Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

Usiniite huku, ngoja niende MMU

There are currently 2600 users browsing this thread. (69 members and 2531 guests) kila sekunde wanaongezeka hapa mwendo wa kimya kimya
 


Tuesday, July 9, 2013 | 1:30 PM




HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..


Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE) ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik' zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.


Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.


Melezo Kwa hisani ya Nipashe.




Read more: AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI...!! - GUMZO LA JIJI
 
Ndo tatizo la kutaka kupata pesa harakaharaka, mbona kuna njia nyingi za kupata pesa kwa njia halali na kwa amani kabisa?
 
pole yao hao Wadada itafika mda watajitambua tu kuwa hii biashara ni hatari sana kilichopo ni kulizika na maisha ulionayo bila madawa maisha mazuri yanawezekana.......
 
Kwa Tanzania sijui hata kama kuna sheria.

Although rarely prescribed, methamphetamine hydrochloride is approved by the U.S. Food and Drug Administration(FDA) for the treatment of attention deficit hyeractivity disorder and obesity under the trade name Desoxyn.
Ndio shida ya Tanzania alivyokufa huyu msanii cowobama clouds walituma haraka mtangazaji wao kule ili kusheresha umbea na kuandaa mazingira ya kutafuna rambirambi.

Lakini issue kama hii hao kina Shigongo wanaokesha usiku kucha kutafuta kufumania watu na starehe zao wanashindwa kutuma mwandishi makini na aende kule na kuja na full investigation report, na ninavyowajuwa mimi Polisi wa South Africa hawana tatizo na wanakupa faragha ya kuongea na mtuhumiwa mkiwa kwenye chumba cha peke yenu.

Kama hizi media zetu zingekuwa zinawaza sawasawa hawa watuhumiwa ni muhimu sana kuwahoji wakiwa kule kwa kuahidi kuwasaidia na ni lazima watasema then Tanzania kama Taifa mnapata kujuwa hii chain ikoje, lakini kwa ukilaza wa waandishi na hasa wamiliki wa media kwa nchi hii basi ni halijojo.

Labda tumtumie Pasco hapa anaweza akawa na reliable source za kule South Africa atumegee taarifa maana mimi mpaka sasa hapa naona chenga tu hasa hizo kilo 150.
 
Huku afrika kusini Wabongo wengi wapo mitaani wakiuza madawa. Jamani watu msikimbilie afrika kusini hata nchi yeyote kama hauna complete plan of what you will do ukiwa huku. Haya si mambo mazuri. madawa yanaua watu yanavunja familia etc.
 
Ndio shida ya Tanzania alivyokufa huyu msanii cowobama clouds walituma haraka mtangazaji wao kule ili kusheresha umbea na kuandaa mazingira ya kutafuna rambirambi.

Lakini issue kama hii hao kina Shigongo wanaokesha usiku kucha kutafuta kufumania watu na starehe zao wanashindwa kutuma mwandishi makini na aende kule na kuja na full investigation report, na ninavyowajuwa mimi Polisi wa South Africa hawana tatizo na wanakupa faragha ya kuongea na mtuhumiwa mkiwa kwenye chumba cha peke yenu.

Kama hizi media zetu zingekuwa zinawaza sawasawa hawa watuhumiwa ni muhimu sana kuwahoji wakiwa kule kwa kuahidi kuwasaidia na ni lazima watasema then Tanzania kama Taifa mnapata kujuwa hii chain ikoje, lakini kwa ukilaza wa waandishi na hasa wamiliki wa media kwa nchi hii basi ni halijojo.

Labda tumtumie Pasco hapa anaweza akawa na reliable source za kule South Africa atumegee taarifa maana mimi mpaka sasa hapa naona chenga tu hasa hizo kilo 150.
kwenye hili media za Tanzania zinatakiwa zijifunze maana sidhani kma wanashindwa kumtuma mtu kwenda kuleta habari kamili kuliko kuandika tuuu.
 

Tuna shida kubwa sana inapofikia suala la investigative journalism hapa kwetu Mambo mengi huwa yanaishia kwenye anga hizi hizi za uvumi, udaku, blogu za uongo na kweli halafu mwisho wa siku habari inapotelea kizani tunaendelea na maisha kama kawaida.
Hatuna utamaduni wa kuchimbua mpaka mzizi wa mwisho kujiridhisha kuwa nini hasa kimejiri! Si mnakumbuka tulivojikanyaga msiba wa Ngwea? Hata autopsy report tu imetutoa jasho...
Immagine gazeti linachukua habari kutoka kwenye "blog" wanairusha kwenye front page live bila chenga...kuna siku wakaingizwa chaka wakaandika eti Tyson kabadili jinsia kumbe ile website ni mahususi kwa habari za kupika....aibu ilioje!
Hivi sasa tunajadili ishu hii lakini hakuna hata mwandishi aliyepiga simu huko SA kuongea na polisi huko au japo balozi kuthibitisha kuwa kuna wabongo wamekamatwa? Are we really serious?? tumekalia umbeya tuu humu jf na kwingineko
 
huyu kumbealikuwa container ya kubeba mizigo daaa bora ange endelea kupiga zile picha zake na kuziuza.
 
These are too young.....ni wao au wanatumiwa? Zimepitaje hapa kwetu?
 
Who is behind this? Any connection with dearth of Ngwair(R.I.P)??

Sasa ngwair kaingiaje hapa?!huwezi kuongelea poda bila kumtaja ngwair?let him RIP bwana!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
huyu kumbealikuwa container ya kubeba mizigo daaa bora ange endelea kupiga zile picha zake na kuziuza.
Kama Mamlaka za Tanzania na vyombo vya habari vinachukulia jambo hili kimzaha basi tujiandae na janga kubwa sana mbele ya safari.

Kwanza kibano cha kwanza kianzie hapa kwetu waliwezaje kutoka na shehena yote hiyo? maana ninavyofahamu mimi biashara ya unga inasafirishwa kwa njia ya tumbo ndio njia salama iliyobakia (ingawa ni risk ya uhai wako)

Kama watu wanaweza kupita madawa kwa njia ya pecking mimi hili haliniingi akili hata kidogo kwa sababu najuwa know how za biashara hii.

Something wrong somewhere na msitalajie lolote kutoka ubalozi wa Tanzania pale Pretolia, wamejaa vilaza watupu kuna siku nilitaka kumtandika makofi Dada mmoja wa kibongo anafanya kazi pale ubalozini baada ya kuniletea majibu ya Manzese wakati yeye yuko pale kwa ajili yetu.
 
Back
Top Bottom