunge' kwa siku 20 tu kwa mwaka! piga hesababu
Kwanini maafisa wanunuliwe V8 ? Kwanini wasipewe pesa za nauli na kuwe na gari chache za Idara na Wizara?
Kwanini karani ajilipie nauli ya kazini halafu alipe TOZO ya kununua V8?
Hoja si kodi au TOZO , hoja ni matumizi mabaya ya fedha yanayolazimisha serikali kutoza tu bila kuangalia namna ya kukusanya kutoka vyanzo vingine. Mfano, tuna madini ya HELIUM kule katavi yanayotafutwa duniani, nani anafikiria ni chanzo kizuri cha mapato?
Kama serikali imeishiwa mbinu, kwanini wasiache wengine wenye mawazo tofauti kama Zambia au Kenya waje na mbinu mpya! Hatuwezi kuishi kwa kukinga Bakuli ughaibuni na kuminya wauza mchicha miaka 60 ya Uhuru
JokaKuu Pascal Mayalla Tindo