Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa wake wanaodhani kuwa kudhibiti vyombo vya habari kuripoti habari za wapinzani kutawasaidia, wajue tu wanajidanganya kwani hivi sasa watanzania wengi wanamiliki smartphone hasa maeneo ya mijini, hivyo watazitumia kupashana habari za uchaguzi zikiwemo habari za wapinzani.
Lissu kasema wametishwa kuripoti habari zake na kwamba wanamuogopa mtu mmoja ila akaongeza kuwa ,watu sasa watutimia WhatsApp kupashana habari za uchaguzi.
Ukweli ni kwamba,Lissu kataja WhatsApp kama mfano tu, ila watu watatumia Facebook,Instagram, Twitter na mitandao mingine kama huu wa JamiiForums kusambaza na kupashana habari za nini kitakachokuwa kinajiri kwenye mkutano ya kampeni ya wapinzani hata kama watu wa TV na magazeti hawataripoti.
Uzuri wa haya mambo ni kuwa,watu wakipuuza hizi media,hata like kitakachokuwa kinaripotiwa na hizi media pia nacho kitapuuzwa, hivyo wataopata hasara ni hao watakaokuwa wanategeme hizi media ziwabebe.
Wao waendelee tu kujidanganya wakati watu Siku hizi wameanza kutegemea social media zaidi kama chanzo cha kupata habari huku mainstream media zikibaki kutumika kwakuwa tu ziko majumbani mwetu.
Siku hizi watu wanasikiliza habari kwenye tv huku teyari wana taarifa za matukio karibu yote ya siku husika tena taarifa hizo wakizipata pasipo kuchujwa ili kumsitiri mtu au kuficha baadhi ya mambo.
Mfano mzuri ni ujio wa Lissu ambao ulitangazwa zaidi kupitia social media lakini karibu kila mtu alikuwa na taarifa na alipokelewa na watu wengi utadhani tukio husika liliitangazwa na vyombo vikubwa vya habari mwezi mmoja kabla.
Labda yule Malaika wa kuzima mitandao ashuke ndio itakuwa ponepone yao ingawa nae anaonekana kukwama huko mawinguni.
Imekula kwao mwaka huu.