Ndio shida ya Tanzania alivyokufa huyu msanii cowobama clouds walituma haraka mtangazaji wao kule ili kusheresha umbea na kuandaa mazingira ya kutafuna rambirambi.
Lakini issue kama hii hao kina Shigongo wanaokesha usiku kucha kutafuta kufumania watu na starehe zao wanashindwa kutuma mwandishi makini na aende kule na kuja na full investigation report, na ninavyowajuwa mimi Polisi wa South Africa hawana tatizo na wanakupa faragha ya kuongea na mtuhumiwa mkiwa kwenye chumba cha peke yenu.
Kama hizi media zetu zingekuwa zinawaza sawasawa hawa watuhumiwa ni muhimu sana kuwahoji wakiwa kule kwa kuahidi kuwasaidia na ni lazima watasema then Tanzania kama Taifa mnapata kujuwa hii chain ikoje, lakini kwa ukilaza wa waandishi na hasa wamiliki wa media kwa nchi hii basi ni halijojo.
Labda tumtumie
Pasco hapa anaweza akawa na reliable source za kule South Africa atumegee taarifa maana mimi mpaka sasa hapa naona chenga tu hasa hizo kilo 150.