Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

afadhali kufanya kazi kwa kanjibai mwishoni mwa mwez anakupa elfu 70 pilipili sado moja na kacholi 3. hawa wanasubir kuchomwa sindano za sumu kabla hawajaachiwa waje wafie tz.
 
duh kama ni uyo balaa wamekamatwa na kilo 150 za madawa zenye thamani ya bilioni 6 za kitanzania kweli walijiamini kupita na mzigo mkubwa kama huo haijawaitokea kukamatwa mzigo mkubwa kama huo huko

wasanii wetu haooo, wakija hapo oooh tuna million mia mojaa kweny accounts haya waongee na kamanda nzowaaaa
 
nami nashangaa title yake
huku kilichomo kikikanusa uhalisia wa uraia wao
cha kujiuliza hayo madawa yalipenyaje JKN airport?
jana tumeambiwa wamewakamata tena wawili wakielekea bangkong
nadhani wahusika wataanikwa,, Bil 6 sio mchezo

Nani atakae waanika? hivi huwezi jiuliza kilo 150 zimepitaje Tanzania? nijuavyo mimi hawawezi kujianika na hata wakianikwa hakuna wa kuwakamata, Mbona Rais aliwahi pelekewa list ya ma big Dealer akaaishia kusema viongozi wa dini wanafanya biashara ya madawa ya kulevya nani alikamatwa?
 

watanzania tuache ushabiki na unafiki..hao wadada wamefanya kipi cha ajabu.mbona amuongelei makontena ya pembe za ndovu yanayokamatwa kila siku na ni mali asili zetu wote..wanachukua hela ili waasi wa nchi za jirani watumie ardhi yetu.meli zinakuja kumwaga uchafu wa nyuklia ktk bahari yetu...EPA,rada na ndege ya raisi wote kimyaa....baba akiwa mlevi,mwizi na mzinzi usitegemee watoto watakuwa waungwana.ni hayo tuuu
 
Ila aiingiii akilini kwa kweli! Sasa alibeba na lift au torori huyo mtoto wa kike? Mifuko 3 ya cement jamani sio mchezo
 
Kumbe gazeti la NIPASHE lina waandishi wa habari vihiyo na ambao kazi yao ni ku copy na ku paste,hata bongo zao zimeganda,pia wahariri habari wao pia ni vihiyo,hivi kweli inakuwaje mwandishi hujidadisi mwenyewe kwanza,eti walibeba kilo 150 ,kweli kwenye ndege ya abiria mtu anaweza kubeba kilo 150 za madawa ya kulevya,hata kujihoji wenyewe wanashindwa,kwa hiyo hiyo mifuko mitatu ya sementi ilifichwa kwenye masanduku,hayo ndio matunda ya waandishi na wahariri wa vibahasha vya kaki,kazi kila kukicha kukimbilia kwenye harambee za kuchangia makanisa na kuandika habari za kusifia chama cha Mabugando.
Ningekuwa mi ndi Mzee Machache huyu mwandishi na mhariri leo hii wangekuwa wako mtaani,kwa kushusha hadhi za gazeti makini na kuwa gazeti la udaku
 
Na wewe ni wa ajabu ndio maana huoni cha ajabu kilichofanywa, hayo uliyoyazungumza kama ufisadi nk tutapambana nayo vipi wakati rasilimali watu ya kupambana na hayo ambayo kwa asilimia kubwa ni vijana ikiwa imeshaharibiwa na madawa? kumbuka mapambano yanahitaji watu wenye akili timamu sio kila mtu anaweza pambana. kwanza wengi wao wakishapiga hayo madawa wala hawakumbuki kuwa wanaibiwa tembo zao, ndio kwanza wanajiona wanaishi mainchi yaliyoendelea.
 
Majanga, majanga, majanga serikali yetu haiwezi kufuatilia hawa watoto wanapata wapi pesa kwani wao pia ni weziiiiiiiiiii, na wao wakifuatiliwa watasema hizo pesa wanazojenga majumba kila siku wanazitoa wapi???? tukianza kuchunguzana leo hii mbona majanga, majanga, majanga twende tuu mwendo mdundooo, imagine hao wadada walipitaje hapo air port DSM very stupidddd..
 

mdau ushawahi kupanda ndege[sio pw au fast jet]???
hao madada walikuwa wawili,kila mtu kabeba mabegi matatu[kuna trolley airport] do the math.....kwenye ndege kuna free 30-60 kg allowance depending on flight,sasa kwa hawa wawili inamaana wana free luggage allowance btn 60-120 depending on the flight,sasa lets assume free allowance kwa flight hii ni 45kgx2=90kg....wana 150kg-90kg=60kg....hizo 60kg WANALIPIA AS EXCESS LUGGAGE......very common kwenye ndege watu wanabeba kilo nyingi sana so hamna cha ajabu mtu kubebea 150kg kwenye ndege ya abiria......

how JKNA security couldnt detect 150kg of drugs,thats another question......
 
Kaka kuhusu kupanda sidhani PW au Fast jet zinaenda masafa marefu kwa hiyo najua ninachokisema huwezi beba hizo kilo kwenye ndege ,hapa tatizo sio kulipia au vipi bali ni jinsi ya usafirishwaji wa hizo kilo 150 .Najua hata mizigo inavyosafirishwa kwenye ndege,haiwezekani,na ndio maana hata wale wauza unga waliokubuhu hawawezi beba hizo kilo kwenye ndege za abiria bali hutumia ndege ndogo binafsi au meli /mashua zao kubeba huo mzigo
 

wewe unazungumzia ndege gani???kuna ndege wanatoa free luggage allowance 60kg....transatlantic flights,then ukiwa na extra unalipia kama excess luggage.......hao mademu walikuwa wawili hapo wanakuwa na 120kg luggage allowance,30kg wanalipia excess luggage.....bado kuna carry on unayopanda nayo ndani mwenyewe mkononi 10kg free...
hivi unajua watu wanaenda china wanarudi na nguo mzigo wa dukani kwa ndege badala ya meli???ni hivi mkienda china leets say mko wa4 kila mmoja ana free 60kg,wenzio watatu mzigo wao ni wa container unawapa hela wanakuuzia free luggage allowance yao so unakuwa na 60x3=180kg plus ya kwako 60kg total 240kg....sasa unashangaa kg 150 watu wawili???
cha muhimu begi moja mara nyingi wanaweka limit 30kg,so utabeba mabegi mengi.
 
Nimekubali mkuu. Unajua alinichanganya pale nilipoona anaendelea kupost pics instagram. Kumbe ilikuwa danganya toto.

Town hii usije ukaona jina la mtu FB au Twitter au Instagram ukajua ndio mwenyewe watu wapo kikazi zaidi
 

Bwana Irizar umeuliza swali zuri kwamba ule mzigo ulipitaje pale DAR!!!!mimi nina imani kabisa kuwa pale Dar waliuona ila wangelipua bomu wangepoteza kazi (ile sio biz ya watoto)walichofanya ni kutoa Info kwenye destination airport,ni kuwaambia namba ya ile tag inayofungwa kwenye begi maana ina maelezo yote.Juzi nilikuwa Doha nasubiri ndege ya kuja Dar,kuna vijana watatu wa TZ pia walikuwa na Sembe walikotoka walitoka salama lakini walipofika tu Doha walikuta waarabu wameshapata Info wanawasubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…