Tatizo si elimu wala njaa au stress, tatizo kubwa walilonalo watanzania wengi hawana maudhui (content), hawana hoja za kuleta kwenye mijadala na mazungumzo ya kawaida. Ili uwe na hoja ya kupinga au kukubaliana na jambo fulani LAZIMA UWE NA MAUDHUI (CONTENT), kama huna content huwezi kuwa na hoja ya kukubaliana au kupingana na kilichopo mezani. Matokeo yake utaanza mashambulizi binafsi, kupaza sauti na kuwa defensive badala ya kujadili hoja. Kuna watu wana elimu sana na wana maisha bora kiuchumi, wakiwemo wanasiasa, watendaji wakuu serikalini lakini hawana content, hawawezi kushiriki mijadala yoyote mizito au kujibu hoja zozote nzito kwa kuwa hawana hoja za kuongea. Matokeo yake wanapatwa na frustrations na kuanza aidha kutoa vitisho, kumshambulia mtoa hoja, kufoka, au kukimbia. Ndiomaana walio wengi ni wepesi sana kujiingiza kwenye mijadala au matukio yasiyo na maana. Wabongo tujifunze jinsi ya kuwa na content ili tuweze kuchangia au kujenga hoja kwenye mazungumzo au mijadala na watu. Kama kuna mtu amesema jambo usilokubaliana nalo, kwa mtu mwenye content hawezi kupayuka, atatulia, atasikiliza hoja na anaweza kutofautiana na mhusika kwa njia za kiistaarabu.
Bado unaweza kuwa una stress zako, una njaa zako lakini kama una content huwezi kuwa kituko.