Watanzania wengi hawaogi na hawapaki deodorant

Watu wachafu watakuja kumtetea
 
[emoji23][emoji23] hatari mnoo
 
Huu uzi una serious jokes....
Nimecheka hizi koments ingawa hazijaandikwa kwa lengo la jokes lakini upande fulani ni jokes hahaaa
 
Mapuani kuna nini sijaelewa hapo
 
🤣🤣🤣🤣🤣unataka anayebeba zege, machinga, mama ntilie, fundi gereji, na fundi welding, selemara, mvuvi, muuza samaki, ndugu zangu wagogo Hapo mazizini wapake, sijui wapulizie hiyo deodorant??
Hahahahaah
 
Kuna sehemu hauwezi kuingia kama sio msafi unanuka. By the way, usafi ni mojawapo ya masomo ya kufundisha shule ya msingi mfululizo madarasa yote hadi mtoto ana graduate.
 
Wewe utakuwa Bashite
 
Kuna sehemu hauwezi kuingia kama sio msafi unanuka. By the way, usafi ni mojawapo ya masomo ya kufundisha shule ya msingi mfululizo madarasa yote hadi mtoto ana graduate.
Mfano wa sehemu ambazo mtu mchafu hawezi kuingia ni zipi mkuu?
 
Haya mambo ya usafi wa mwili na kunukia harufu nzuri kwa mtu binafsi kiasi cha kutungiwa sheria huwa yanawezekana kwa nchi ndogo ndogo duniani na kwenye majimbo yanayojiamulia kujitungia sheria zao za ajabuajabu. Wengine hufanya hivyo ili kuvutia watalii kutembelea nchi zao, tena wanaenda mbali zaidi kuweka sheria ni marufuku kununanuna, mwendo ni tabasamu tu. Ili la kuoga na kupaka manukato bongo ni zoezi gumu kutokana na aina ya maisha na kazi wanazozifanya wabongo wengi. Kula ni lazima kuoga ni hiari
 
Wataoga tu, ilimradi sheria itungwe
 
Kuoga kuanzie kwa wanandoa, unakuta wanandoa hawaogi wananuka uvundo, mke hajali usafi wa mume wake, kazi kubwa mojawapo ya mke ni kuhakikisha mume wake ni msafi ameoga. Unakuta wanandoa wananuka miili yao na midomo unajiuliza hivi wanapeanaje majamboz wakiwa wananuka vibaya hivyo?
 
Mkuu kupaka hizo mambo ulizosema si lazima kabisa mimi mwenyewe sipaki kabisa nimetoka zangu kuoga napaka mafuta yangu ya nazi nakuwa nimemaliza shughuli
 
Mtu mzima utamshikia bakora akaoge? Mnapenda kusingizia wanawake Mme asipooga mkewe wakati maji yapo amegoma kuoga iweje shida iwe kwa mkewe [emoji43][emoji43][emoji43]

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…