Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 9,626
- 6,731
Dawa ya hawa ni kunyonga ama kuwachoma moto ili liwe fundisho kwa wenzao kwani hawa ndiyo wanaoangamiza jamii bila hata huruma, kwanini tuwaonee huruma wao?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo tatizo la kutaka kupata pesa harakaharaka, mbona kuna njia nyingi za kupata pesa kwa njia halali na kwa amani kabisa?
Jamani hebu twende taratibu....
Hivi mnafahamu kilo 150 ni sawa na mifuko mitatu ya Cement? hakuna kitu kama hicho katika biashara ya usafirishaji unga kwa njia ya kupanda nao kwenye ndege.
Watanzania tujaribu kuwa na akili za udadisi kidogo, hata hao wanaomeza tumboni mtu anayejitahidi sana umeza kilo moja tu ya unga ambayo inakuwa kwenye vipipi. Huu ni uongo wa mchana.
Kama kungekuwa na unga wa uzito wa kilo 150 basi ungetumika usafiri wa baharini au kwa gari, tusipende kulishwa habari za uongo uongo tu.
usiniudhi...nimeweka thread yenye akili kuhusu hiyo kitu red hapo mods wameifukia wanaisoma wao tu na mademu zao na watoto wao.....hawakutaka mpate madini....
Tuna shida kubwa sana inapofikia suala la investigative journalism hapa kwetu Mambo mengi huwa yanaishia kwenye anga hizi hizi za uvumi, udaku, blogu za uongo na kweli halafu mwisho wa siku habari inapotelea kizani tunaendelea na maisha kama kawaida.
Hatuna utamaduni wa kuchimbua mpaka mzizi wa mwisho kujiridhisha kuwa nini hasa kimejiri! Si mnakumbuka tulivojikanyaga msiba wa Ngwea? Hata autopsy report tu imetutoa jasho...
Immagine gazeti linachukua habari kutoka kwenye "blog" wanairusha kwenye front page live bila chenga...kuna siku wakaingizwa chaka wakaandika eti Tyson kabadili jinsia kumbe ile website ni mahususi kwa habari za kupika....aibu ilioje!
Hivi sasa tunajadili ishu hii lakini hakuna hata mwandishi aliyepiga simu huko SA kuongea na polisi huko au japo balozi kuthibitisha kuwa kuna wabongo wamekamatwa? Are we really serious?? tumekalia umbeya tuu humu jf na kwingineko
Sihitaji madhara ya madawa hayo labda utakuwa msaada kwangu kama unaweza kunipa orodha ya madawa yaliyopigwa marufuku na mengine yameruhusiwa kwa kibali maalum, bado hujajuwa mimi nitafuta nini hasa kwa kuuliza hizi information, haya mambo mengine unaweza kukuta hata hawa waliokamatwa hawajui walibeba, am just thinking....
Mimi nimekaa na wauza unga wakongwe na process zote mpaka wanavyomezeshana vipipi nafahamu, lakini aina hii ya madawa kilo 150 hili ni jipya kwangu, kwa sababu ninavyofahamu mimi kuna madawa yapo hospital lakini ni marufuku kuwa nayo mtu binafsi.
Mimi nimejaribu kwenda mbele zaidi ya hapo unapofikiri wewe, kama ni madhara hata pombe za mataputapu na gongo pia vina madhara.
umenena wangefaulu hawa wote tungewasifia kama wamefanikiwa kimaisha na kuwapa sifa mbali mbali bila ya kujali wanachofanya na najiuliza hivyo inakuwaje mzigo mkubwa hivi haujaonekana JNIA???????Kwa ukubwa huo wa mzigo, kwa vyovyote kuna system ambayo imekuwa ikifanikisha zoezi mara zote ila wakati huu mambo yameenda ndivyo sivyo, labda kwa kusalitiwa ama vinginevyo...kina dada kazi yao ilikuwa ni kusindikiza tu.
Any way kufa siku moja, kuzaliwa siku moja.....wanapofanikiwa ni sisi sisi hujikuta tukiwaabudu, na wala tusingejali wametoa wapi hiyo mihela.......sasa kwa kuwa dili imebuma tutaanza kuwazodoa.
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!usiniudhi...nimeweka thread yenye akili kuhusu hiyo kitu red hapo mods wameifukia wanaisoma wao tu na mademu zao na watoto wao.....hawakutaka mpate madini....
enewei mods endeleeni kusoma thread yangu ile muikariri muje muwadithie mademu zenu.....
aiseee hii shori aisee
![]()
Kwa hali halisi ya mtandao wa madawa ya kulevya wahusika hawawezi kupatikana kitakachofanyika kama sio kuwaokoa hao waliokamatwa basi ni kuhakikisha hawafikii hatua ya kutaja nikimaanisha watauliwa kabla.
South Africa hiyo network ipo, niliwahi kukaa Flat moja na Wanigeria Cape Town, hawa jamaa ni hatari kuliko maelezo wamepenya wanawatumia mpaka cabin crew wa International flight
Kutokana kuwa na uchumi mkubwa hawa jamaa kwanza huwawinda kimapenzi na wakishakuwa wapenzi uwashawishi kuingia kwenye biashara hii, kwakweli kama roho yako ndogo ni lazima uingie kwenye hii biashara na hasa ukiona maisha wanayoishi hawa watu na magari wanayoendesha wakiwa nchi ya kigeni.
Kuna kipindi soko la white suger lilivuma sana Australia ilikuwa unaruka ndani ya wiki umeshageuka na una dolali zako za kutosha, wale Wanigeria waliposhindwa kuniingiza kwenye biashara hii sasa naweza kuthubutu kusema siwezi kufanya hii kitu, nina option nyingi sana za kupiga pesa.
Lakini mtu mwenye Passport ya Tanzania anayethubu kubeba unga ni mjinga kabisa, Passport ya Tanzania ni kimeo kupita maelezo, mimi nimeshawahi kukaa Airport mpaka ndege tatu zimeshusha na abiria wametoka arrival lounge mimi bado nasachiwa tu lakini abiria wengine niliokuwa nao ndege moja hawakusachiwa.
Hii ni just a Trailer tu subulini Switzerland nako kisanuke ndio mtaipata habari yenyewe, kule wadada wa kibongo wamejaa kibao na biashara ni sembe tu, unajuwa ile siyo ya kupiga box.
Kwa hali halisi ya mtandao wa madawa ya kulevya wahusika hawawezi kupatikana kitakachofanyika kama sio kuwaokoa hao waliokamatwa basi ni kuhakikisha hawafikii hatua ya kutaja nikimaanisha watauliwa kabla.
Huku afrika kusini Wabongo wengi wapo mitaani wakiuza madawa. Jamani watu msikimbilie afrika kusini hata nchi yeyote kama hauna complete plan of what you will do ukiwa huku. Haya si mambo mazuri. madawa yanaua watu yanavunja familia etc.
Kama ni kweli pole sana Agnes😡
Hivi tanzania agness gerard ni mmoja tuu hamna wengina nan anapicha za usibitisho kuwa ni huyo video qeen...nawasilisha
Usiharibu majina ya watu, drug dealer habebi mzigo, hawa wanaitwa containers.