Watanzania wengi hawaogi na hawapaki deodorant

Watanzania wengi hawaogi na hawapaki deodorant

Yani ni tatizo aiseh.... Kuna siku nkipanda daladala zinazoenda umbali mrefu... Akapanda baba mmja kananyua mkono kushika chuma maan alikua kasimama..... Ehh kumchek kweny kwapa nywele zimeota zimekua nyingi alaf kumejaa ukoko mweupe.... Nlicheka hyo siku Aecha kabisa
Watu wachafu watakuja kumtetea
 
Yani ni tatizo aiseh.... Kuna siku nkipanda daladala zinazoenda umbali mrefu... Akapanda baba mmja kananyua mkono kushika chuma maan alikua kasimama..... Ehh kumchek kweny kwapa nywele zimeota zimekua nyingi alaf kumejaa ukoko mweupe.... Nlicheka hyo siku Aecha kabisa
[emoji23][emoji23] hatari mnoo
 
.
Screenshot_20220723-202423_1.jpg
 
Huu uzi una serious jokes....
Nimecheka hizi koments ingawa hazijaandikwa kwa lengo la jokes lakini upande fulani ni jokes hahaaa
 
Ila ni aibu sana...nina mgonjwa hii week ya pili...... Yani watu ninaopishana nao hospital asubui najiuliza hivi huyu kaoga au..... muda mwingi sana watu wanafundisha kutumia limao kweny kwapa , unanyoosha ka nguo vzuri, unavaa..... Sasa asubui unakutana na mdada ananuka jasho alf ukimsalimia anaitikia mapuani khaaa[emoji28]
Mapuani kuna nini sijaelewa hapo
 
Kuna sehemu hauwezi kuingia kama sio msafi unanuka. By the way, usafi ni mojawapo ya masomo ya kufundisha shule ya msingi mfululizo madarasa yote hadi mtoto ana graduate.
 
Heri ya sikukuu ya sabasaba.

Kwa masikitiko makubwa naomba niwakilishe malalamiko yangu kuhusu ndugu zangu na wananchi wenzangu. Wengi wenu hamuogi, hamfui nguo zenu na hampaki deodorant achilia mbali perfume.

Jana nilikua kwenye misongamano ya watu sehemu mbili tofauti katika jiji la Dar es Salaam, yaani uvundo na harufu mbaya za watu karibu zinifanye nihairishe safari zangu. Imagine unakwenda kumuangalia mgonjwa kwenye wodi ya hospitali ya Muhimbili, kwenye ngazi unapishana na kundi la watu wanaonuka mchanganyiko wa harufu mbaya zenye kustaajabisha.. Halikadhalika, mikusanyiko ya watu kama kwenye maonesho ya sabasaba unaweza kuchefukwa na harufu mbaya za watu na ukastaajabu..

Kwa maoni yangu, sehemu kubwa ya watu hawa hawaogi, hawafui nguo zao, wana magojwa ya fungus miguuni, hawapaki deodorant au manukato.

Nini kifanyike?

1. Elimu ya usafi wa mwili itolewe kuanzia shule za chekechea mpaka vyuoni. Raia wafundishwe umuhimu wa kuoga na kupaka deodorant. Waeleweshwe kwamba kutofanya hivyo ni ukatili kwa wengine kwani kunawasababishia maumivu ya kiakili na kero kubwa;

2. Watu wasiooga au kupaka deodorant wakibainika watozwe fine kwa uchafuzi wa mazingira na kusababishia raia wengine kero na maumivu ya kiakili; na mwisho

3. Wasiruhusiwe kuja mjini.

Namshukuru mkuu wa mkoa mstaafu bwana Paul Makonda aliwahi kulishughulikia ili swala, natumaini Raisi wangu msikivu atalishughulikia pia.

Naomba kuwasilisha
Wewe utakuwa Bashite
 
Kuna sehemu hauwezi kuingia kama sio msafi unanuka. By the way, usafi ni mojawapo ya masomo ya kufundisha shule ya msingi mfululizo madarasa yote hadi mtoto ana graduate.
Mfano wa sehemu ambazo mtu mchafu hawezi kuingia ni zipi mkuu?
 
Haya mambo ya usafi wa mwili na kunukia harufu nzuri kwa mtu binafsi kiasi cha kutungiwa sheria huwa yanawezekana kwa nchi ndogo ndogo duniani na kwenye majimbo yanayojiamulia kujitungia sheria zao za ajabuajabu. Wengine hufanya hivyo ili kuvutia watalii kutembelea nchi zao, tena wanaenda mbali zaidi kuweka sheria ni marufuku kununanuna, mwendo ni tabasamu tu. Ili la kuoga na kupaka manukato bongo ni zoezi gumu kutokana na aina ya maisha na kazi wanazozifanya wabongo wengi. Kula ni lazima kuoga ni hiari
 
Wataoga tu, ilimradi sheria itungwe
 
Kuoga kuanzie kwa wanandoa, unakuta wanandoa hawaogi wananuka uvundo, mke hajali usafi wa mume wake, kazi kubwa mojawapo ya mke ni kuhakikisha mume wake ni msafi ameoga. Unakuta wanandoa wananuka miili yao na midomo unajiuliza hivi wanapeanaje majamboz wakiwa wananuka vibaya hivyo?
 
Mkuu kupaka hizo mambo ulizosema si lazima kabisa mimi mwenyewe sipaki kabisa nimetoka zangu kuoga napaka mafuta yangu ya nazi nakuwa nimemaliza shughuli
 
Kuoga kuanzie kwa wanandoa, unakuta wanandoa hawaogi wananuka uvundo, mke hajali usafi wa mume wake, kazi kubwa mojawapo ya mke ni kuhakikisha mume wake ni msafi ameoga. Unakuta wanandoa wananuka miili yao na midomo unajiuliza hivi wanapeanaje majamboz wakiwa wananuka vibaya hivyo?
Mtu mzima utamshikia bakora akaoge? Mnapenda kusingizia wanawake Mme asipooga mkewe wakati maji yapo amegoma kuoga iweje shida iwe kwa mkewe [emoji43][emoji43][emoji43]

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom